ANAYEONA POSHO YA BUNGE LA KATIBA HAITOSHI AFUNGASHE VIRAGO VYAKE

Dodoma. Wizara ya Fedha imepigilia msumari maombi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ya kutaka waongezewe posho na kusema anayeona ameacha kazi inayomlipa zaidi kwenda bungeni afungashe virago na kuondoka.

Msimamo huo umekuja siku moja tu baada ya gazeti hili kudokeza kuwa madai ya wajumbe wa bunge hilo kutaka waongezewe posho kutoka Sh300,000 za sasa kwa siku, yamegonga mwamba baada ya kamati iliyoteuliwa kuchunguza uhalali wake kusema kiwango hicho kinatosha.

Mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Pandu Kificho alisema jana bila kutaja viwango, kuwa ripoti ya kamati hiyo imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi.

Madai ya wajumbe kutaka waongezewe posho, yamechafua hali ya hewa ndani na nje ya Bunge, huku baadhi ya wananchi wakipaza sauti zao na kumsihi Rais Kikwete alivunje bunge hilo iwapo wajumbe watashikilia msimamo wa kutaka nyongeza ya posho.

Jana, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema wanaoshiriki kutunga Katiba ni Watanzania na siyo wataalamu washauri waliokodiwa kutoka nje.

Alisema kwa msingi huo, Serikali ilitarajia kuwaona watu hao wakitanguliza uzalendo zaidi badala ya kudai malipo manono.

“Katika kutengeneza Katiba hii, hatujakodi consultants (wataalamu washauri) kutoka Uingereza, Marekani, Kenya, Uganda wala nchi nyingine yoyote… Hawa ni Watanzania na kazi wanayoifanya ni yao,” alisema.

“Wangekuwa wataalamu wa kukodi wangeweza kudai malipo hayo, lakini hapa ni tofauti... wanafanya kazi yao na kila mtu anafanya kazi yake na anapaswa kujivunia kushiriki katika tendo hili la kihistoria kwa kutanguliza uzalendo,” alisema.

Nchemba alisema anazielewa hoja za baadhi ya wajumbe walioibua suala la posho, lakini kwa mtazamo wake, hoja hiyo hata kama ingekuwa na mashiko kiasi gani, imewasilishwa wakati usiokuwa mwafaka. Alisema wapo makandarasi na wazabuni waliotoa huduma kwenye taasisi mbalimbali za umma lakini hawajalipwa.

Alisema kwa kawaida, Februari ni mwezi mbaya kwa kuwa baadhi ya wilaya zina historia ya kukumbwa na uhaba wa chakula hivyo kuhitaji fedha nyingi za Serikali ili kuokoa maisha ya watu katika maeneo hayo.

Pia alisema si wakati mwafaka wa kudai nyongeza hiyo hasa ikizingatiwa kuwa kuna walimu wapya 30,000 nchini kote ambao hawajapangiwa vituo kutokana na kukosekana kwa fedha za kulipa stahiki zao.

Nchemba alisema mbali na walimu hao wapya kutokupangiwa vituo, walimu wengine wanadai malimbikizo ya fedha zao na kwamba hawajalipwa kutokana na ufinyu wa bajeti serikalini.

“Siku zote ukweli unauma. Nasema kama kuna mjumbe ambaye anaona huko alikokuwa kabla ya kuteuliwa alikuwa anapata pesa zaidi kuliko hii, basi kwa heshima afungashe virago na kuondoka,” alisema.
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ebwanae hapo umesema vizuri na nimekuelewa,ikiwa hiyo posho waongezwe nikazi ipi wataifanya ambayo wataeidhia malipo hawa hawa viongozi wetu wengine niwazembe na kutaka kuhipalilia wao tu sio kufanyakazi inavyo takiwa.

    ReplyDelete
  2. yes bwana mkubwa mchimbi kumamake wambie, wakafie mbele

    ReplyDelete
  3. Aaa mi huwa nakuamini bwana mwigulu kiukweli rais hakukosea kabisa kukupangia nafas zote unazowakilisha kaza but watanzania weng tupo nyuma yako

    ReplyDelete
  4. Serikali ndio imeonyesha mfano mbaya kutokana na mfumo tulionao umefanya uzalendo na ubinadamu kutotiliwa kipaumbele bali maslahi tena yenye ulafi.Vizazi vilivyopo vinagawanyika toka shule,mwenyenacho anakwenda shule nzuri asienacho toka shule,matibabu nk ni duni.Ikiwa serikali inaweza kumpa billioni 6 Mzindakaya na nyumba 15 azipangishe kwa nini mbunge asione kuwa posho haitoshi.Tuangalie pande zote mbili tokea awamu ya pili utu kwa nchi yetu unazidi kudidimia!

    ReplyDelete
  5. hamna lolote, huyu ni hao hao, anataka tu kujipatia umaarufu tu hapa, tangu nimsikie huyu bwana sidhani kuna zuri lolote ambalo nimemsikia nalo!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata hili nalo sio zuri? au na ww ndo walewale vichwa vizito?

      Delete
  6. waondoke waachie wenye kuridhika na hicho kiasi pumbavu yanapenda kula sana

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad