MGOGORO MZITO MIRATHI YA MAREHEMU MOSES KULOLA

Stori: Waandishi Wetu
HALI ni tete! Familia ya aliyekuwa muasisi wa imani ya kilokole nchini na Askofu wa Kanisa la Evangelist Assembles of God Tanzania (EAGT), marehemu Dk. Moses Samuel Kulola (83), inadaiwa kuingia kwenye mgogoro mzito wa usimamizi wa mirathi ya mali alizoziacha kiongozi huyo.

CHANZO?
Ilidaiwa kuwa gogoro hilo limekuja baada ya mtu mmoja kuibuka na kudai yeye ndiye msimamizi halali.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya mazishi ya marehemu Kulola miezi mitano iliyopita, familia ilikaa kikao na kufuata taratibu za mirathi kwa kuzingatia wosia wa marehemu  ambapo mjane wa marehemu, Elizabeth Kulola ndiye aliyetakiwa kuwa msimamizi.

KATUNZI
Habari zinapasha kwamba wakati familia hiyo ikiwa katika msimamo huo ghafla aliibuka mtu aitwaye Florian Katunzi ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la EAGT City Center, Temeke jijini Dar na kudai kuwa ndiye mrithi wa mali kisheria kwani marehemu Kulola alimweka kuwa msimamizi. 
Ilidaiwa kuwa, Katunzi alisema ana maandishi halali ya tamko na wosia wa marehemu mzee Kulola.

TAHARUKI
Chanzo chetu kiliendelea kutiririka kuwa, wanafamilia walijikuta wakitaharuki na kupigwa butwaa kuhusu jambo hilo ambapo walimuomba Katunzi awaoneshe wosia huo lakini alikataa katakata na kuamua kuufikisha mahakama moja ya mwanzo ya jijini hapa.
Ilibidi familia ilivalie njuga suala hilo hasa wakitaka kuuona wosia huo mpya jambo ambalo walifanikiwa.

PINGAMIZI
Habari kutoka ndani ya familia ya marehemu Kulola zinasema kuwa baada ya kuuona wosia huo, Septemba 29, mwaka jana, wanafamilia hao waliweka rasmi pingamizi kwa kile kilichodaiwa kuwa, ulikuwa na makosa mengi, ikiwemo tofauti ya ukubwa wa mihuri iliyopigwa kwenye ukurasa wa kwanza na wa pili kutoka mwisho


Pia familia ilibaini tofauti ya saini za marehemu Kulola katika kurasa mbili, uwepo wa mashahidi wakati wosia huo ukisainiwa, uwepo wa watu ambao hawahusiki na mirathi hiyo kama vile Msimamizi Mkuu wa Huduma ya Ushauri Kibiblia na Maombezi (BCIC), Askofu Sylvester Gamanywa.

Kubwa zaidi, ilielezwa kuwa familia ilibaini kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa katika mahakama ya mwanzo kinyume na sheria ya mirathi ya mwaka 1984 inayotoa mamlaka kwa  mahakama ya hakimu mkazi pekee.


MZEE WA UPAKO
Hata hivyo, kabla patashika hilo kuchukua sura katika familia hiyo, Mchungaji Katunzi na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Lusekelo Anthon ‘Mzee wa Upako’ nusu washikane mashati baada ya Katunzi kumfuata mwenzake akitaka rambirambi aliyoahidi kuitoa wakati wa kifo cha mzee Kulola.
Siku hiyo Mzee wa Upako aliahidi kutoa rambirambi ya shilingi milioni 15 akimzidi mwenzake, Mchungaji Joseph Gwajima aliyetoa shilingi milioni 10. 
Inaelezwa kuwa,  Mzee wa Upako alikuja juu akimuuliza Katunzi kwamba anadai kama nani katika familia ya marehemu.

MJANE WA KULOLA
Akizungumza na waandishi wetu kwa majonzi huku akiangua kilio mara kwa mara nyumbani kwake, Capripoint jijini hapa, mke wa marehemu, Elizabeth alisema amemwachia Mungu mambo yote na kuongeza kuwa jambo hilo linamuumiza na kumfanya akumbuke enzi za uhai wa mume wake.
Alisema kuwa mumewe alimwambia akifa watu wengi waliokuwa karibu yake watamkimbia na marafiki kugeuka maadui hivyo hashangai kinachotokea sasa.

Akizungumzia uhusiano kati ya Katunzi na marehemu Kulola, mama Kulola alisema marehemu hakuwa na uhusiano na Katunzi kiasi cha kufikia kumwamini katika suala nyeti la familia kama mirathi.
Mbali na hilo, mjane huyo alisema siku zote alikuwa akimfahamu Katunzi kama ndugu katika Injili na si vinginevyo.
 Katika kuchimba zaidi, ilibainika kuwa hata uongozi wa Kanisa la EAGT ulimpa Katunzi sharti la kuachana na jambo hilo mara moja au kama angeendelea alipaswa kuacha vyeo na uumini wake wake katika kanisa hilo.
Ilisemekana pia kwamba, Katunzi aliahidi kutekeleza lakini mwishowe aliapa mbele ya familia hiyo kuwa angeendelea na kesi hiyo hadi kieleweke. 

KATUNZI ANASEMAJE?
Baada ya kulinyaka sakata zima, Risasi Jumamosi lilimbana Mchungaji Katunzi ambaye alijitetea kama ifuatavyo: 
“Wewe njoo uchukue ‘document’ uandike, nilishatangaza hadi kwenye magazeti, njoo uchukue sasa sitaki kuongelea suala hilo.” 

NINI HATIMA?
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni haikujulikana nini hatima ya suala hilo.

TUJIKUMBUSHE
Askofu Kulola alifariki dunia Agosti 29, 2013 katika Hospitali ya African Medical Investments (AMI) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na kuzikwa jijini mwanza.

Imeandaliwa na Chande Abdallah, Denis Mtima na Jerald Lucas wa Global Publishers

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huwa wachungaji wa kilokole ka majambazi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani we acha kutwa kuwafanya waumini wao Kama mandondocha yaani Mimi wananikera kweli ukikutana nao kujiona ndio watakatifu wengine wote wadhambi

      Delete
  2. Huyo mchungaji ni tapeli. Yeye c mke wa kulola wala mtoto wa kulola je mirathi inamuhusu vp. Huyo ni jambazi. Ameshazoea kula vya dhuruma kwa waumini wake hivyo haoni hatari kumzurumu marehemu kulola.

    ReplyDelete
  3. Kimsingi katunzi ni mojawapo wa wachungaji niliotokea kumwamini sana na kujua kuwa anachokifundisha ktk injili ndicho hicho anatenda lakini mbona tofauti ,sasa amerisishwa kivipi yeye ni nani ktk familia hii.

    ReplyDelete
  4. Mchungaji Mdhurumaji,usishangae Bado Watu Wanaendelea Kusali Nae,

    ReplyDelete
  5. Jamani mali si alipaswa aziache zishughulikie mambo ya kanisa!Hawa watu hatari sana wanawaibia watu kwa kuwaingiza kwenye imani.

    ReplyDelete
  6. naungana na 4:57 haya makanisa yanayojiita ya kiroho ni wezi watupu huyo mchungaji nae ni mwizi wamekwiba na moses familia inajua wizi huo na ma kataba yao ya kishetani? masikini wamekuwa miradi ya watu wasio na utu wala huruma mungu wanaomwabudu wao ni mungu gani hyo. yatisha kwelikweli mara wajiite wachungaji manabii. mmmmmmmmmmm

    ReplyDelete
  7. Mwenye akili ataelewa huo ulokole na unabii maana yake ni nini, mara upako sijui, wezi wakubwa hao hawana cha Mungu wala dini. Mali zote za Kulola ni sadaka, haya leo huyo Katunzi wanagombea na family ya Kulola, n mindi u hawa watu ndo hukaa madhahabuni kujinadi ni watu wa Mungu, walipita huku na kule tz kutangaza neno, leo hii mali yawaumbua, hv kuna mtu anaemjua Mungu haswa anaweza gombea sadaka? I hate walokole toka niwajue, wanajifanya wajuaji wa neno la Mungu bt ni wanafiki wakubwa. Nitabaki a dini yangu ya kuzaliwa Lutheran mpaka kufa.

    ReplyDelete
  8. Labda mchungaji alikuwa mke mdogo wa kulola sasa mama Elizabeth avumilie mke mwenzie awe mcmamiz wa mirathi tu ila mali zote warithi wawe watoto wa kulola,huwezi mtu na akili zako ulilie urithi ambao haukuhusu hawa wachungaji wengine vipi?na huyu mzee wa upako ameshampa Elizabeth hiyo rambirambi?ili tuendelee kumuheshimu atimize ahadi yake ampe mjane haki yake aliyoahidi.

    ReplyDelete
  9. Alipe wapi alitaka sifa mbele za watu sasa hivi waki mkumbusha alipe anajidai mbabe ndio hao hao matapeli kutwa kuwadanganya waumini wake

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad