Web

RAIS KIKWETE ATANGAZA KUWA KESHO JUMATATU NI SIKU YA MAPUMZIKO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.


Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.


Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.


Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.


Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Waafrika hawajui kutawala mwafrika ujuzi wake ni mambo 3 la 1 umalaya la 2 ujambazi la 3 ulevi hayo ndio mambo na ujuzi aliyonayo muafrika lau kama ingekuwa zanzibar mpaka sasa yatawaliwa na sultan ingekuwa imepiga hatuwa sana afadhali udhalimu wa sultan kuliko udhalimu wa mwafrika!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaan kweli kabisa...Umesahau jambo moja...kuwaozesha mabint zao wakiwa wadogo wapate pesa...Mie nataman tz tungeendelea kutawaliwa nadhan tungekuwa kama s.africa sasa...

      Delete
    2. Wadau naona mnachemka,,,Bora tuwe masikini kuliko kuwa majajiri watumwa.
      Hata huko South,majumba na barabara nzuri zinawasaidia nini wazalendo???
      Si bora sisi mara mia,Tuko huru na tuna amani.

      Delete
  2. Bora kuwa masikini huru kuliko kuwa tajiri mtumwa,,,hayo mabarabara ya south yanawasaidia nini wazalendo????Si bara sisi Bongo twajilia ugali maharage twalala,hakuna kuamshwa

    ReplyDelete
  3. Ametumia akili nyingi jk

    ReplyDelete
  4. Tena akili ya kuzaliwa

    ReplyDelete
  5. Si kwamba wafrica hawajui kuwatawala wafrica, mwafrica ni nani? si sisi wenyewe ndio wafrica. Ni kwamba wafrica tumeshindwa kujitawala na kujiongoza wenyewe kwa wenyewe,

    ReplyDelete
  6. South Africa sio kwamba ilikuwa bado inatawaliwa la hasha, south africa ilisha pata uhuru wake miaka mingi tena kabla sisi hapa watanganyika au wabongo, Sema ilikuwa inaongozwa na makaburu from Netherland kabila, na utawala wa uongozi ulikuwa ni wa kibaguzi, kubagua mwafica, katika nyanja zote, na ilikuwa ni koloni la mwingireza kama sisi, ila ilishapata uhuru muda. utawala wa mwingireza ulisha kwisha, madaraka yakashikiliwa na wazungu jamii hiyo ya kutoka Netherland kabila, na ikambagua mtu mweusi mwafrica,

    ReplyDelete
  7. Mheshimiwa hapo sawa!.

    ReplyDelete
  8. kuna watu hawajitambui wanasema tu mambo yasiokua na msingi tuseme hao wazee wetu walojikomboa walikuwa hawataki raha na kama kulikuwa na raha kwanini wajikomboe wacheni ujinga watu wamepoteza maisha yao kwa kulilia umtu na kuondoa ubaguzi kwao wao na vizazi vyao.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad