NIKKI WA PILI ATOA DARASA..SOMA ALICHOANDIKA HAPA

Hii makala imeandikwa na rapper Nikki wa II, ukishaisoma unaweza kusema chako chochote…
Anaanza kwa kuuliza >>>> thamani ya sanaa ni KIKIII? ? ?
Nakutana na wasaniii wachanga wengi, Kwenye show, mitandaoni, mtaani, studio na wengine wananipigia
Wengi huomba kolabo, ushauri, namba za simu za watu mbali mbali wa Kwenye industry hii
80% huomba ushauri wa kutoka, kolabo kwa dhana ya kuwasaidia kujulikana mapema, ama kusaidiwa kufikisha cd zao kwa watu Fulani Fulani.
Ni Ngumu sana kukutana na msanii mchanga akakuuliza namna ya kuboresha uwezo wake wa ku rap, kuimba ama kuwa mwandishi mzurii…kwa kifupi kuwa msanii bora
Msanii wa kwenda Kwenye concert anataka kwenda studio, msanii Ana nyimbo Moja na nusu Ana taka umtafutie Dili ya kurekodi….Mimi mpaka naenda studio nilikuwa nishaperfom matamasha mengi ya kushindanisha vipaji na nilikuwa na nyimbo mbili mpya kila wiki hazikuwa Kali ila ndio zilikuwa hatua za kujifunza ku rap na kuandika mashairi.
Wakati natafakari nini msingi wa Sanaa kuonekana rahisi namna hii na kua maarufu kuwa ndio inspiration kwa wasaniii wachanga na wala sio usaniii bora…nikawasha TV Mara nikaona nyimbo ya kiwango sawa kabisa na jamaa Mmoja ananiimbiaga nikienda saloon,
ikafuata nyingine na nyingine za aina hiyo
Theni ikaja interview mtangazaji anamuuliza msanii kwa nin mziki haulipi?? Nikacheka utalipaje wakati ni kitu rahisi sana nikitoka nje tu hapo nakipata, na hata mfanya kazi wako wa ndani anaimba sawa tu na unaye muona kwenye TV. hamna kitu kisicho na thamani kinacholipa….kitu ambacho sina uhakika ni Kama na yeye akiwa gheto kwake huwa Ana angalia play list anayoipangaga
Nibiashara Binafsi sio sahihi kumjaji MTu kwa anachofanya…lakini je haujiskii furaha kipindi ulikuta una fans 200 ukafanya wakawa 2000 loyal fans, hautajisikia furaha kizazi kinachofuata nao wakaja kalia kiti hicho. Biashara zetu ni binafsi lakini Jamii yetu sio na nijukumu letu la ujumla kuandaa mazingira bora kwa watoto na wadogo zetu.
Any way turudi Kwenye mada, natafakari watu Kama kendrik lamar, 50 cent, iliwachukuwa si chini ya miaka 10 kufika mainstream, kina keri hillson miaka 5 yakuwa backup singer, nikakumbuka mfuko wa joh makini uliokuwa umejaa mashaiiri tumeutundika pale sebleni kwetu.
Nikakumbuka kuwa gemü ya mziki wa kizazi kipya ina Kama miaka 15 ila ina zaidi ya wasanii 50 walio wika na kupotea wakati NAs, snoop, jay z wana karibia miaka 20 Kwenye gem on top. Radio Kama hot 97 na host Kama funk master flex toka miaka ya 90 mpaka Leo wanakimbiza New York, source magazine, alafu nawaza baadhi ya vipind vikubwa vilivyo poteza umaarufu hapa bongo, shows za TV ambazo nilikuwaga naziota kuwepo, sikumbuki Mara ya mwisho nimeaangalia lini
Shows za kujaza diamond jubilee, msanii mmoja ndio alikuwa na thamani ya show Moja ya club Leo ni wasanii 8.
Thamani…value…hujengwa na nini?………na hujengwa na nani?,…….na unawezaje kuilinda kulingana na mabadiliko ya muda na tamaduni za kinyakati?………..towa maoni yako uki ya elekeza kujibu maswali hayo…..
Unaweza niandika on my twitter account Nick mweusi @nikkwapili ama on Instagram @nikkwapili

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad