PINDA KUITIA HASARA SERIKALI..ONA HIYO BARABARA

Sehemu ya Barabara ya Mlandizi- Chalinze, ikiwa imeharibika kutokana magari makubwa kuzidisha uzito na kusababisha uharibifu huo.Picha 
Dar es Salaam: Uamuzi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuruhusu malori makubwa ya mizigo yaendelee kuzidisha uzito wa mizigo, umetajwa kuwa ni hatari na utaisababishia Serikali hasara ya mamilioni ya fedha.

Hasara hiyo inatokana na uharibifu wa barabara za lami ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na malori yanayozidisha uzito wa mizigo kinyume cha sheria na kanuni namba 7 (3) ya Sheria ya Usalama Barabarani ya 2001.

Ujenzi wa barabara ni wa gharama kubwa na hata ukarabati wake umekuwa ukitengewa mabilioni ya fedha za walipakodi kutokana na uharibifu unaofanywa.

Mathalani katika bajeti yake ya 2013/14, Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, imetenga kiasi cha Sh314.535 bilioni kwa ajili ya mpango wa matengenezo ya barabara kuu na barabara za mikoa.

Kiasi hicho cha fedha ambacho ni zaidi ya robo ya bajeti nzima ya wizara hiyo kwa mwaka, kinatosheleza kujenga barabara mpya ya lami yenye urefu wa kilometa zipatazo 315, kwa makadirio ya kilometa moja kugharimu Sh1 bilioni. Katika mwaka huu wa fedha, bajeti nzima ya Wizara ya Ujenzi ni Sh1.226 trilioni.

Kauli ya Dk Magufuli

Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, aliwahi kunukuliwa akisema ataendelea kusimamia sheria ya barabara namba 30 ya mwaka 1973, hadi anaingia kaburini kwa kuhakikisha hakuna magari ambayo yanazidisha uzito na kuharibu barabara.

“Nchini Ujerumani, uzito wa magari yote ni tani 40, Uingereza tani 40, Ufaransa 40, Urusi 38 lakini Tanzania tani 56, wakati mwingine tunakamata hadi tani 96,” alisema Dk Magufuli.

Hata hivyo, ujasiri wa Dk Magufuli ulizimwa na amri ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliyetengua agizo la waziri huyo na kuamua kuruhusu magari yenye uzito uliopitiliza kuendelea kutumia barabara.

Wasemaji wa Serikali

Ofisa Habari wa Wizara ya Ujenzi, Martin Ntemo alisema suala hilo wameliachia Ofisi ya Waziri Mkuu. “Hilo suala liko Ofisi ya Waziri Mkuu, siwezi tena kulizungumzia,” alisema Ntemo kwa kifupi.

Hata hivyo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk Florence Turuka alisema siyo sahihi kusema kwamba Waziri Mkuu amevunja sheria kwani ilikuwa ni lazima serikali ichukue hatua jumuishi kwa kuwashirikisha wadau husika.
-Mwananchi
Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hii ndio tanzania bana ,akili zetu ni kama..........hatujielewi,sheria tuweke siye na kuzivunja tunazivunja siye,majanga,big up dr magufuli;wewe ulifaa uwe ulaya sio hapa ktk nchi ya kibabaishaji,well done dr,

    ReplyDelete
  2. Magufuli ukifanya hivyo kama ulaya uoni unawaumiza wafanya biashara wetu,kwann musiboreshe barabara tu.

    ReplyDelete
  3. wewe vipi?tutaboreshaje wakati kiwango chetu cha kubeba mzigo ktk barabara zetu ni tani40.hao wafanyabiashara wapunguze nmizigo yao.ili barabara zidumu.kanchi chenyewe kila kukicha shida.tuwe naakili sometime

    ReplyDelete
  4. Jamani bora hata umelizungumzia suala hli la barabara ya mlandz chalinze serikali naomba ichukue hatua za haraka kuepusha uharibifu wa barabara unaoendelea kutokea ambao pia umegeuka chanzo cha ajali nyingi hasa maeneo chalinze

    ReplyDelete
  5. Jamani bora hata umelizungumzia suala hli la barabara ya mlandz chalinze serikali naomba ichukue hatua za haraka kuepusha uharibifu wa barabara unaoendelea kutokea ambao pia umegeuka chanzo cha ajali nyingi hasa maeneo chalinze

    ReplyDelete
  6. Ndio maana akachaguliwa kuwa Waziri Mkuu! Angeweka mjuaji kama Dr. wasingewezana kwasababu angekuwa anaathiri miradi ya wenye Nchi Tanzania au Wanaoimiliki ! Lol!

    ReplyDelete
  7. Tukisema serikali hii ni yakishkaji mnachukia je tusemeje? Ona sasa je hii hasara pinda atalipa? Magufuri ndo jembe.

    ReplyDelete
  8. Sio kweli,hiyo barabara ni mbovu hata kabla ya Pinda hajaingilia kt suala la mizani!!!kwa nn paharibike eneo hilo tu kwani toka Chalinze hadi Moro hayo maroli yanaruka?

    ReplyDelete
  9. Waziri Mkuu mambo mengine yanahitaji ufumbuzi wa kitalamu sio kuridhisha kikundi kidogo cha watu ili wapate wanachotaka kwa maslahi yao huku unazidi kudhoofisha uchumi wa nchi na watu wake na hii inatokana na kumbana mwananchi kwa kodi zisizo na msingi ndio maana yanatokea haya serikali haikubali kumpunguzia kodi mwanachi inakubali kupata hasara ambazo zinaepukika nnchi hii ukiachia utajiri wake wa rasilimali pia mwananchi anailiipa serikali pesa nyingi kuliko yeye anacholipwa na serikali kodi zisizo za lazima zinaumiza wanachi na ndizo zinazoitafuna nchi.

    ReplyDelete
  10. 4 thc case all blaming iz belongs 2 prime minister 4 his bad statement also 2 the road contractorz cos why most of dat effects found at chalinze only? how about chalinze to iringa?
    chalinze tanga?
    and other main roads?
    there is no dat heavy lories?

    ReplyDelete
  11. Pinda ni mzigo.ila hata hivyo system yote ya uongozi Tanzania ni mzigo mzito.haiwezekani serikali inaendeshwa kifamilia familia kisa eti familia ya mkulu ina biashara katika secta fulani basi maamuzi ya kipuuzi ya kuvunja sheria kama haya ya Pinda yanafanyika

    ReplyDelete
  12. gari hazizidushi uzito .east africa yote inatumia uzito sawa .tatizo barabara hazijengwi kwa viwango .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad