KIPUTE CHA LEO KOCHA WA YANGA ASEMA"KILA NAFASI BAO"

Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanatumia kila nafasi wanayopata kufunga bao dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Yanga na Al Ahly zitakutana kesho katika pambano la raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga ilitinga hatua hiyo baada ya kuibwaga Komorozine kwa kuicharaza  jumla ya mabao 12-2, ikiwa ni baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 nyumbani na ushindi wa mabao 5-2 ugenini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Pluijm alisema anaamini njia pekee itakayomwezesha kuizamisha Al Ahly ni wachezaji wake kupachika bao katika kila nafasi watakayopata.

“Tulishinda mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwa sababu tulikuwa makini kutumia nafasi. Jambo zuri ni kwamba uwezo wa kutengeneza nafasi tunao  hivyo ni wajibu wetu kuzitumia,” alisema Plyuijm.

“Nataka  tunatengeneza nafasi nyingi basi na mabao yawe mengi. Tukiwa makini katika hilo sina shaka kwamba tutawafunga.”

Katika hatua nyingine, Pluijm alisifu mazingira ya kambi yake kwa kusema hayana tofauti na yale waliyoweka nchini Uturuki mapema Januari.

“Hoteli ni nzuri pia uwanja tunaoutumia kufanyia mazoezi ni bora kabisa kiasi ambacho kimemfanya kila mmoja wetu kuifurahia,” alisema Pluijm.

Hata hivyo, Pluijm alishindwa kuthibitisha kama atamtumia beki Mbuyu Twite ambaye aliumia wakati wa mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting.

“Twite jana (juzi) aliniambia anajisikia maumivu, lakini leo amefanya mazoezi hivyo nasubiri kama atakuwa fiti hadi kufikia Jumamosi lakini kwa sasa siwezi kusema moja kwa moja kama nitamtumia au la,” alisema Mdachi huyo.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. leo mwaarabu lazima wasahau basi na kukimbilia bajaji kama tambwe, sababu ya kichapoooo!! leo anapigwa za wikiiiii!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad