MDAHALO WA WAZI KATI YA DR SLAA NA DR KITILA MKUMBO

Bila shaka huu ni wakati muafaka sana ambapo inafaa kuwa na mjadala wa wazi kati ya Dr. W.Slaa na Dr. Kitila mkumbo juu ya "Tanzania na siasa tunayoitaka"

Nasema hivi kwa sababu, Kwa takriban miezi miwili mfululizo, Dr.Kitila amekuwa akiandika makala zenye maudhui mazito ambayo hayawezi kupuuzwa.Katika makala zake zote, zimekuwa zikionesha maudhui ya ujumla kwamba siasa za upinzani tanzania kwa sasa zimegeuka na kuwa ni sawa sawa tu na zile za CCM au pengine hata kuwa na udhaifu zaidi hata ya zile za CCM.kwa ujumla Dr.Kitila yeye anadhani pengine hilo linaweza kuwa ndio sababu kuu ya watanzania kuamua kuichagua CCM tu(LICHA YA UDHAIFU WAKE), huku upinzani ukianguka.

Kwa mfano Kitila Katika moja ta makala zake anasema "Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua."

Bila shaka unahitajika mjadala kati ya hawa Madaktari wawili ambao wote wana shahada ya juu ya falsafa (Dr.Slaa Vs Dr.Kitila), ili kupitia mjadala huo mambo haya yote yakawekwa sawa kwa hoja na vielelezo vya wazi na watanzania wakapata picha kutoka kwa watu wenye weledi na uelewa wajuu.

Naamini kama mjadala huo utafanyika, basi kutokea hapo, wadau wataweza kujadili wakiwa na msingi mzuri na imara wa marejeo, Badala ya utaratibu huu wa kila mtu kuibuka na kutoa hoja yake kwa wakati wake.
Credits:Jamii forums
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mkumbo bado MDOGO Kwa slaa lakini pia hatachangia kisomi Kwa sababu ya tension ya kutimuliwa so sidhani kamaatachangia vizuri

    ReplyDelete
  2. dr.kitila atachangia vizur! kwan huyo slaa mwenyewe anapanik juzi ktk oparasheni zao alisema"anaemtaka zitto amfuate"kisa mabango yaliyo andikwa"zitto mmemuonea" wananchi hana jipya hoja za zitto kabwe zimemshinda richa ya kutumia fedha,wafuasi,chopa,na cd kumchafua zitto!

    ReplyDelete
  3. Hata elimu kitila ni Dr wa ukweli cjui hii ya slaa ya uchungaji inakua vipi.huwezi kumlinganisha na slaa na PHD ya kutunukiwa

    ReplyDelete
  4. Kitila ana PHD ya elimu,na cyo siasa kuwa na elimu kitu fulani cyo kuwa mwanasiasa mzuri,hawezi kushindana na Slaa maana c wa kiwango chake.

    ReplyDelete
  5. hadhi ya dr. Slaa kisiasa na hata kiuelewa imeshuka sana kwa sababu sasa hivi hana tena mawazo tegemezi kwa vile pamoja na udaktari wake anaendeshwa na mawazo ya Mbowe, nafahamu hili litapingwa na wakereketwa wa Chadema lakini ukweli ndiyo huo na ni vigumu sana kwa chadema kukuwa kisiasa kwa vile ni kweli wanachokifanya sasa hakina tofauti na yanayofanywa na ccm.ufisadi wanaoupigia kelele umeshatua na kuwaganda kwenye chama ninaamini mdaharo huo hautapewa baraka na chama kwa hiyo sio rahisi kufanyika

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad