MAHAKAMA YAAMURU JENGO LINALOCHUNGULIA IKULU LIPUNGUZWE UREFU

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mkuu, Richard Maliyaga, kila mmoja kulipa faini ya Sh15 milioni au kwenda jela miaka tisa baada ya kuwatia hatiani kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuruhusu ujenzi wa jengo la ghorofa 18 karibu na Ikulu.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo alisema jengo hilo lilipaswa kuwa la ghorofa sita na kuamuru kubomolewa kuanzia ghorofa ya saba kwenda juu.

Hakimu Fimbo alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 13 wa upande wa mashtaka, vielelezo 20 vilivyowasilishwa na ushahidi wa utetezi uliotolewa na washtakiwa wenyewe, upande wa mashtaka ulithibitisha pasipo shaka mashtaka dhidi ya vigogo hao waliodaiwa kuruhusu ujenzi wa ghorofa 18.

Hivyo aliwahukumu washtakiwa hao kila mmoja kulipa faini ya Sh5milioni au kutumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kila kosa lililokuwa likiwakabili. Kila mshtakiwa alilipa kiasi cha Sh15 milioni mahakamani hapo na kuepuka kifungo.
Baada ya hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alisema ndani ya kipindi cha miezi sita baada ya hukumu hiyo kutolewa, Kifungu cha 40, namba 1 na 2 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kinawaruhusu kutaifisha jengo hilo.
Washtakiwa hao walikuwa wakitetewa na Mawakili Majura Magafu na Paschal Kamala.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mambo ya kuhonga hayo. Wakome kutoa vibali kinyume cha sheria . Ama usikute hawakuucheck na wstaslsmu kuwa gorofa 18. Zitakua ndefu sana. Uzembe kazini au watu hawajui kazi zao?

    ReplyDelete
  2. Kwani huko ikulu kuna nini hata kusichunguliwe aaah mpisheni mieeeeeeee

    ReplyDelete
  3. Wakuchungulie sana kafenge wewe jakaya

    ReplyDelete
  4. Mamlaka Ya Majengo ilikuwa wapi? wakati wanaanza kujenga hadi waje kushtuka wamesha malizaa!? huwo ni utumiaji wa madalaka kizimamoto zimamoto.

    ReplyDelete
  5. wanaandaa njia ya kwenda mbinguni!

    ReplyDelete
  6. acheni ujinga kwani ilikuwa amuoni ikijengwa??? tena ikulu sio ata porini!!! hii nchi vipi???

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani Hii Nchi Huijui Likishatokea Ndio Wanachukua Hatua Sasa Kama Ni Mambo Yao Si Wameshafanya Kipindi Jengo Linajengwa

      Delete
  7. hii kali! hivi nanyie mahakimu mnadhambi kabisa mjengo umejengwa hadi kuanza kutumika leo unaanza kuzaa matunda mnaleta kelele yaani!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad