NANI WAMEIBA BILION SH 480 BILIONI HAZINA?

Tangu gazeti dada la The Citizen lichapishe mwishoni mwa wiki habari za upotevu wa Sh480 bilioni katika Wizara ya Fedha, Serikali imekaa kimya kama vile wizi huo ni tukio la kawaida, hivyo halihitaji maelezo ya kina wala ya haraka. Wananchi walitegemea kwamba Serikali ingetoa kauli haraka iwezekanavyo kuhusu mazingira ya upotevu huo na hatua inazochukua kuwawajibisha wahusika.

Tunasema kiasi hicho cha fedha zilizoibwa ni kikubwa kwa sababu ni zaidi ya bajeti ya mwaka kwa baadhi ya wizara, zikiwamo wizara kubwa kama ya Uchukuzi ambayo katika mwaka wa fedha wa 2013/14, kwa mfano ilitengewa Sh491 bilioni.

Tunaambiwa Sh480 bilioni zilizopotea katika Wizara ya Fedha zinaweza kujenga kilomita 375 za barabara kwa kiwango cha lami ikiwa ni urefu wa kutoka Dar es Salaam hadi Gairo, kilomita chache kutoka Dodoma. Tujiulize kiasi hicho cha fedha kingeweza kugharamia madawati, zahanati na madarasa mangapi kwa ajili ya wagonjwa na wanafunzi wetu.

Pamoja na ukimya wa Serikali kuhusu wizi huo, tumetiwa moyo na hatua ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), ambayo imemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kuchunguza upotevu huo wa kiasi hicho kikubwa cha fedha ambacho kilitumika pasipo maelezo katika kipindi cha miaka miwili ya fedha cha 2012/13 na 2013/14.

Wasiwasi wa kamati hiyo ni kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuwapo kwa mtandao mkubwa wa wizi wa fedha za Serikali katika Wizara ya Fedha. Jambo hilo limethibitishwa na vitendo vya wizi wa kimtandao ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya watumishi wake wakishirikiana na baadhi ya watendaji wa Tamisemi.

Ugumu uliopo hapa ni kwamba haijulikani kama fedha hizo zilizopotea zilitokana na kodi za wananchi au wafadhili ambao walichangia Sh842 bilioni katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/13. Ni sahihi kabisa kwa Kamati hiyo ya Bunge kushangazwa na kuendelea kuwapo kwa vitendo vya ufisadi serikalini, hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba ripoti za CAG kila mwaka zimekuwa zikifichua wizi wa mabilioni ya fedha katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. Kujirudia kwa vitendo hivyo kila mwaka ni ishara kwamba Serikali haina dhamira ya kupambana na vitendo hivyo.

Mwenendo huo wa Serikali unashangaza, hasa kutokana na ukweli kwamba mwaka 2013/14 ilikuwa na nakisi ya Sh847 bilioni katika bajeti yake. Hivyo, utekelezaji wa mipango yake ya maendeleo ingekwama kama siyo kukopa mabilioni ya fedha kutoka vyanzo vya nje na ndani ya nchi.

Matokeo yake ni kuzidi kuongeza mzigo wa Deni la Taifa ambalo limefikia Sh27 trilioni sasa, huku ikishindwa kukusanya kodi na kupanua wigo wa vyanzo vya kodi. Ndiyo maana iko hoi kifedha na karibu shughuli zake zote zimesimama, huku ikisuasua kulipa mishahara ya watumishi wake.

Pamoja na hali hiyo mbaya kifedha, bado vitendo vya wizi na ufisadi serikalini vinaendelea kama tunavyoshuhudia vikishamiri katika Wizara ya Fedha. Ni jukumu la Serikali kudhibiti ubadhirifu na ufisadi miongoni mwa watumishi wake, vinginevyo uchumi wetu utazidi kudidimia. Kwa kuanzia iwasake na kuwawajibisha wote walioiba Sh480 bilioni kutoka Hazina.

MCL.
Tags

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hivi hii nchi lika mtu mwizi eeh? aisee kuna nini jamani? hatuna viongozi au? inasikitisha na kukatisha tamaa!

    ReplyDelete
  2. VIONGOZI WAPO LAKINI MABOYA Yanaudhiiiii.

    ReplyDelete
  3. viongozi wenyewe wezi

    ReplyDelete
  4. sasa walimu wapya wataajiriwa kwel?

    ReplyDelete
  5. Viongozi wezi nchi wanaizidisha kuipandikiza madeni, pesa wanalipana nyingi na hakuna cha maana wanachoweka, mahospitali huduma mbovu. Wagonjwa wanalala mpaka kwenye koridoo huku wanafunzi nao wakiwa wanapata shida mashuleni kwa kukaa chini walimu wakibaki kulalama hakuna vitendea + mishahara midogo
    Lakini hela kama wao wako radhi kujinufaisha matumbo yao na familia zao wanasahau viapo walivyopiga na kushika vitabu vya dini wakati wakiiapa kuitumikia nchi yetu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani wanakera sana, na hapo watapiga kimya kimya msala utaisha hivi bila sisi kujua kilichoendelea. Sina imani na hii serikali aisee

      Delete
    2. Yaani wanakera sana, na hapo watapiga kimya kimya msala utaisha hivi bila sisi kujua kilichoendelea. Sina imani na hii serikali aisee

      Delete
  6. wamkabidhi magufuli wizara ya fedha haya matatizo yataisha

    ReplyDelete
  7. SASA INABIDI HII NCHI APATIKANE KIONGOZI IMARA YAANI RAISI IMARA,ASIYEKUWA MUOGA NA MPENDA KHAKI NA MAENDELEO YA NCHI YAKE NA ASIE KUWA MWIZI AU FISADI NDIO ITAAPAA, NA KUESHIMIKA DUNIANI, KWA SASA VIONGOZI WOTE WEZI, WIZI UMEZIDI MPAKA HATA WALE WA NGAZI YA CHINI WANALIFILISI TAIFA, KWA HELA ZA KODI YA WANANCHI WA KAWAIDA, HII NI MICHOSHO SANA, MAENDELEO YATATOKA WAPI SASA, KILA KITU HOVYO HOVYO

    ReplyDelete
  8. Unauliza nani kakwiba? Ina maana hujui uchaguzi wa ccm umewadia au umesahau EPA?

    ReplyDelete
  9. Afu vya katiba 300,000 kwa siku balaaaaaa

    ReplyDelete
  10. Yan kwakweli inasikitisha...mi nilishasema sitopiga kura nchii mpaka naenda kaburi sababu sioni faida yake kila kiongozi anaekuja ni yale yale tuu...Ukweli ni kwamba uo uongozi wanaougombania kila siku si kwajiri ya wananchi ni kwa faida zao na familia zao..Wanaishi ktk majumba ya mabilioni na magari wanayotembelea yanacost mpaka milioni mia mbili but mtanzania wa kawaida ana ata uhakika wa kula..That is not fair at all,ata wanancbi wakiongea hakuna anaesikilza wala kujari...Watanzania hamkeni na tupiganie haki kwa taifa lenye mafanikio na haki sawa kwa wote ata kwa faida ya watoto wetu baadae...inauma na inatia hasira mambo ya nchi hii na viongozi tuliwachagus kwa kula zetu wenyewe....but siku itafika tuu na mda si mrefu kama vita iwe vita na tukose wote.

    ReplyDelete
  11. Maccm yametudharau watz 100%. Hasa yakiiba na tukirudi mtaani tunayapa kura. Alieturoga wa tz yupo wapi tumwombe msamaha?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad