MAVAZI KATIKA OFISI ZA UMMA-UTUMISHI WATOA MWONGOZO

Wizara ya utumishi wa umma imetuma waraka unaotoa mwongozo wa mavazi kwa watumishi wote wa ofisi za umma na wananchi wote wanaohitaji huduma ktk ofs hizo.
Waraka huo namba 3 wa mwongozo wa mavazi wa mwaka 2007 unawatka wafanyakazi wote wa ofisi za umma na wananchi wote kutokuvaa mavazi yafuatayo:-
-Jeans
-Nguo zenye maandishi yoyote
-Nguo zinazobana mwili wako
-Nguo zilizo juu ya magoti (sketi/gauni)
-Kaptula
-Pedo
-Jezi za timu za mpira
-Nguo za chama chochote cha siasa
-Suruali ambazo hazijapindwa
-Blauz zinazoacha kifua/mgongo wazi
-Kuvaa mlegezo
Waraka huo ulikuwepo ila uekelezaji haukufanyika,hivyo kwanzia mwaka huu utaanza kutumika nchi nzima.
Wananchi usiende ofisi za umma ukiwa umevaa mavazi tajwa hapo juu,utaishia kufukuzwa bila kuhudumiwa...

NINI MAONI YAKO?
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Eti suruali ambazo hazijapindwa, jeans, bora wangesema nguo zisizositiri mwili.Hivi kuna mtu anavaa suruali za kupinda sasa hivi?mbona ni style ya mwaka 47.Jeans ni vazi la Europe tunavaa kanisani, maofisini, na kwenye occasion mbalimbali.Kwann wabongo mnaliona halifai?

    ReplyDelete
  2. Naomba nifahamishwe sababu tatu zinazosababisha jeans kupigwa marufuku, ikizingatiwa jeans ni mojawapo ya nguo kama kodrai, na kadet, smahani kiingereza sijui vizuri lakini nadhani nimeeleweka

    ReplyDelete
  3. Mdau wa 4.45am Europe hawaruhusu kuvaa jeans ofisini labda ukienda kubeba box

    ReplyDelete
  4. Nimeipenda hii system

    ReplyDelete
  5. mdau 5.45 europe hipi hawaruhusu jeans ofisini

    ReplyDelete
  6. hIzo ni kelele za kila siku tushazizoea ila kikubwa tufanye kazi kwa bidii Serikali inasema (BIG RESULT NOW ) ionekane sasa sio kuangalia mtu kaingiaje ofsn mara katokaje yote ya nn?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad