ALIYEZAA NA SHILOLE AIBUKA, WAONYESHANA MALAVIDAVI HADHARANI

Denis Mtima, aliyekuwa Igunga, Tabora
KWA mara ya kwanza, mzazi mwenza na msanii wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Elias Makala ameibuka na kujinadi hadharani wilayani Igunga, Tabora.

Tukio hilo lilitokea Februari 14, mwaka huu (Valentine’s Day) ambapo Shilole aliyekuwa amekwenda kufanya shoo mkoani humo, alishindwa kuzuia hisia zake baada ya mzazi mwenzake huyo kujitokeza na kujikuta wakioneshana mahaba mbele za watu.

Pozi hilo la kimahaba liliwashangaza watu na kuanza kudhani kuwa huenda wawili hao wakarudisha penzi lao lililokufa miaka mingi iliyopita.

“Mh! Kweli mtalaka hatongozwi, hebu ona Shilole alivyorembua alipomuona jamaa yake, pale Makala kumchukua ni kama kumsukuma mlevi,” alisema shuhuda mmoja
Baada ya paparazi wetu ‘kuusoma mchezo’ huo, aliamua kumuuliza staa huyo kama penzi lao limerudi upya au laa?

“Hahahahaa! Kwa kweli unanichekesha kuniuliza kama nimerudisha penzi kwa mzazi mwenzangu, huyu ni baba wa mwanangu Joyce, itabaki kuwa hivyo. Siwezi kumtenga na sioni ajabu kupiga naye picha, hakuna kinachoendelea,’’ alisema Shilole.

Licha ya kufafanua hivyo, usiku wa siku hiyo, Shilole alipokuwa jukwaani akipagawisha mashabiki kwa shoo kali, alimpandisha jukwaani mzazi mwenziye huyo hali iliyozua mtafaruku mkubwa kwa mpenzi wa sasa wa Makala aliyefahamika kwa jina la Maguno.

Baada ya shoo kuisha, Maguno aliyekuwa na jazba kwa mpenzi wake kupandishwa jukwaani, alimsaka Shilole kwa udi na uvumba kutaka kumtembezea kichapo lakini bahati haikuwa yake, hakuweza kumpata hadi msanii huyo aliporejea jijini Dar siku iliyofuata.
Credits:Global Publishers
Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mtu mwenyewe anaonekana kachokaaaaaa wa nn sasa kujishusha hadhi alikuwa wapi siku zote

    ReplyDelete
    Replies
    1. afu nyie udaku kuweni makini na tarehe zenu leo ni 19 au 20 mbona mko nyuma na kalenda?

      Delete
  2. Jamaa alitamani zigo lake kama akumbushie vile.

    ReplyDelete
  3. Huyo ndio makala bangi mtu pombe mtu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umenena usoni tu anaonekana kalewa tena pombe za kienyeju

      Delete
  4. ganja planta....

    ReplyDelete
  5. Huyu mkulima ndio anakupendeza nendeni kijijini mkalime uache umalaya hapa mjini.na bangi inaonekana analima mwenyewe huyu babu

    ReplyDelete
  6. Hongera Sana Shilole kwa kukumbuka nyumbani Safi Sana.

    ReplyDelete
  7. Mwenyewe anajiona katokerezeaa na brauzi Yake ya kike cheni shingoni ukute anawanawake zaidi ya watatu wanamgombania

    ReplyDelete
  8. Pole sana shilole na hicho kibabu nafikili usingechomoka tabora ungekuwa umechoka kama jamaa yako ,zile bukubuku za maroli ndiyo zilikuwa zinakuzingua ,siunaona hata hampendezi mtoto wowow safi zamani tulikuwa tunaona kwenye magazeti ya sani siyo kwamba hawakuwepo ila walikuwa wanavaa nguo za kujisitili siyo kama zako, ukibakwa ooo kanibaka mungekuwa mnavaa hivyo hivyo mahakamani uone kama hakimu uzalendo haujamshinda utasikia kooti naomba kwenda kuongea na mlalamikaji faragha kidogo halafu tutaendelea.

    ReplyDelete
  9. malaya haachi asili

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad