LICHA ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuweka zuio la muda kwa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujadili uanachama wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mjumbe wa CC, Tundu Lissu amedhihirisha wazi kuwa chama kimemvua Zitto uanachama.
Lissu ambaye pia ni Wakili wa Chadema katika shauri hilo la zuio, jana katika mkutano na waandishi wa habari na viongozi wa Chadema kuhusu tamko la hatua iliyochukuliwa dhidi ya wanachama watatu waliovuliwa nyadhifa zao akiwemo Zitto, bila kujali zuio alikiri mbele ya waandishi hao kuwa Zitto ataendelea kuwa Mbunge na mwanachama kwasababu ya Mahakama na si matakwa ya chama hicho.
“Ni wazi kuwa harakati zao hasa Zitto za kukichafua chama hazikuanza leo, ni njama zilizoanza muda mrefu sana, hao ni wahusika wa uhaini na usaliti kwa chama na kwa hakika Zitto ataendelea kuwa Mbunge na mwanachama kwa sababu ya Mahakama tu na si kwa matakwa ya Chadema,” alisema Lissu jana katika mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya Chadema, jijini Dar es Salaam.
Kwa kauli hiyo ya Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), ni wazi pamoja na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kueleza waandishi juzi kuwa CC haikujadili uanachama wa Zitto, kutokana na zuio la Mahakama Kuu, uanachama na uongozi wa Zitto ulijadiliwa hadi kumpa kibali Lissu kutoa kauli hiyo, inayodhihirisha uanachama wa Zitto kwa sasa unashikiliwa na Mahakama tu na Chadema ilishafanya uamuzi.
Kabla ya kauli ya Lissu, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa aliwaeleza waandishi wa habari katika mkutano huo kuwa CC haikujadili wala kuamua kuhusu uanachama wa Zitto kutokana na amri ya Mahakama na kwamba mara baada ya uamuzi wa Mahakama, hatua hiyo itafuata na uamuzi utakaofikiwa kutokana na maazimio ya Kamati Kuu, utatolewa kwa wanachama na wananchi kwa ujumla.
Mbali na Zitto, wengine ambao ni watuhumiwa waliofukuzwa uanachama na CC katika tamko la awali la chama, lililotolewa jana katika mkutano huo na Dk Slaa ni aliyekuwa Mjumbe wa CC, Dk Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Mtu annayekuchukia ni mbaya kuliko muuaji kama alikua na shida wewe lissu na uongozi mlikua mmekufa kipindi hicho ss mmefufuka? mtu mzima kama wewe hufai kuwa muongo mtu kama hammtaki mwambieni tu sio kutoa sababu za kipuuzi
ReplyDeleteHongela LISU! Toeni hiyotata inayochafua chama, zzk hatufai kwani kunawa2 wamepoteza maisha halafu yy anajiuguza wehu! Manayakenini?
ReplyDeleteBora ang'oke tu....hatumtak.....!
ReplyDeleteWw anonymous 10:29 nafikir akili yako imeoza,walikwambia hawamwitaji?haya mambo ya siasa km hatuyajui tujikalie kimya!hauwezi ukawa mchafu kwenye matendo yako hlf ucwe accounted for,im sure chadema wameona ambayo mm na wengine hatujayaona,besides hayo ni ya kwao,ww lia na serikali yako sikivu, tangu umeanza kulipa kodi,imekuwa ikielekezwa wapi palipo na mabadiliko ya kimaendeleo?
ReplyDeleteAende 2, hatumtaki, wa2 2nasota kwa ajil ya ulafi wa wachache! NGOMA IKIVUMA SANA MWSH HUPASUKA.
ReplyDeleteZitto pambaf!...hamia ccm, chadema kina wenyewe, watu makini siyo usaliti wako wa kitoto!
ReplyDeleteNyie woootee unaotetea chadema ndio waleee msioenda shulee,huyo tundu lisu ana nini hasa anachokijua kuhusu chadema? Bali na yeye anapelekwa pelekwa tuu hata kazi yake haijuiii kutwa kujipendejezaa ili asifukuzwe kazii!!! Mnashabikia vitu tuu msivyo vijuaa undani wakee, mhhh..rudini shuleee ili mjue haki zenu ktk chama,..zito ni msomi aliyebobea na anawapeleka kisomi akiwa ni mtoto mdogo lakini kawazidi upeoo..Mburulaaz nyiee msiejua muendakoo shut up!!!!
ReplyDeleteUsaliti wa zito uko wapii!!?pumbav weweeeee mbowe ndo msaliti namba 1 aliyepewa milioni 100 na mzee mkono ili afungue gazeti...mbona hamsemi hayooo,,,bac kwa taarifa yako hatoki chadema na akitoka utaona nn kitatokea mmezoea kuonea watu sasa mmepata kiboko yenuuu., shughuli ndo kwanza inaaanzaaa subirini muone movie yenyewee mtajutaaa!!!!!!tumejipangaaa kulikoo tunataka mjue nn maana ya siasa..
ReplyDelete