MCHUNGAJI GWAJIMA AVAMIWA NA MAJAMBZI USIKU NA KUNUSURIKA KUUAWA MARA TATU

ILITOKEA lakini haikuandikwa kwa sababu haikudakwa! Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lenye makazi yake kwenye Viwanja vya Tanganyika Perkas, Kawe jijini Dar, Josephat Gwajima alinusurika kuuawa mara tatu kufuatia kuvamiwa na majambazi watatu mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumzia suala hilo hivi karibuni, Gwajima alisema tukio hilo lilijiri nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini Dar ambapo siku ya kwanza, majambazi hao waliingia nyumbani kwake saa nne usiku wakiwa wameficha sura na kumkuta yeye sebuleni ambapo walimuuliza, ‘Gwajima yuko wapi?’
“Ni kweli nilinusurika kifo na majambazi, walinivamia mara tatu nyumbani. Zilikuwa siku mbaya maishani mwangu. Siku ya kwanza walikuja na bunduki huku wameficha sura, walinikuta sebuleni, wakaniuliza alipo Gwajima, niliwajibu ametoka, wakaondoka wakisema watarudi kesho yake.
“Nilijua ni utani, lakini kweli siku iliyofuata saa nne usiku walikuja tena, wakanikuta ndiyo naingia nyumbani, wakaniambia niko chini ya ulinzi, nilimuomba Mungu aokoe maisha yangu kwani nilipatwa na mshtuko, wakahoji; ‘Gwajuma yuko wapi?’ Kabla sijajibu mmoja akasema; ‘huyu bwana mdogo ndiye tuliyemkuta jana,’ wakaondoka.
“Sikuwa na wazo la kuripoti polisi ila nilimwamini Mungu aliye hai. Siku ya tatu walipitia juu ya paa kwa kung’oa vigae na kushukia chumbani wakiwa na bunduki.
“Mimi nilikuwa kitandani na mke wangu, wakauliza tena Gwajima yuko wapi? Nikawajibu bado hajarudi, wakasema; ‘haka (Gwajima) ndiyo kale kale ka bwana mdogo ka jana.’
“Mungu mkubwa, kwa nje zilisikika kelele za mbwa kisha wakatoweka ghafla, niliona ni siku za majaribu kwangu, nilimwomba Mungu atupilie mbali majaribu yale, baada ya siku kadhaa niliamua kuhama kwenye nyumba ile.
“Ila nakumbuka ile siku ya mwisho walisema tunamtaka Gwajima kwa sababu anajifanya kufufua misukule kisha anataja majina yetu.
“Ndipo nilijua kumbe kisa ni kufufua misukule. Najua umbo langu ndiyo mkombozi wa yote kwani waliponiona walijua Gwajima hawezi kuwa na umbo dogo kama mimi nilivyo,” alisema Gwajima.
Katika mahojiano marefu na gazeti hili, mchungaji huyo alisema kuwa mpango wa kumuua uliofanywa na mtu ambaye aliwahi kutajwa jina na binti msukule aliyemfufua kanisani kwake. Alisema mtu huyo aliyetajwa na msukule ni  mtumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (jina hakumtaja).

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Aaaaaa huu uongo WA mchana kweupe

    ReplyDelete
  2. acha uongo sema tu unataka waumini kanisan kwako waongezeke ili makusanyo ya sadaka yaongezeke...
    unadhani si wajinga kihivyo we unavyo fikiri wewe??????

    ReplyDelete
  3. Ina maana hao majambazi walienda kuua mtu wasiyemjua? Inawezekanaje? Hiyo siku ya tatu waje wabomoe vigae hadi kuingia ndani ndo mbwa waanze kubweka kweli? Dah sielewi elewi hapa juu ya hili

    ReplyDelete
  4. Hawa ndo wale manabii feki wapotee gafla coz kelele za mbwa huYo mbwa alkua wap mda wote wanaingia getin na kutoa vigae

    ReplyDelete
  5. sasa watumishi wa mungu mmezidi uogo ww uvamiwe mara 3 bado umekaa vyombo vya usalama ww unahisi kazi yak ni ipe

    ReplyDelete
  6. Hivi huyu ni mtumishi wa Mungu kweli?!?!

    ReplyDelete
  7. Local promo
    Usually businesses requires advertisements
    Mtumishi sisi watu wazima tuna akili

    ReplyDelete
  8. Uongo mtupu,sijashangaa kwn Gwajima nakujua vzur sn km Tapeli na nliacha sali kwko baada y kugundua uchawi wko,na pia ulivokua unamtaka shoga yngu Rhoda,hips zilikuchanganya

    ReplyDelete
  9. Gwajima acha uwongo ww kwanini unakuwa muongo ebu jieshim utaeshimika

    ReplyDelete
  10. kama wangekua wanatoa mataji ya uongo nahs we ungeongoza kwa kuchukua yote

    ReplyDelete
  11. BABA ACHANA NA KUJIELEZEA SANA KWENYE VITU KAMA HIVI,BLOGS.NAKUFAHAMU NA NIMESIMAMA NA KUJUA KWELI BAADA YA KUSALI KWAKO HAO WANAO COMMENT VIBAYA HAYAJAWAPATA YAMKINI WAMECHUKULIWA PIA

    ReplyDelete
  12. MAFUNDISHO YAKE YA KUIBIWA NYOTA,ADUI WAKO NI YULE WA NYUMBANI MWAKO,SOMO LA MTUPE NJE,JINSI WACHAWI WANAVYOFANYA NA NI VIPI TUPAMBANE NAO ,MAJESHI YA BWANA ,YOUR VISION AND OTHERS OOH BE BLESSED SENIOR PASTOR

    ReplyDelete
  13. YOUR A HUMAN BEING AND HANDSOME ,KAMA HATA MFALME DAUDI ALIMTAMANI MKE WA HURIA WHO ARE YOU NOT TO BE ATRACTED BY WOMEN,YOU KNOW HOW TO REPAINT PASTOR IF POSSIBLE STOP INVOLVINTG IN THIS

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad