MWANAMKE ALIYE PANGA NJAMA ZA KUMUUA MUMEWE ILI AFAIDI MALI ZAKE AENDELEA KUSOTA RUMANDE

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha jana imekataa ombi la hati ya dharura ya dhamana ya mke wa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, Janeth Jackson (32), anayedaiwa kupanga njama za kumuua mumewe wa ndoa.Janeth na mshitakiwa wa pili, Novatus Elias kupitia Wakili wao, Samsoni Rumende waliwasilisha hati hiyo katika Mahakama Kuu, kuomba dhamana baada ya mahakama ya wilaya ya Arusha iliyoko Sekei, kuwanyima dhamana.

Mahakama iliwanyima dhamana washitakiwa hao, kwa maelezo kuwa kufanya hivyo ni kuharibu kesi, kwani kuna watuhumiwa wengine hawajakamatwa.
Hata hivyo, Jaji Mary Moshi alikataa kumjumuisha mshitakiwa wa pili katika hati hiyo, kwa maelezo kuwa wakili hakumjumuisha katika hati.
‘’Katika hati ya dharura, naona jina la mshitakiwa wa kwanza tu ndiye anayeombewa dhamana, lakini jina la mshitakiwa wa pili, Elias, haliko hivyo siwezi kusikiliza kwa kuwa ni kinyume na utaratibu,’’ alisema Jaji Moshi.

Pamoja na hayo, Jaji Moshi alimnyima dhamana Janeth kwa maelezo kuwa Wakili Rumende amefanya makosa ya kisheria, kwani alipaswa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama ya wilaya wa kumnyima dhamana mteja wake.
Alisema kuomba hati ya dharura ya kuomba dhamana, sio utaratibu wa kisheria na kutokana na hali hiyo, alimtaka wakili huyo kwenda kujipanga upya .
Awali akizungumza mahakamani hapo, Rumende alimwomba Jaji Moshi kumpa dhamana mteja wake, kwani ana mtoto mchanga wa miezi mitano.
Rumende alidai kuwa dhamana ni haki ya msingi ya mteja wake na hawezi kuathiri mwenendo wa kesi na atatii masharti ya dhamana kwa jamii, inayomzunguka bila ya wasiwasi wowote.
Hoja hizo zilipingwa vikali na Wakili wa Serikali, Edana Kasala aliyedai kuwa utaratibu umekiukwa na pili mahakama ya wilaya iko sahihi kuwanyima dhamana washitakiwa hao.
Janeth ambaye ni mkazi wa Moshono, jijini Arusha pamoja na Novatus Elias, katika kesi hiyo katika mahakama ya wilaya, wanashitakiwa kwa kula njama ya kutaka kumwua Jackson Manjuru ambaye ni mume wa Janeth.
Washitakiwa wote wawili pia wanadaiwa kutenda kosa la kula njama na kutaka kumwua Desderi Sabas, anayeishi Bukoba mkoani Kagera, ambaye ni mtoto wa nje wa mume huyo.

Washitakiwa wote hawakutakiwa kujibu lolote mahakamani hapo, kwa sababu Mahakama hiyo kisheria haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HUYU MAMA AJATULIA, ALIMPA NAFASI SHETANI. MALI ZINATAFUTWA UHAI WA MTU HAUTAFUTWI, MIMI BINAFSI NAJUA MUME WANGU AKIFA ATAONDOKA NA KILA CHAKE NAMAANISHA MALI YAKE ITAKWISHA MAKE YEYE NDIYE ANAJUA ANAVYOSTLAGO. MIMI KAMA MKE NA MIE NATAFUTA KWA VILE TAYARI NAWEZA KUTAFUTA, KAMA UWEZI KUTAFUTA ATA UKIMUUA MALI ZITAKWISHA. MALI KITU GANI PASIPO BABA WATOTO WAKO! UMETUAIBISHA WANAWAKE. USHINDWE KWA JINA LA YESU

    ReplyDelete
  2. Huyu mama hafai bora afie magerezani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ole wako uoe huko alafu uwe mali lazima wakuue hao

      Delete
  3. Malaya ni Malaya tuu kumabake akafie jela skendolous bitch

    ReplyDelete
  4. ndo tatizo la kuchukua wanawake bar.

    ReplyDelete
  5. Ndio kawaida yao ukishazaa mtoto wa kiume na ukiwa na mali wanakuua ili wachukue mali wanafundishwa na mams zao huko hakunaga mke

    ReplyDelete
  6. Ao watakuwa wachaga ndo zao ukioa huko utakoma

    ReplyDelete
  7. Mnauhakika? Au mnaongea tu wadao ! Wanaume wa huku Arusha wakikuchoka ndo walivyo! Watakusingizia Umemtega BAba yake au ndugu yake ili mladi wakutoe kwake na usipate chochote, ujue hapo kapata mwingine nauyo mume kasimamia kesi kidete sababu ana pesa anaweza fanya lolote atakalo! Angetaka kumuua si angempa ata sumu kwenye msosi na nani angejua kama yy kaweka au kwenye kinywaji? Mchunguze sana huyo mama anataka kuzurumiwa asiambulie chochote kwenye mali na hivi mume wake anayo pesa atasota kwa Rushwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad