NANI ANASEMA POSHO YA SH 300,000 KWA SIKU HAZITOSHI BUNGE LA KATIBA

Hata kabla ya kupita wiki moja tangu Bunge Maalumu la Katiba kuanza rasmi shughuli zake, wajumbe wake wameendelea na vituko kiasi cha kutupa wasiwasi kama kweli wengi wa wajumbe hao wanastahili kutuwakilisha katika chombo hicho kufanya kazi ya kihistoria ya kutunga Katiba Mpya. Tulisema jana kupitia safu hii kwamba wengi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba hawaonyeshi kama kweli wanatambua nafasi na hadhi waliyonayo kama wawakilishi wetu katika chombo hicho, kwani vitendo na kauli zao vinajenga picha tofauti. Ndiyo maana tulionya kwamba Bunge linapoanza shughuli zake kwa kutawaliwa na vioja na vituko haliwezi kamwe kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Ni jambo la kusikitisha kuwa, pamoja na angalizo letu kwa wajumbe wa Bunge hilo, jana na juzi tulishuhudia mwendelezo wa vitendo vya aibu ambavyo kwa vyovyote vile siyo tu vimekidhalilisha chombo hicho, bali pia vimeibua maswali mengi miongoni mwa wananchi ambao wamehoji kama kweli Bunge hilo limeundwa na watu wenye sifa na hadhi ya kuitwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba. Kilele cha vioja na vitimbi hivyo ni pale wajumbe wengi walipozusha zogo mithili ya watoto wa chekechea kwa madai kwamba posho ya Sh300,000 wanazopewa kila siku hazitoshi na badala yake wanataka wapewe Sh420,000.

Ni kichekesho cha karne kwamba akili za wajumbe wengi, badala ya kuelekezwa kwenye ufanisi wa shughuli za Bunge hilo kama kudai wapewe makabrasha yenye nyaraka zilizoandaliwa vizuri au nakala za kutosha za Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, zimeelekezwa kwenye fedha na kuchumia matumbo yao. Tayari wamesahau kwamba waliteuliwa kuingia katika Bunge hilo kujitolea na kujitoa mhanga ili kuhakikisha inapatikana Katiba Mpya na siyo kugeuza uwakilishi wao katika Bunge hilo kuwa ajira.

Kichekesho kingine ni kwamba madai hayo ya kipuuzi waliyatoa wakati wa semina waliyoandaliwa kwa ajili ya kupatiwa rasimu ya Kanuni zitakazoongoza shughuli za Bunge. Badala ya kuzungumzia rasimu hiyo, wajumbe walilifanya suala la posho kuwa kipaumbele chao na kutaka walipwe viwango vya posho kama makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba walivyolipwa, huku wakipuuza ukweli kwamba makamishna hao na madereva wao walistahili kulipwa viwango hivyo kwa sababu walisafiri nchi nzima, tena katika mazingira magumu na kufanya kazi usiku na mchana. Uzoefu wetu umetuonyesha kwamba wengi wa wajumbe wa Bunge hili watatumia muda mwingi kuchapa usingizi au kukacha vikao. Ndiyo maana wanataka walipwe posho hata wasipohudhuria vikao.

Kwa sababu ya woga usiokuwa na msingi wowote, uongozi wa Bunge umesikiliza upuuzi huo na kuteua kamati ya watu sita eti kwenda kuona ugumu wa maisha ulivyo mitaani. Badala ya kusimamia ukweli kwamba Sh300,000 ni nyingi sana kwa matumizi ya kila siku, uongozi wa Bunge na Serikali sasa utakuwa unaandaa mkakati wa kuongeza posho hizo. Hii ni kinyume na hali ya uchumi wa nchi yetu ilivyo, kwani Serikali imeelemewa na Deni la Taifa la zaidi ya Sh27 trilioni, kwa maana ya Sh20.23 likiwa deni la nje na Sh6.81 trilioni likiwa deni la ndani ambalo Serikali imeshindwa kulilipa. Tusisahau kwamba ukarabati wa Ukumbi wa Bunge umegharimu zaidi ya Sh8 bilioni.
Credits:Mwananchi
Tags

Post a Comment

25 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. baadhi ya hawa watu hawastahili kabisa kuwemo, sababu yamekwenda kule kuvuna na siyo kwa manufaa ya mtanzania, we posho ya 300,000/= kwa siku, kwa siku ni ndogo? halafu uko dodoma ambapo usafiri pamoja na malazi yako chini compare na miji mingine!! yanatania hayo hayana hata aibu, upumbavu wao hao wengi wananyumba ndogo wanataka kutumia hela za walipa kodi kwenye mambo yao ya kihuni, pumbaf!

    ReplyDelete
  2. Baba wa taifa shuka uone jinsi watanzania walivyokengeuka? hivi kizazi hiki kimeingiliwa na mdudu gani? kila mtu anaangalia MASLAHI BINAFSI! hivi yule mwananchi wa kijijini ambaye kula yake tu ni bahati nasibu, mkulima ambaye analazimishwa kuuza mazao yake serikalini kwa bei nafuu, kutwa anadanganywa kwa ahadi hewa za maisha bora atatathmini vipi hili jambo? yani badala ya kujipanga waone ni jinsi gani wataikabili kazi iliyowapeleka pale na kuifanikisha ndani ya muda uliopangwa, wao wameanza na kuunda kamati ya kushinikiza posho! hivi hizi rekodi mnazoweka kwa kizazi kijacho si kitawalaani! wataseme hivi ndivyo wazee wetu walivyo behave? hii ni aibu kubwa na mtikila alivyosema hili ni bunge la kihuni ni kweli mnajionyesha hivyo, hivi kweli mnaangalia maslahi ya taifa ? na ya vizazi vijavyo? hata nchi majirani na mataifa yanayoisaidia tanzania watashangaa! hivi wanaotoa misaada kusaidia nchi hii mnadhani wanatoa wapi fedha? hizo ni pesa zimepatikana kwa wao kujinyima? sasa wewe unayepewa msaada unataka kutapanya, jamani muogopeni MUNGU! Hapanidipo tunapoona hali halisi ya mtazamo wa watanzania! UKIPATA NAFASI ITUMIE! USIJALI WENGINE! NI UBUNAFSI! alafu mnasema hii nchi ya kijamaa! kizazi hiki kimeharibika na ni wazi kabisa kwamba labda tutegemee vizazi vijavyo ndivyo vije kuiokoa nchi hii. Sisi wazazi tunajaribu kuwalea watoto wetu wadogo katika mtazamo tofauti wa kutokujiangalia wao wenyewe, ili tubadilishe mtazamo wa kizazi hiki cha nyoka, maana hii ni dhambi! hebu angalia ufisadi unavyofanyika serikalini! inatisha jamani! hivi tutaendelea kweli! na hakuna wanaochukuliwa hatua! NATAMANI SIKU ATOKEE KIONGOZI SERIOUS AOKOE NCHI HII! TABIA YA KULINDANA NDIO INAANGAMIZA TAIFA HILI! KAMA YULE WA KOREA YA KUSINI, LABADA WATU WATASHIKA ADABU!

    ReplyDelete
  3. Laki 3 ni kwel haitoshi jaman waongezweeeeeee

    L

    ReplyDelete
    Replies
    1. shwain wewe ndo walewale eeeee

      Delete
    2. Sio shwaini ni zaidi natamani nimtukane ila sijuagi jamani naombeni kunisaidia kumtukana Huyu msenge anayeunga mkono laki tatu hazitoshi labda baba Yake ni fisadi

      Delete
    3. Usimtukane sana, hawara'ake yupo katika hilo DUDE la katiba!

      Delete
    4. Haona haja ya kimtukana kuma huyu!

      Delete
    5. Dah! Watanzania ni wajingaaaa saaanaaa tena ni malimbukeni hawajiwezi. Hakuna atakayeandamana kupinga ukubwa wa hiyo posho. Kwa sababu kitendo cha kuibuka mitaani na kuandamana mtapigwa kwa sanaaaa kama mbuzi. FFU watatanda mabarabarani na kuwamwagia pilipili usoni. Tena watanzania wenyewe ni mambumbu wa kutupwa hawana uwezo wa kutafakari mambo kwa kina na wala kiusomi. Watanzania wanaendeshwa kama gari bovu duh! Lahaula! Ndio nchi hiyo ya wajinga na wapumbavu. Na dhubutu zenu mkileta ujinga tutawatandika na FFU wapo tayari wamekaa mkao wa kula. Tena mkae mbali kabisaaa.......

      Delete
  4. imenisikitisha sana ni dhahili kuwa hawa watu hawafai kabisa kuwa katika hili bunge ni wazi kabisa walichokifata huko ni pesa na si kitu kingine, wamenikasirisha sana kama ningekuwa rais walah mlango walioingilia ndio walitakiwa kutokea, hebu tujiulize laki tatu hata haifiki kima cha chini cha mshahara na ana familia na anasomesha,leo mtu anapewa laki tatu kwa siku anacompleain, ujue hawa watu hawana maana kabisa na hawatufai hata kidogo ujue nimekasirika sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani unishindi Mimi kwani Hasira yangu nimeshindwa ata kula ninalia kwa jinsii wanavyotunyonya Sisi wanyonge

      Delete
    2. Mtaishia na porojo zenu humu humu kwenye haya mablog yenu feki. Hamna uwezo wa kuandamana wala kuupinga huo ufisadi. Siku ya siku wote kimya. Mafisadi wanajilia vyao kiulainiiiii na nyie mmekaa hapo hapo na porojo zenu. Kama kweli mmesikitishwa na huo ufisadi nendeni mkaweke mabango pale nje ya ukumbi wa bunge muone cha mtema kuni. Kama hamkutandikwa na kugalagazwa galagazwa nyoooo......
      mtaishia humu humu na story zenu uchwara. Ikulu ile pale?? Kwa nini msiandamane mpaka pale magogoni? Mnachoogopa ni nini?? Acheni porojo zenu bana. Acha sisi tujilie vyetu. Nyie ndio mlie tu na ufukura wenu wa mawazo mpaka wa mali. Shweeeenziiii......Hahaha!

