SITTA"UWOGA NI ADUI MBAYA SANA WA MAENDELEO NA HAKI"

Waziri wa tanzania Samwel Sitta amewasihi vijana kutokuwa waoga, kwani "UWOGA NI ADUI MBAYA SANA WA MAENDELEO NA HAKI" hivyo kila mwananchi ana haki ya kufurahia rasilimali za nchi, ambazo kuna baadhi ya viongozi wanataka kuhodhi madaraka kwa namna yeyote ili waendelee kuchumia matumbo yao. 

Akamalizia kwa kusema, yuko tayari "KUBEBA TOCHI ALIYOIACHA MWALIMU NYERERE". Vijana walilipuka kwa shwange na makelele, kongamano hilo alikuwepo waziri mwingine wa tanzania Dr Harrison Mwakyembe na viongozi wengine waandamizi wa serikali na viongozi wa dini pia.

Haya banah, tutashuhudia mengi sana mwaka huu 2014, hoja hii ya Sitta inafanana na ile ya Kamanda makini Lema "HAKUNA DHAMBI MBAYA NA KUBWA DUNIANI KAMA WOGA".

Yangu macho tu

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. "NIKO TAYARI KUBEBA TOCHI ALIYOIACHA MWALIMU NYERERE" Je tuchukulie km mweshimiwa ndio katangaza kampeni?au...

    ReplyDelete
  2. Katangaza kiana!

    ReplyDelete
  3. Ndio maana yake, prezdaa material ni hawa tu, lowasa, sitta, magufuli na mwakyembe, ila najua magamba watachagua membe brazameni kama kawaida, hawapendi mtu anayesema NO and he mean it!

    ReplyDelete
  4. Kutokana na makundi aliojitokeza ndani ya chama hiki na kutokuwa na a distict figurehead mwenye guts za kukemea km alivyokuwa Mwalimu na predict a big fracture ndani ccm right before election na if not checked will lead to a demise of it.

    ReplyDelete
  5. Namshuru waziri,pia naomba ashughulikie swala la uhamiaji haramu,kwa kushirikia na waziri wa mambo ya ndani,kwa kuwa wahamiaji haramu wanaishi karibu na mbuga sikuzote,hawaishi tena mjini,serikali iwe makini sana,kwa kuwa taarifa km hizi tunazipata nje ya mipaka yetu,nashukuru pia kwa swals la visa la tourism in east africa,Tanzania ni lazima tuwe na maamuzi yetu kwa faida ya Watanzania tuwe makini sana kwa swala la wahamiaji haramu ,tunaharibiwa sifa yetu katika dunia,ns muundo wa jeshi ls polisi,uongezewe taalums,kiwepo kikosi maalum cha kupambana na majambazi na usalama wa raia kinacho jitegemea na mawasiliano yao,,hata km ni kuchangia tupo tayari,nchi haieleweki watu kuteka magari,au kuiba kwenye mabenki.

    ReplyDelete
  6. "UJEMBE" nasi vjana hatuna nidhamu ya woga 'kuku ni kuku jogoo jina 2'.

    ReplyDelete
  7. Kumbe 6 ni nouma eti....!?

    ReplyDelete
  8. Yetu ni macho na maskio...2015 hiyooo mbio ndo hizooo...:

    ReplyDelete
  9. Natamani Januari Makamba baadae aje kuwa Raisi kwa miaka ya baadae sababu jamaa kichwa sana Na ana elimu ya kutosha kiasi kwamba ukifuatilia mijadala yake anayoifanya Na wanafunzi wa chuo utagundua kuwa jamaa ni noma..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad