Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam imechukua hatua ya kushangaza ya kujitoa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Zanzibar katika dakika za mwisho.
Uongozi wa Yanga ulichukua hatua hiyo siku moja kabla ya mashindano hayo yanayoshirikisha timu 12 kutoka Kenya, Uganda na wenyeji Tanzania kuanza.
Kwa kweli hatua hii ilikuwa ya ghafla mno na tunaamini imewakwaza na kuwapa mtihani mkubwa waandaaji wa mashindano hayo.
Itiliwe maanani kwamba mashindano hayo ya mwaka huu ni makubwa zaidi na yamepewa uzito mkubwa kwa vile yanafanyika wakati Zanzibar inasherehekea miaka 50 ya Mapinduzi. Kitendo cha Yanga kujiondoa kwenye mashindano hayo tena dakika za mwiso kimeshangaza hasa kwa kuzingatia uhusiano wa klabu ya Yanga na Mapinduzi ya Zanzibar.
Historia inaonyesha kuwa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume aliwahi kutumia fedha za wananchi wa Zanzibar katika kusaidia kujenga makao makuu ya klabu ya Yanga yaliyopo Jangwani, Dar es Salaam.
Sasa inashangaza kwa uongozi wa Yanga kusahau historia hiyo na kujitoa katika mashindano yanayotukuza Mapinduzi hayo ya mwaka 1964.
Ukiacha suala hilo la kihistoria, mashindano hayo ya Zanzibar yalikuwa muhimu mno kwa Yanga katika maandalizi yake ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo wanashiriki mwaka huu.
Yanga ingeshiriki mashindano hayo timu yake ingepata nafasi ya kujua upungufu na udhaifu wake kwani katika hatua za awali ingepambana na Azam ya Dar es Salaam na Tusker ya Kenya ambazo ni timu kubwa na ngumu.
Kuondoa benchi la ufundi na kuitumia kama ndiyo sababu ya kujitoa kwenye mashindano hayo hakutoshi kwani klabu kadhaa zimekuwa zikifukuza makocha lakini zinaendelea na mechi zinazowakabili.
Kama uongozi wa Yanga ungekuwa umejipanga vizuri ungekuwa tayari na kocha mpya ambaye angeitumia michuano ya Kombe la Mapinduzi kuona na kufahamu aina ya wachezaji alionao. Yanga ni lazima ijifahamu kuwa ni klabu kubwa na yenye mashabiki wengi nchini kwa hiyo inatakiwa kutafakari kwa makini kabla ya kuchukua uamuzi wowote ule.
Ni dhahiri kwamba kujitoa kwa Yanga kwenye mashindano hayo kutawaathiri sana waandaaji hasa kwenye mapato kwani mechi za Yanga zilitarajiwa kuwavutia mashabiki wengi.
Lakini, kama Yanga ingejitoa mapema katika mashindano hayo na kuukataa mwaliko wa kushiriki kungewapa nafasi waandaaji kualika timu kubwa kwenye mashindano hayo na ambayo ingepata nafasi ya kujiandaa kabla ya kwenda kwenye mashindano.
Inajipanga kwanza
ReplyDeleteWOGA UMEWAZIDI,
Deleteau milango ilifungwa mambo
ya Issa Makongolo HAKUNA?
hayo ndo matatizo ya club zetu za tazania hawakubali walikotoka ndiomana timu zetu tunategemea wachezaji wageni kwa matatizo hy hayo hatusani vyakwetu tuache ujinga hata club za ulaya haziwasahau mashujaa wao ndio njia ya mafanikio club zetu zinapoteza kumbukumbu ndio maana soca letu zero
ReplyDeleteUsichanganye mambo
DeleteTabia ya kuogopaogopa anayo yanga tu,
Simba si mchezo haogopi
timu yoyote kama alivyo
MNYAMA tishio MSITUNI
sauti tu unajikojolea
yanga eti walijua watakutana na SIMBA.
Wewe si mwanamichezo
DeleteTunachoongelea ni yanga,
Wala si timu taifa.
Timu binafsi inauwezo wa kuchukua mchezaji yoyote duniani, iwe yanga,simba, azam,
ashanti n.k
Na wachezaji wetu wazawa wana
Uwezo wa kucheza matifa mengine.
cyo lazima Yanga ishiriki mashindano yote, kwani timu nyingine hazitaki kushiriki, walichofanya ni sahihi kuwapatia fursa na wengine washirika, kama Ashanti vile.
ReplyDeleteWewe mwoga wa kufungwa
Deleteau katika wale waliozimia
kipigo cha goli 3?
Yanga,Simba kazi yao ni kucheza mpira football
M'mekimbiaa M'meogopaaaa
na jana tumewapa milioni kumi, ambazo ni nyingi kuliko thamani ya kombe lenyewe, sasa huo siyo uungwana?
ReplyDeleteYanga
ReplyDeleteImekimbia kipigo
Bado wanawaza kipigo cha goli 3ile ni bonanza tu jamani
Nasikia tetesi mnawashawishi waliowafunga siku ile muwachukue! Mnatafuta goli 7 mtazipata lini mvunje record? MNATIA AIBU KUTOSHIRIKI
KOMBE LA MAPINDUZI kumbe si wazalendo!