BAADA YA BAADHI KUJIUNGA CCM-BONGO MOVIES VIPANDEVIPANDE!

Stori: Waandishi Wetu
MPASUKO mkubwa umeikumba tasnia ya filamu Bongo baada ya baadhi ya wasanii wanaong’ara kuchukua kadi rasmi za kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.

Tukio hilo lilitokea juzi, Jumapili jijini Mbeya kulipokuwa na sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais Jakaya Kikwete.

Mashabiki mbalimbali wa sinema za Kibongo, waliingia kwenye mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii, mara baada ya wasanii hao kuonesha uamuzi wao, kila mmoja akieleza mtazamo wake.

WASANII WENYEWE
Baadhi ya wasanii waliochukua kadi za CCM ni pamoja na Jacob Steven ‘JB’, Single Mtambalike ‘Richie’, Irene Uwoya, Haji Salum ‘Mboto’, Tamrina Posh ‘Amanda’, Blandina Chagula ‘Johari’, Wastara Juma na Haji Adam ‘Baba Haji’.

MIJADALA
Watoa maoni walikuwa na mawazo tofauti kuhusiana na uamuzi wa wasanii hao wenye mashabiki wengi, wengine wakiwapongeza huku upande wa pili ukiwashutumu kwa maelezo kuwa wanawagawa mashabiki wao.

Mtoa maoni aliyejitaja kwa jina la Mussa Juma aliandika: “Sijui hawa wasanii wetu watakua lini? Huwezi kuonesha itikadi yako ya kisiasa wakati una mashabiki wengi. Hapo wamechemka. Mfano mimi siyo CCM na siwezi kununua tena filamu za JB.”

IPYANA LWIGA:
“Hii ndiyo demokrasia, unawavuta watu wajiunge kwako kwa kuwapa usafiri na mahitaji yote muhimu! Wameona mbali sana, nawapongeza sana! Wajifunze kwa Marlaw!”

BENATUS MARWA NYAMBORI:
“Huo ni uamuzi wao. Hauhusiani na kazi zao. Kama umechukia, chukua kazi zao zote piga moto. Kiukweli Chadema mnafikiri watu wengi wanawasapoti? Hapana... huko vijijini wanakuja kuangalia helikopta maana hawajawahi kuiona.”

JACOBS KING:
“Sasa hivi ndiyo watakoma kabisa, najua hakuna wa kununua kazi zao, wataibiwa mpaka wakome, CCM wanataka kuwatumia kwenye kampeni mikoani ili wawavutie wananchi kwenye mikutano yao lakini kwa sasa Watanzania tunajielewa.”


COCU BATENGA: 
“Wasanii wana haki ya kuchagua chama chochote wakipendacho. Wakati wa kazi ni kazi, siasa ni siasa. Mbona Sugu (Joseph Mbilinyi – Mbunge wa Mbeya Mjini) yupo bungeni? Mbona Afande Sele (Seleman Msindi) ametangaza kujiunga Chadema, mbona hayasemwi? Hakuna mantiki hapa.”

JB BUNGENI
Hivi karibuni, JB alitangaza nia yake ya kugombea ubunge ingawa bado hajataja jimbo, kitendawili cha atagombea kwa tiketi ya chama gani, kimeshateguka baada ya kuchukua kadi ya CCM.

Hata hivyo, minong’ono inasema kwamba, JB huenda atagombea Jimbo la Kinondoni (kwa sababu ndiyo eneo analoishi) au Same (kwa sababu ni mzaliwa wa huko).

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yani hapa Tanzania Luna watu mabwege sana inamaa domokrasia yakwei ni kusapoti upinzani.msanii kuamia chama tawala ndio usinnue cd zake? na pia inamaa huko alipo amia hakuna mashabiki wake,mi sitaki kuamini kua watu wanaoandaa hizi mijadala hawa upeo kiasi hicho

    ReplyDelete
  2. sasa tatizo lipo wapi? mbona hata nchi zilizoendelea wasanii hujitokeza hadhalani na kujitangaza kumuunga mkono mgombea wa chama furani na watu still wananunua kazi zao? ot tatizo ni kujiunga CCM? acheni upumbavu kila mtu ana uhuru katika imani yake kwa kitu akipendacho! Jb na wenzako pigeni job nzuri tutanunua

    ReplyDelete
  3. JZ na Beyonce walipiga campaign kwa Baraka Obama na still wako juu na mziki unaendelea kama kawaida,sioni kosa la wasanii kujiunga na CCM mbona Sugu na Sele wako Chadema watu hawajawasema Watanzania wenzangu t tubadilikeni kila mtu anauhuru wa kuchagua Chama anacho kitakawee kama Chadema mwaga sera zako wavutie watu wajiunge acheni kulalamika!!

    ReplyDelete
  4. HAWA NDO WASANII LEO CCM KESHO CHADEMM

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad