Mara yule babu akamuuliza mwanae, “ nini hicho kinapiga kelele mwanangu?”
Mtoto akajibu, “ Ni jogoo anawika huyo baba!!”
Mzee akatulia kama dakika kisha akauliza tena baada ya jogoo yule kuwika tena, “ Nini hicho kinapiga kelele mwanangu?”
Mtoto akajibu tena, “ Ni jogoo anawika huyo baba mbona husikii!!”
Wakaendela kuongea kwa dakika chache na kisha babu akauliza tena, “ ni nini hicho kilichokuwa kina piga kelele mwanangu?”
Kwa hasira mtoto akajibu, “ baba mbona unakuwa mgumu kuelewa ni jogoo huyo alikuwa anawika,sasa hujaelewa nini hapo baba????”
Mzee yule akauliza tena baada ya daikia moja, “mwanangu ni kelele za nini zilezilizosikika?”
Safari hii yule mtoto uvumilivu ulimshinda na kujibu kwa kelele na hasira, “ baba sipendi maswali yako ya kijinga, kwani hujui huyo ni jogooo, Au unataka tutafutane ubaya mida hii?????”
Taratibu babu yule alinyanyuka na kwenda ndani na kurudi akiwa kashika kitabu chake kidogo cha kumbukumbu alicho kiandika mika 42 iliyopita na kumpa mwanaye ambaye sasa ana miaka 45 ili akisome.
Mtotoyule aliumia sana baada ya kusoma maneno yaliyoandikwa miaka 42 iliyopita na baba yake wakati huo mtotohuyu alikuwa na miaka 3.Mtoto yule aliskia sauti ya jogoo aliwika na akamuuliza baba yake ile ni sauti ya nini…
Baba yake aliandika katika kumbukumbu zake , “Leo nina furaha sana kwani mwanangu kasikia sauti ya jogoo akiwika na kaniuliza mara 23 kuwa sauti ileni ya nini na wala sijachoka kumjibu na nikamkumbatia na kumwambia kila muda aniulize swali lolote nami nitamjibu kwani yeye ni furaha yangu”
Mtoto aliulizwa mara 4 tuu na baba yake lakini akaona ni kero na wakati baba aliulizwa mara 23 na bado akafurahi na kuona kapata bahati ya kuulizwa swali na mwanae.
Je ni wangapi leo ambao yunaona kero kupokea simu za wazazi wetu au hata kero kuwa nao karibu na hata kuwapa nafasi wao watuulize au kufurahi nasi hata mara moja tu????
Tunahitaji kubadili mienendo yetu na kuwafurahia wazazi wetu na kuona tuna bahati kuwa nao.Fikiri ni wangapi tunakosa bahati ya kuwa na wazazi wote wawili?
Kwanini Umpeleke Baba/mama/babu/bibi yako katika kituo cha kulelea wazeee? Je wewe ulivyokuwa mtoto hujiwezi wangekupeleka kituo cha kulea watoto ungejisikiaje sasa?
imenikuna cn hy na pia imenifundisha naomba mungu anipe moyo wa uvumilivu niwalee wazazi wangu km walivyo nilea
ReplyDeleteEwe mola nipe umri na uwezo niweze kuwaangalia na kuwasaidia wazazi wangu hadi mwisho naomba uniepushie roho mbaya na ya uchovu juu yao,kwani kama wao wangechoka leo hii nisingekuwepo,Ameen.
ReplyDeleteIna maana huo upuuzi wa kuwapeleka wazee kwenye vituo upo hapa kwetu? sidhani kama huo upuuzi umeshafika hapa kwetu na ninatamani hata usikubaliwe ,yaani mtu una watoto wako wangali hai na wana uwezo halafu unampeleka mzazi wako kwenye kituo cha kulea wazee hapana kabisa kwa hili tulikatae ndugu zangu.Ahmed, Gairo
ReplyDeleteEe Mungu tusaidie sisi kizazi cha sasa,maana tumekuwa wabinafsi na wenye kujipenda wenyewe kuliko wazazi wetu!
ReplyDeleteKwa kweli nimepata fundisho
ReplyDeleteWe Ahmed, Gairo hujui kama hivyo vituo cha kulelea wazee kimojawapo kipo Morogoro ulipo wewe, au wewe uko Gairo ya wapi?
ReplyDeleteNina muomba mwenyenzi Mungu, aniepushe na roho kama iyo. Anisaidie ili niwe mukarimu kwa mama yangu alie hai kwa sasa. Umenifunza sana.
ReplyDeletehiyo ni picha ya Mashaka, yule mtanzania anayeishi Marekani alikuja kutoa misaada huko Bagamoyo
ReplyDeleteacha ufala we mbisi ulitaka picha ya tukio halisi??....
ReplyDeletepia hakuna aliyesema picha inauhusiano na stori
kma vp kapige na mzazi wako utuletee!!
Mdau wa 9:28 AM nafahamu kama kuna hivi vituo hapa kwetu, lakini vituo vya kwetu viliweka mahususi kwa wazee wasio na uwezo na si kama kwa wenzetu wa ulaya hata ndugu au watoto wako wakiwa na uwezo wanakupeleka tu yaani qualification ya kwenda huko ni uzee na sio kingine lakini hapa kwetu ili upelekwe kule mara nyingi ni kwa wale wasio na ndugu au wasio na uwezo kabisa, mimi nilikuwa nina maanisha kwa wale watoto wenye uwezo wa kifedha kama wale wa ulaya halafu wanawapeleka wazazi wao kwenye hivyo vituo na sio hawa wa hapa kwetu ambao wazee wenyewe hawana uwezo na wamechoka na pia watoto wao au ndugu kwa lolote.Ahmed ,Gairo
ReplyDeleteMwenyezi mungu naomba unipe maisha marefu niwalehe wazazi wangu, maana roho inaniuma sna navyoona wazazi wakiwazika watoto wao baada ya watoto kuwazika wazazi wao. Ameni.
ReplyDelete