      Delete
  5. Laki tatu(300,000) haitoshi, na mimi nasimamia hilo hadi iongezwe hii kazi ni ngumu. watu wamekuja na wanasheria wasaidizi ili kuwasaidia na kuwashauri.
    2. Malipo ya dereva.
    3. Nyumba Dodoma zimejaa sana si chini ya elfu arbaini(40,000).
    4. Mafuta ya gari.
    5. Mtu umeacha kazi zako na familia unakaa dodoma kwa miezi miwili(2).
    6. Ada za shule.
    7. taarifa za watoto kuumwa. nk.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Peleka ujinga huko anayeona hiyo hela ndogo achape lapa hakuna aliyeshikiwa kisu ili akubali uteuzi. Mbona wako kimaslahi binafsi zaidi ya kilichowapeleka??? wasifikiri wao ni bora kuliko mamilion ya watanzania tulio nyuma yao.

      Delete
    2. 8. Nyama choma
      9. Totoooooos
      10. nk

      Delete
    3. 11.Shilole mauno
      12.Wema Sepetu
      13.Kidoti sijui nani
      14. Jacqueline Wolper
      15.JB
      16.Dah! Na kadhalika na kadhalika......

      Delete
    4. 17.diamond platinumz.....hahaha!

      Delete
  6. tena hii kazi ilitakiwa iwe ya kujitolea, sababu inatuhusu wote na ni kwa manufaa ya wote, kama ni posho ni yakujikimu tu, dereva analipwa kila siku posho yote hiyo ya nini, nae apate ya kujikimu, acheni upumbavu jamani, tulikubali hilo kirahisi kama hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ingekuwa angalau nzuri, lakini kila kukicha gharama za maisha zinapanda mshahara hautoshi, embu fikirieni usitetee utumbo hapa mdau wa 12:37 AM, au wewe ni mmojawapo wa hao?

    ReplyDelete
  7. Laki 300,000 mi naona ni hela kubwa sana akihuzuria tu mara mbili ana 600,000 embu acheni hizo ina maana wenyewe wana matumizi kutuzidi sisi huo mshahara ni wa miezi miwili kwangu ufisadi tu mshahara huo unawatosha wasiongezwe,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mi natamani hupunguzwe sio kuongwezwa

      Delete
    2. Utatamani sana huku umejianika hapo uvunguni mwa kitanda.....wewe ulie tu......

      Delete
    3. Yaani wewe ndio unazidi kuniliza jamani nani aanzishe jamani tuandamane Mimi mtoto wa mkulima sijui ata pa kuanzia zaidi naweza pambikiwa kesi nikaozea jela ooh Mungu tusaidie tunasngamia

      Delete
  8. hawa wanaleta nmzaha mana walimu wako wanalipwa laki tatu wanasomesha na wamepanga najuwa malaya wa bongo muvi nmeona ista wameanza safar za dom so wanataka hela wakafanye usodoma wao hawa

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndo zao hao wasenge,,walipwe 100,000.kuma nina zao.

      Delete
    2. Acha porojo zako wewe. Achana na mambo ya wivu. Huo wivu utakutoa pua. Kama na wewe vipi, si ufunge hiyo safari ya kwenda Dodoma????? Achana na ulimbukeni man. By the way Watanzania ni watu wajinga siku zote. Wamekuwa wakiendeshwa kama gari bovu. Kama namna gani vipi ingia mitaani uandamane ili ukipata kilichomtoa nyoka pangoni. Na sio kuishia kulalamika lalamika kwenye hizi Blog uchwara.

      Delete
  9. hamna haja ya kuingia mtaani kuandamana, hii ni tiketi mojawapo ya watanzania kuamka na kukubali mabadiliko, kuipiga chini ccm na kuweka wengine tuone watafanya nini, nao waki burunda wanapigwa chini, kama nchi zilizoendelea, ndiyo inavyotakiwa, lakini kwa ubozo wetu utakuta mtu bado anayasifia haya macccmmm, ooh lowasa ndiyo anatufaa kumbe ni walewale, AAMKENNI WATANZANIA mtabaki kulalamika tu wakti wenzenu wanakula tuu!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad