LEO KUMEKUCHA KESI YA MBUNGE MAARUFU WA CHADEMA NA CHAMA CHAKE MAHAKAMA KUU HAPATOSHI LEO LIVE

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini alifungua kesi hiyo dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema, akiiomba mahakama hiyo ikizuie chama kujadili uanachama wake, hadi rufaa anayokusudia kuikata Baraza Kuu la chama kupinga kuvuliwa nyadhifa, itakaposikilizwa.


Katika kesi hiyo namba 1 ya 2014, Zitto pia aliiomba mahakama hiyo imwamuru Katibu Mkuu wa Chadema ampatie mwenendo na taarifa za Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichomvua nyadhifa zote alizokuwa nazo ndani ya chama na iwazuie walalamikiwa kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake kama Mbunge wa Kigoma Kaskazini.


Kesi hiyo ambayo inasikilizwa na Jaji John Utamwa imepangwa kuanza kutajwa leo kabla ya kupangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa rasmi.

Tayari mahakama imeshatoa amri ya zuio la muda kwa Chadema kumjadili na au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake.


Uamuzi huo ulitolewa Januari 7 na Jaji Utamwa, kutokana na maombi ya Zitto, kupitia kwa Wakili wake Albert Msando.


Awali mawakili wa Chadema, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu na Mkurugenzi wake wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala walipinga maombi hayo wakidai kuwa hayajakidhi matakwa ya kupewa zuio la muda.

Katika uamuzi wake, Jaji Utamwa alikubaliana na hoja za Wakili Msando kuwa maombi hayo yametimiza matakwa yote ya kupewa zuio hilo.
CHANZO NI MWANANCHI
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ushauri wangu kwa kabwe, nenda ccm tu achana na Chadema, huku kwetu hatukutaki, unasikia bwaa mkubwa, tokea siku nyingi tulikuwa tunajua wewe ni mamluki, pamoja na Chadema kukuinua kimaisha, kama si Chadema usingekuwa hapo ulipo bwaa mkubwa!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ww unaonyesha ni shoga tena uatombwa na mtei

      Delete
  2. Leo hamumtaki ktk chama chenu na majina yote mabaya mme mpaka,M'mbwa yeye,kirusi yeye baada ya kuonyesha msimamo wake,wakati akimwaga cheche Bungrni nyienyie ndio mliokuwa wa kwanza kumsifia Mbunge kijana analipeleka bunge mbio,ndio raisi wetu wa 2015???? ,yiko huru Chada hatoki na wala CCM haendi kitaeleweka tu mnyonge mnongeni lakini haki yake mu mpe,asilimia kubwa ya viongozi wa vyama vyote Tanzania hawapendi kuambiwa ukweli au kuulizwa !!! Ni utawala wa Kidikteta ikitokwa watu kama zito waropokaji basi lazima wawekwe kitako na kuanza kupandikizwa chuki ktk jamii,,Poleni wapenzi wa Siasa ila siku zote siasa mchezo mvhavu!!?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wambie, wana roho hata motoni wanaishi, kuma hao na chopa zoote wameambulia kata 3 aib serikali za mtaa 2nasubili cdm kwisha

      Delete
    2. Mgonjwa wa akili utamgundua tu kwa kauli za matusi yake,pole Mirembe hosp.inakusubiri!

      Delete
  3. mmmh! c lazma kutukana ! matus ni kipimo tosha cha uelewa tulionao,

    ReplyDelete
  4. kwani hapo juu waliotukana ni nani? utawajua tu watoto wa shule za kata waliolelewa na cccccmmmm ya leo, hayana akili, wala hoja, kazi ni kutukana tu, mchukueni huyo zito wenu, hatumtaki!!

    ReplyDelete
  5. tamaa mbaya utakuja juta zito unacheza na ccm, watakutumia mwisho wa cku tupa kule

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad