ALIYE SHINDA KURA ZA MAONI CHADEMA APIGWA CHINI APEWA NAFASI MSHINDI WA PILI MDADA.


Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi jimbo la Kalenga walivyompongeza Sinkala Mwenda siku ya kura za maoni baada ya kushinda wenzake 13.

KAMATI kuu ya chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imemteua aliyekuwa mshindi wa pili wa kura za maoni katika zoezi la kura za maoni Bi Grace Tendega kupeperusha bendela ya Chadema katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kamati kuu ya Chadema iliyoketi jijini Dar es Salaam leo zinadai kuwa aliyekuwa mshindi wa kura za maoni mwanasheria Sinkala Mwenda hajateuliwa na kamati kuu hiyo mbali ya kuongoza kwa kura kura 132 dhidi ya kura 122 alizopata mpinzani wake wa karibu Grace Tendega 

Katibu wa Chadema wilaya ya Iringa vijijini Felix Nyondo amethibitisha kuwa amepata taarifa hizo za kuteuliwa Bi Grace Tendega kuwa mgombea wa Chadema jimbo hilo la Kalenga .

Hata hivyo alisema anapongeza maamuzi ya kamati kuu na kuwataka wana Chadema Kalenga kujiandaa kwa kampeni za uchaguzi huo na kuanza kumnadi mgombea wao ili kuweza kushinda uchaguzi huo mdogo.

Kutokana na uteuzi sasa Tendega atavaana Godfrey Mgimwa wa CCM katika uchaguzi huo ili kuziba nafasi iliyoachwa waziri na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga marehemu Dr Wiliam Mgimwa aliyefariki mwanzoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo duru za kisiasa kutoka ndani ya Chadema zinadokeza kuwa sababu ya kuachwa kwa mgombea huyo aliyeshinda kura za maoni mwanasheria Mwenda ni kutokuwa na mtaji wa watu kwa maana ya kutokubalika ndani na nje ya chama hicho hivyo Chadema kuona kumsimamisha Mwenda ni kulipoteza jimbo hilo.

Huku kwa upande wa mteule wao Bi Tendega amekuwa na sifa ya kugombea katika jimbo hilo kupitia chama cha Jahazi Asilia na kufanya vema japo si kwa kushinda hivyo nin imani yao kupitia Chadema anaweza kufanikiwa kushinda.
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haijalishi jombo mshalikosa tayari tunarithishiana vyeo katoka baba ataingia mwana kama bole karume na kenyata kwa ipande wa africa na upande wa pili wa dunia bush na baba yake haaaaa poleni chadema mmemnyima haki aliye teuliwa. Na kamati mkampa huyo mama kwa faida zenu Kalenga hatumpi kuraa mshatugawa makundi.

    ReplyDelete
  2. We 8.13 jifunze kwanza kiswahili ndo uje uchangie!

    ReplyDelete
  3. Mwandishi unatuambia mwenda hakubariki ndani na nje ya chama,sasa amewezaje kushinda Kula za maoni?,labda mtuambie Kula za maoni ni kiini macho tu,kunavigezo vyengine viongozi wanaangalia?

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  5. Typing error. Sio swala la kujifunza kiswahili ukweli unabaki palepale hakuna cha kujifunza kiswahili wala sera za chadema wewe unaojua kiswahili umefaidika nini? Pole kwa kujua misamiati ila ukweli kawapa na ueelewa.

    ReplyDelete
  6. Next time,msitutangazie mshindi mtu msitemtaka,maana mnatuchanganya sasa,mpange mshindi mapema ili kukinusuru chama

    ReplyDelete
  7. WAMEVURUNGWA!

    UCHANGA UTAWAMALIZA

    KISA YUKO KAMBI YA ZITTO

    CCM-HAPO MUMEISHAPATA USHINDI!

    ReplyDelete
  8. CDM-KWISHA WAANZISHE KAMPUNI YA ULINZI KWANI SARE C WANAZO!

    ReplyDelete
  9. huo ndiyo ukomavu wa siasa, Chadema oyeeeeeeee!! kama mwenyewe alivyosema "ukishaona mapanya yameingia kwenye gala la chakula, hautachagua paka wa rangi gani umtume huko galani" kwahiyo mapanya yameshaingia kwahiyo Chadema itatuma paka yeyote bila kujali rangi yake kwenda kuyakamata!! Chadema hoyeeeee!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad