MALINZI:TUMERITHI ZIGO LA MADENI TOKA KWA TENGA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema changamoto kubwa linaloikabili sasa ni madeni ya mamilioni ya fedha waliyoyarithi kutoka uongozi uliopita wa Rais, Leodegar Tenga.

Akizungumza na Mwanaspoti katika tathimini yake ya siku 100 tangu alipochaguliwa kuwa rais mpya wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi, alisema madeni hayo ni makubwa ukilinganisha na kipato cha TFF kinachotegemea zaidi mapato ya milangoni ya mechi mbalimbali.

“Madeni tuliyoyakuta ni makubwa, lakini mengine tumegundua ni hewa, hivyo yanafanyiwa uhakiki ili tujue madeni halisi ili tuweze kuyalipa,” alisema Malinzi aliyeingia madarakani Oktoba 27, mwaka jana.

“Pia tunafanya mazungumzo na watu wanaoidai TFF ili watupe masharti nafuu ya kulipa madeni hayo.”

Kauli ya Malinzi imekuja ikiwa imepita miezi sita tangu TFF ipate aibu ya mabasi yake kukamatwa na Kampuni ya Udalali ya Flamingo ili kufidia deni la zaidi ya Sh50 milioni.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmeshaanza majungu ok sema unadaiwa bei gani? Na ni akina nani wanakudai? Kaka ilikuaje kuhusu Okwi? Mbona mnafanya vitu vya kiupenzi kukomoana mnategemea kukuza soka tutafika kweli. Yani kuhusu okwi mmefanya vitu ambavyo avijawahi tokea kwani mlitakiwa toka inaletwa leseni yake ilitakiwa muoji sasa wenzenu wameleta leseni bado sku m1 mnazuia na mnaifanyia ivyo timu m1 tu mara ngasa kasaini mata mbili sasa je uyo aliyemsanisha mara mbili mlichukulia atua gani. Isije kutokea kama ya Misri kuana viwanjani
    Leo wapenzi wayanga awana ata kidogo uaminifu na tff

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mada nyingine na coment nyingine! Duh waTz Mungu tusaidie.

      Delete
  2. hatuna uaminifu na hawa jamaa wa TFF hata kidogo, wao kazi yao kuishobokea Yanga tu, sijui wanatatizo gani nayo, Okwi alikuwa kesha ruhusiwa na FIFA na CAF, wao wakaa kikao sijui hiko kikao kilikuwa cha nini? na kuanza kumjadili Okwi bila ya sababu yeyote, sasa hivi mchezaji yuko nje, hayajui yanaua kiwango chake, Ngasa alilimwa faini, lakini hao waliomsainisha wakijua wanafanya makosa, mbona wao wameachiwa, vipi hawa TFF? upumbavu mtupu!

    ReplyDelete
  3. nyie ttf mnajiumbua wenyewe kwa kukurupuka, haya sasa tuambieni suala la Okwi, mlikuwa na kizunguzungu au?

    ReplyDelete
  4. nyie ndiyo mnaliua hili soka la TZ, na wala c simba au Yanga kwa tamaa za mitumboo yenu, kikao cha kumjadili Okwi mlikaa ali mlipane posho, pumbaf!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad