MFANYABIASHARA WA KIKE APIGWA RISASI USONI NA KUPORWA MABEGI MAWILI YA HELA KARIAKOO

Damu ya Mfanyabiashara huyo ikiwa imetapakaa katika gari lake baada ya kupigwa risasi na majambazi waliompora kiasi kikubwa cha fedha na kutoweka.
Mfanyabiashara mmoja (Jina Halikufahamika) Mwenye asili ya Asia ameshambuliwa na majabazi (majira ya saa 12 Kasoro jioni )kwa kupigwa risasi katika paji la uso wake na kisha majambazi hao kutoweka na mabegi mawili yaliyoojaa fedha.
Hata hivyo haikujulikana kwa haraka ni kiasi gani cha fedha ambacho kilikuwemo katika mabegi hayo. Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya mashuhuda wa tukio walidai kuwa majambazi hao walikuwa  watatu na mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG

Wakielezea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara wengine katika maeneo hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo (Kariakoo) walidai kwamba Mfanyabiashara huyo alitoka na kufunga duka lake huku akiwa na mabegi mawili na Mashine ya kutolea Risiti ya EFD na kuelekea katika gari lake dogo aina ya Suzuki Carry na Ghafla walitokea watu wawili waliokuwa katika pikipiki na mmoja wa tatu alikuwa amesimama pembeni kidogo na gari hiyo na kisha kuelekea moja kwa moja katika gari hiyo na kumpiga risasi mfanya biashara huyo aliyekuwa akijiandaa kuondosha gari lake.


Hata hivyo baadhi ya watu wamelaumu utaratibu wa wafanya biashara wengi wa kariakoo kuhifadhi fedha nyingi katika maduka na badala yake wamewataka wafanya biashara hao kutafuta mbinu mbadala itakayowaezesha kuweka fedha na mali zao salama kabisa ikiwa ni pamoja na kutumia huduma za kuhamisha fedha kwa kutumia mitandao, cheque, na hata credit card kuliko Cash kwani imekuwa kawaida kwa mtukio haya kujirudia eleo hili la Kariakoo.

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tukio la kwanza kumkaribisha IGP mangu hilo...!!

    ReplyDelete
  2. Tatizo la wafanyabiashara wengi ndio hilo, yaani cashier ndio yeye, muhasibu ndio yeye, dereva ndio yeye yaani anahodhi nafasi zote mwenyewe.

    ReplyDelete
  3. udaku specially acheni uongo aliyefariki ni kaka cio dada...kwa udhibitisho zaid ni mdogo wa boss wa company yetu hata leo hatujaingia kwa ofice plz muwe mna collect news vizuri cio kupotosha watu jamaniiiii..............

    ReplyDelete
    Replies
    1. kama wewe unajua vizuri habari hii si ungeitoa mapema au ulisubiri mtu atoe uanze kukosoa.mnafki mkubwa we!

      Delete
  4. Udaku kuma mako kwa habari za uongo mbona mnahabari za kisenge

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwani ulilazimishwa usome? Kipapa chako cha nyuma

      Delete
    2. Acha kutukana wewe. hapa tunafata habari na habari ni yakushtua cyo ya kimbeya. kibinadam ukiona the heading lazma usome. sasa huyo bwana ako anaandika uongo akiambiwa unakuja juu.

      Delete
  5. Jamani ni kaka aliepigwa siyi dada

    ReplyDelete
  6. Jamani huko bongo kuna tisha hivi ina maana polisi wameshindwa kuanzisha operation tokomeza ujambazi?kuwafahamu majambazi ni rahisi sana mbona hawachukui hatua?au wanakula nao?watalii wengi wanapenda kwenda africa ila matukio kama haya yanakatisha tamaa.Tanzania hakuna amani tena

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad