Web

SHILOLE AWACHANA MASTAA WABEBA UNGA

Stori: Shani Ramadhani
STAA wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amewachana wasanii wanaojihusisha na madawa ya kulevya kuwa ni wavivu.

Akizungumza na paparazi wetu pasipo kuwataja majina, Shilole alisema wasanii wengi ni wavivu na kinachowaponza zaidi ni tamaa za kuwa na maisha mazuri, wanafikiri mafanikio yanakuja kirahisi pasipo kuhangaika.

“Wanafikiri mafanikio yanakuja kirahisi bila kujishughulisha, ninawashangaa sana kwani wanajishushia hadhi zao kwa tamaa ya kutaka kuwa na maisha mazuri bila kufanya kazi, badilikeni,” alisema Shilole.
By Global Publishers

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Naye abadilike...avae nguo za staha. Ni mdada mzur...ila mavaz siyakubali kabisa.

    ReplyDelete
  2. dada Shilole badilika jamani kuweka maumbile yako wazi unamkosea Mungu aisee!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad