WASTARA AWAPASUKIA WAANDISHI WA HABARI , NA HICHI NDICHO ALICHOKISEMA

Muigizaji wa kike wa filamu za kiswahili, Wastara Juma amesema tangu mme wake Juma Kilowoko aka Sajuki afariki anakutana na changamoto nyingi kwenye mazingira yaliyomzunguka kwa sasa.


Akizungumza na tovuti ya Times FM 100.5, Wastara amesema tangu Sajuki afariki kumekuwa na taarifa zisizo za kweli zinazodai kwamba amepata mume.

“Nina changamoto nyingi sana,unajua siku zote kama mtu ukitaka kuheshimiwa basi heshima ndio msingi wa maisha,lakini tangu mume wangu afariki (Sajuki)kumekuwa na maneno mengi sana kwenye magazeti,mara nimeolewa sijui nimevishwa pete na ukija kuangalia mtu aliyeandikia hiyo habari unamjua na ukimpigia simu anaanza kukukwepa. Kama habari za kuolewa siwezi kwanza kutangaza, naomba waandishi waandike habari za uhakika ili ujumbe ufike mzuri kwa wananchi wanaotutazama sisi Wasanii.” Amesema Wastara.

Katika hatua nyingine Wastara amesema mwaka huu amejipanga vizuri katika kutoa filamu zake mpya sinazotarajia kutoka hivi karibuni.

“Mwaka jana mwishoni nilijikita sana kwenye kuandaa filamu mpya za kwangu na nyingine nimeshiriki kwa hiyo mashabiki wakae tayari.”
CREDIT : TIMES FM WEBSITE

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. http://internetduty.com/user/dashboard.php

    ReplyDelete
  2. Unaboa sn stara hv uwezi kuishi km mm mjane? Kila kukicha unatoa habari zako kwenye mablog itakusaidia nn zaidi ya kujichoresha? Ooh nataka mume Tajiri mara ooh nataka prado. Jamani tumekuchoka dear mlillie mola shida zako sio binadamu. Mwislamu gani ww? Lea mwanao swali blog hazina maana ni haram

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nadhani umemtafsiri vibaya, hapo inaonekana ameweka wazi kuwa waandishi wanajitungia habari na kuandika. So, amejaribu kuweka sawa kuhusu habari zinazotoka kwa kutungwa sidhani kama ni vibaya na ukizingatia wamegundua kuwa anauza habari siku hizi daah!! Mi mwenyewe nilishashuhudia habari imetoka kwenye gazeti inamuhusu mtu na muhusika mwenyewe hajui imetokea wapi, kujaibu kuwafuatilia wanamwambia wampe hela atulie ni upuuzi tu!!

      Delete
    2. Yaan alichokiongea hujamulewa watu wengine sujui mnafikiria na matako!

      Delete
  3. jamani mdaunakuunga mkono manahuyudada kilaleo anamsema mmewake kwann unakuawakuwekakila kituwazi?manahata hayamagazeti yanaandikwa kutokana namwonekano wamtu mwenyewe sasa yy sjuindoanataka sifakuitwa mjane! kituambacho nikibaya sana kwamwanamke aliemkubwa hlonijalibu lawote achakujtangaza sirizako nizakonamungu wakomala natakakuolewa namilionea nispate shida einamana ww hukuaunaridhika nasajuki?ulpata wpinguvu zakusema nenokamahilo? jiheshimu mimihatakama nikiwamsanii szanikama nitakuawakuandkwa kilasku kwenye magazeti nimwonekano wamtu ukijilahisi lazima mwandishi aandikeapendavyo mwonekano wako ubadilike mama .....neno lamwnyzimngu linasema ssnibarua ambayoimeandikwa watuwatuonapo mwonkano tu mtuajifunze toka kwako nass nitaa matendoyako nitaakwawatu sasa unapoangaza ujinga mtu hatojifnza kitu kwako zaidi yakukutangazatu badrika mama badotunakupenda ssmashabiki zako.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kiswahili chako kibovu, au unaandika ukiwa unakunya?

      Delete
  4. Ana victim mentality .Ana penda kuwa victim na hiyo ni dalili ya mtu manipulative

    ReplyDelete
  5. lakini wastara kwanii usiolewe tena?

    ReplyDelete
  6. MALAYA HUYO ANAJIUZA TU KWNY VYOMBO VYA HBR.

    ReplyDelete
  7. Unakosea kumwita mwezako malaya soma kwanza vizuri malalamiko yk hapo juu pili! Hii tabia ya waandishi kuzusha habari wanao sn ukifanya uchunguzi sn unakuta hata mhusika hajui kinachoendelea

    ReplyDelete
  8. Anonymous 4:20 AM una kigugumizi mpaka kwenye mwandiko??!!duh!hii kali.......

    ReplyDelete
  9. No, huyu dada kazidi kulialia kwenye mitandao, hata kanusha yake haina nguvu, km anamfahamu anae mzushia si achukue hatua.kiulize, kuna wasanii wangapi ambao privatelife zao hatuzisikii kwenye mitandao?hii ni hulka ya mtu.anachotakiwa kufanya niku keep her private life private.

    ReplyDelete
  10. Shut up Wastara unapenda media mno kutwa unatoa habati zako mwenyewe kaa lea mtoto kwani lazima kama amaarufu umesha basi khaah watu wamekuchoka sanaaaaaa

    ReplyDelete
  11. Keep it up grl dnt give up....i knw u cn do it n dnt mind what people r sayin abt u. Keep urself on truck

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad