NISHA ASHINDWA KUKAA KIMYA KUHUSU SKENDO YA KUTOA MIMBA INAYOMKABILI

MTAYARISHAJI na mwigizaji wa Bongo Movie, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka akidai kuwa maendeleo yake katika filamu yamemtengenezea maadui.

Akizungumza na Mwanaspoti, Nisha alisema maadui hao wamefikia hatua ya kumzushia kuwa ametoa mimba au ‘ame-flush’ wakati anaumwa na kichwa.

Alisema amebaini kuwa ana maadui wengi ambao hawapendi kuona anavyoendelea na ndio maana wamekuwa wakimzushia maneno yanayomchafua katika jamii.
“Huku Bongo Movie hatari sana, hata ukiwa na rafiki yako kuwa makini naye kwani ipo siku atakuuza na kukupoteza, mimi sifuatilii mambo ya mtu mwingine zaidi ya biashara zangu na kazi yangu tu,’’ alisema.

“Bongo Movie kuna watu wanaotaka kila siku wajue Nisha kafanya nini ili wakuseme vibaya, kuwa na maendeleo ni kutengeneza maadui nahisi kuwa na maadui pembeni yangu,” aliongeza Nisha.
Nisha ambaye hivi karibuni alikuwa mgonjwa, alitoa kauli hiyo baada ya kuripotiwa maradhi yaliyokuwa yakimsibu chanzo chake ni mimba aliyoitoa.

Hata hivyo Nisha aliwashangaa waliomzushia hilo na kufafanua kuwa alikuwa anaumwa kichwa na kama ingekuwa ametoa mimba angekuwa anaumwa tumbo.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata akitoa tatizo nn. Atajijua mwenyewe na Muumba wake siku ya hukumu. Hatuna haja ya kumlazimisha aseme kweli...

    ReplyDelete
  2. Watu kazi umbea Tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad