KUNDI LA WASANII KUJIUNGA CCM KWA PAMOJA...NI KUPENDA KWAO AMA KUNA USHAWISHI?

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na Mtindo wa Wasanii wa Fani Mbali mbali kujiunga na Siasa hasa wasanii kutoka kambi ya Bongo Flava...Mfano Sugu , Vick Kamata, Afande Sele, Roma na Wengine...Hii imekuwa sasa kama staili ukichukulia kwamba wasanii hao wana ushawishi mkubwa kwa Jamii yetu ya Kitanzania
Jana kuna Kundi la wasanii ambao wamejiunga CCM...Nilipost habari hiyo na Watu wametoa hisia tofauti tofauti kuhusu tukio hilo la Wasanii Wengi kwa Pamoja kuingia CCM wengi wamekuwa na shaka kuhusu hilo na kuuliza maswali yasio na majibu ...Wasanii hao walionekana wakipanda ndege ya Fast Jet Kuelekea Mbeya kwa Makundi ...Je wewe Unaona ni sawa na wamejiunga kwa kupenda kwao ama kuna ka ushawishi ? TOA MAONI YAKO
Udaku Specially Blog
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mtu kujiunga na chama ni uhuru wa mtu

    ReplyDelete
  2. Kumamazenu mlitaka ajiunge nani? Hii issue ndo imezua gumzo mbona kuna mengi ya kuongelea akha,kwa nini tusijadiri jinsi ya kutafuta mbinu ya kukomesha huu mchezo mchafu...niuseme au?

    ReplyDelete
  3. Hii danganya toto mbona wasijiunge siku za nyuma zilizopita yan mtu aache kuchukua kadi ya ccm dar aende mbeya kirahis tu tena kwa ndege kufuata kad ya ccm!wenzenu wameshatengeneza hela nyie humu ndan mnachongaa!

    ReplyDelete
  4. WAANGALIE WOOOTE HAOO, UJARIBU KUFUATILIA ELIMU ZAO. NDIO MAANA WANASHOOT VIDEO WANAZIITA FILAMU ZA KITANZANIA. HATA FILAMU MAANA YAKE HAWAJUI. KWA WALE TULIOSOMA KISWAHILI TU CHA 4M4 KUNA TOFAUTI KUBWA SANA YA FILAMU NA MAIGIZO AU TAMTHILIA. BONGO MUVIE BONGO LALAA BONGO MUSIC, TAALUMA AMBAYO UBONGO HAUTUMIKI. WATAISHIA KUONESHA VIDEO ZAO USWAHILINI NA KUONESHWA KWENYE MABANDA YA MIAMIA

    ReplyDelete
  5. Ni wajibu wa vyama kushawishi( mobilize ) wanachama wapya,hata hivyo uamuzi wa mtu kujiunga ni wake binafsi, wote hao ni watu wazima.

    ReplyDelete
  6. Kwani wewe ulikatazwa shekhe au bibiii kila mtu nanjaazake bongoiii iyangalie vizuri na post zako ohoo "Bongo darisalamii"

    ReplyDelete
  7. Nawewe jiunge na chadem

    ReplyDelete
  8. wameishiwa hawa, wanatafuta hela za kujikimu toka ccccccmmmm, hawajui hizo ni hela za wananchi wanapewa!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad