MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishushia tuhuma nzito Baraza la Mawaziri, baada ya kudai baadhi ya mawaziri walioteuliwa hawana elimu ya kutosha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya. Alisema chama chake, kina wasiwasi na elimu ya Waziri Mkuya, kutokana na wasifu wake kutoonyesha vyuo alivyosoma wakati wa kupata shahada ya kwanza na ya pili katika masuala ya biashara.
Alisema katika tovuti ya Bunge, wasifu wa waziri huyo umeonyesha sehemu aliyosoma elimu ya sekondari na kuhitimu kidato cha sita.
Alisema katika tovuti hiyo, haionyeshi chuo alichosoma shahada ya kwanza ya biashara, ingawa inaonyesha masomo aliyochukua jambo ambalo linatia mashaka uhalali wake kuongoza wizara hiyo nyeti.
“Ukiingia kwenye tovuti ya Bunge, utaona wasifu wake kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita na shule alizosoma, lakini kuanzia elimu ya shahada imeonyesha masomo aliyochukua na kupata shahada ya kwanza ya biashara, haionyeshi vyuo, jambo ambalo linatia mashaka,” alisema Lipumba.
Alisema nafasi aliyopewa inahitaji kiongozi mwenye upeo wa hali ya juu, kuweza kupambanua mambo yanayohusu uchumi wa nchi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha za ndani na nje ya nchi.
“Napata wasiwasi kama Rais Jakaya Kikwete, aliangalia wasifu wa waziri wake kwa sababu asingeweza kumchagua kushika nafasi kubwa kama hii, wakati vyeti vyake vina mashaka,” aliongeza.
Alisema kitendo cha kumuweka mtu mwenye vyeti vya mashaka, kunaweza kusababisha nchi kuyumba kiuchumi, kuongezeka kwa deni la taifa, kwa sababu uamuzi wake unatokana na ufahamu wake.
Alisema kutokana na hali hiyo, uamuzi wa Serikali wa kuwaondoa mawaziri mizigo hautafanikiwa kwa sababu waziri huyo anaweza kuongeza mzigo mwingine kwa nchi.
“Mawaziri mizigo, wanaisababishia Serikali kuwa na viongozi mizigo, hivyo basi tunapaswa kuwa makini kwa kupinga kuongozwa na viongozi mizigo, kwa sababu wanaweza kutuletea matatizo,” alibainisha.
Akitolea mfano katika kipindi ambacho Waziri wa Fedha anapaswa kuwa makini na matumizi ya fedha za Serikali, ni pamoja na kuwepo kwa mchakato wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura, mchakato wa Bunge maalumu la Katiba, vitambulisho vya uraia na mambo mengine ambayo kwa kiasi kikubwa yanahitaji fedha.
Alisema kutokana na hali hiyo, waziri huyo anapaswa kusimamia matumizi ya fedha katika shughuli mbalimbali zikiwemo za halmashauri na safari za Rais, ambapo katika kipindi hiki cha robo mwaka, safari zake za nje zimemaliza bajeti yake ya mwaka mzima.
Alisema kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete alipaswa kumchagua mtu makini mwenye sifa stahiki kukalia nafasi hiyo, ili aweze kutimiza majukumu yake kwa kufuata taratibu za kisheria.
Alisema chama hicho hakina mashaka na uteuzi wake, lakini wana mashaka na chuo alichosoma na kupata shahada ya kwanza na ya pili.
WAZIRI AJIBU
Akizungumza na MTANZANIA Jumatatu kuhusu madai hayo, Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, kwani alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini Zanzibar.
Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza. Alisema mbali na masomo hayo, pia amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuhitimu mwaka 2009.
“Nimehitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland. “Kwa sasa nachukua Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar es Salaam,” alisema Mkuya.
Source: Mtanzania JUMATATU, JANUARI 27, 2014
Bora kasema Lipumba, ningesema mm wangesema Udini. Laiti vyeo vingegawiwa kwa uwezo na c kulenga balance ya udini na gender nchi isingekuwa hapa tulipo. Vyeo sio pilau ya msiba au harusi ampapo watu hugawiwa sawa sawa. Kusoma c lazima uelimike kwa ngazi ya uongozi, kiongozi ni extra unayopewa na Mungu au kufundishwa pia , sio kila mtu anaweza kuwa kiongozi wengine wanafaa kwa utendaji tu. Kwa tabia ya sasa kwamba vyeo vinazingatia udini, gender na ukanda au mikoa tutarajie mawaziri mizigo mpaka kufa. Hongera Lipumba, pengine wapo watu watakuelewa kwa jicho la tatu kauli yako.
ReplyDeleteacha majungu profesa, ulitaka uteuliwe wewe! mbona wapo wengi baadhi ya wabunge wanateuliwa kwa siasa siyo kisomo, nyerere alishasema bora ujue kusoma na kuandika. baadhi ya wabunge hawawezi kuongea kiingereza japokuwa wanaonesha vyeti vya digrii, nashangaa! KARABAGAO
ReplyDeleteWe acha upumbavu kwani kingereza umeona ndo elimu kuna Maprofesa kibao duniani hawajui kingereza Na ukienda nchi kubwa za ulaya German,Italy,France,China kuna wasomi wakubwa hawajui kingereza,Halafu unasema Nyerere alisema bora ujue kusoma na kuandika kwa hiyo kwa akili yako una maanisha mtu anaweza kuwa waziri Kama anajua kusoma Na kuandika ukiachana Na mambo mengine,basi ikibidi hivyo hata mtu wa darasa la kwanza anaweza kuwa waziri ilimradi ajue kusoma Na kuandika..Ama kweli kuna mijitu mijinga kwelikweli duniani...
DeleteNyerere alikuwa Mungu kiasi kwamba alikuwa hakosei?Kuwa waziri unatakiwa uwe na upeo mkubwa sana wa kupanga, kutenda na kuongoza
DeleteHongo ya ngono, kapewa cheo hana elim
ReplyDeleteProf yuko sahihi maana sheria inasema waziri lazima awe na shahada ya kwanza na kuendelea
ReplyDeleteLipumba hongera kumuweka sawa huyo brother,avunje tena baraza kabla nchi haja iyuza
ReplyDeleteHamna kitu kibaya kama wivu
ReplyDeleteMarehemu Sheikh Zaid Al Nahyani- Rais wa UAE hakusoma hata darasa la tano lakini Nchi yake ipo Juu ki Uchumi, hapa kwetu hata uwaweke Ma PHD efu katika wizara moja basi Ndio wezi utazidi... tumeona Maprofesa kibao katika wizara nyeti mbona hatukuona Matunda yao! wacheni Ubishoo - kwakuwa Mzanzibari ndio Mnaanza chuki sasa hao maprofesa wenu wametuletea matunda gani!! labda Uproofesa wa Kuiba kwa Style yake Bila kuhukumiwa na Huku Watanzania wakiwapigia makofi.
ReplyDeleteUsifikiri kuwa UAE imeendelea kwa sbb ya Sheikh Zaid, kuna vichwa vilikuwa chini yake vilivyotanguliza maslahi ya nchi na wala si binafsi.tanzania tuna resource nyingi lakin tutaendelea kuwa maskini kwa sbb ya tamaa za watu wachache
Deletehttp://tasktojob.com/index.php?task=109658
ReplyDeleteDiploma mara mbili
ReplyDeleteKisha akasoma Masters!! Duh kaazi kwelikweli! Kumbe diploma zikiwa mbili zageuka degree!! Tz bila ujinga haiwezekani!!!!
Jamani huyu waziri kimeo bila shaka kabisa.
ReplyDeleteTuache masihala!
ReplyDeleteKuna wizara nyngne znahtaj viongoz walio watendaj na wenye elimu.huyu kaonesha elm yke yakuunga
dploma + diploma = degree
kaz kweli kweli
huyo mwanamke hawezi kuongoza hiyo wizara tuache masihala. tutakoma miaka miwili hii. yaani mzigo mwingine umeongezwa serikalini. waziri kimeo na uchumi utakua kimeo. wapo watu wengi wana uwezo lakini nashangaa watu wanateuliwa kiuswahiba badala ya uwezo. nchi hii kwishnet!
ReplyDeleteNamshauri Raisi afikirie tena kuhusu hiyo wizara hongera lipumba kwa kutufumbua akili
ReplyDeleteTusipoteze nguvu kujadili vitu ambavyo tunajua kwa hakika hakuna kitakacho badilishwa.Mulugo alivumiliwa kipindi chote,si bora hatahuyu mwenye elimu iliyopitia SPEED BUMPS.Katiba mpya ndio jawabu..
ReplyDeleteMnataka awekwe msomi hela za kampeni mtatoa nyie.Hawa wasomi wataanza ku-question mambo mengi..miaka 9 iliyopita ka account ka EPA kalisaidia....
ReplyDeleteNyie watu wawili hapo,juu mmenifurahisha sana nawapa big up
ReplyDelete