YAFAHAMU MATATIZO YA KUPIGA PICHA ZA UTAMU UKIWA NA MPENZI WAKO FARAGHA

Baada ya kusoma na kuangalia baadhi ya blogs zinazoonesha udhalilishaji wa Dada zetu Hapa Tanzania, nikaona bora na mimi nitoe somo kidogo, 

Somo langu si kubwa sana lakini ni la Muhimu sana kwa wasichana wanao jiheshimu na kutaka kulitunza Hekalu takatifu, (mwili ulio umbwa na kubarikiwa na Mungu mwenyewe.
Chumbani ni sehemu ya Siri, ambayo inamfanya mtu ajitawale na kufanya matendo ambayo hayawezi kufanywa  mbele ya hadhara, ikiwemo na kuvua nguo, kujaribisha nguo, kulala ukiwa mtupu kwa kujiamini, na kufanya lolote ambalo mbele za watu utaona Aibu.

Lakini sasa nimeona mambo ya chumbani yanafanyika hadharani kwa kutupa picha za video na mnato kwenye mitandao sijajua kwa maana gani ila mambo hayo yanawaweka watu Fulani Fulani kwenye utata sana hasa Dada zetu.
Picha za utupu.

Mimi naamini kuwa Picha hizi hupigwa kwa usiri mkubwa lakini utunzaji wake si wa Siri tena. Laptops na simu zetu za mikononi, ndio zinazo waumbua wengi sana, hasa zinapo haribika, na kuhitaji kupeleka kwa mtaalamu atengeneze.

Kuna Msichana mmoja alijikuta anatembeza penzi lake kwa wanaume karibu sita, baadaye akagundua kuwa anajidhalilisha na mwisho kupatwa na ugonjwa wa zinaa, ambao kwa sasa amepona lakini hiyo life experience imemfanya asiwe na furaha ya maisha kwa sasa.

Sababu kubwa alipiga picha wakiwa watupu na mpenzi wake, na mwisho wasiku zile picha zika vuja na kupelekwa mtandaoni, na zingine kusambaa kwenye simu za watu.

Ushauri wangu. Wasichana msikubali kupiga picha za utupu, kwasababu zinaudhalilisha uanamke wako na kukuvunjia heshima maisha yako yote. Kwani kitu kikisha ingia mtandaoni, hakitoki. Labda admin aamue kukitoa. Na Watu wanatabia ya kushare, hata mmoja akitoa, wengine wanakuwa wamesha download, na kuweka kwenye mitandao yao, hicho ndicho kibaya zaidi.

Kuna msanii mmoja anatafuta umaarufu kwa kupiga picha za mamna hiyo na kuziweka mtandaoni, yeye amependa je Hao wasichana wanapenda?

Mwisho wa siku tujaribu kukumbuka tuliko tokea

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mimi binafsi toka nizaliwe sijawahi fanya upuuzi huo hivi inakuwaje unapokuwa na mpenzi wako faragha mnaamua kupiga picha za utupu hasa kwa lengo gani?na ukiona mpenzi wako anakupigisha picha hizo ujue wala hakupendi wala kukuthamini manake hayo si maadili,ila baadhi ya watz ni fashion kwao sijui huko kwetu kenya?yaani mtu uache kwenda mbio kutafuta hela ujenge maisha mazuri unafukuzana na picha za uchi mwisho wa siku huyohuyo mpenzi wako anazivujisha,jamani wanawake heshima zetu na utu ziko wapi?

    ReplyDelete
  2. Wengine hyo ni biashara yao bila kuonyesha mauno yao bado hawa jauza kitu hvyo kujiweka wazi wao huwa wanaona ni kupata wateja haraka.

    ReplyDelete
  3. Watanzania kwanini hamujisitahi mpaka mukubali kupingwa picha za uchi,na wanaume zenu wanapiga na wao shenz tap.

    ReplyDelete
  4. Hulka hii imejaa tele kwa ndugu etu wasichana, wengine huona fahari kupiga picha wakiwa watupu, nakumbuka mara moja baada ya kudate na msichana mmoja Dar bila hata kunifahamu vulivyo, ikiwa mara yangu ya kwanza kukutana nae, mara ghafla akaanza kuvua nguo zake na kuniambia ''tafadhali nipige picha' nilishangaa sana kuona binti mzuri mwenye mwili wa kuvutia tena wala sio changu wa kujiuza sijui aliniiamini vipi. hapo nikajua kuwa hiyo kuwa ni hulka ya mtu mwenyewe.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad