Wauza sembe wamegundua njia mpya ya kusafirisha sembe kupitia JNIA kwa kutumia kampuni zinazosafirisha vifurushi. Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba ameimbia Kamati ya Bunge ya Miundombinu iliyotembelea JNIA kuwa wiki iliyopita mamlaka husika uwanjani hapo zimekamata jumla ya vifurishi nane vilivyokuwa na dawa za kulevya.
Amesema jumla ya watuhumiwa nane wameshakamtwa kuhusiana na vifurishi hivyo na kuongeza kuwa wamiliki wa vifurushi hivyo bado hawajapatikana.
Amesema moja ya vifurishi hivyo kinapelekwa nchini Nambia huku kikionyesha kuwa kulikuwa na kitabu cha biology. Lakini kilipochunguzwa kilikutwa kikiwa na kiasi kikubwa cha heroin iliyokuwa imewekwa ndani ya kusasa za kitabu hicho.
Waziri ameongeza kuwa wauza unga pia wamekuwa wakitumia sandals na pakti za majani ya chai kusafirisha dawa za kulevya. Ameongeza kuwa vifurishi vingi vyenye dawa za kulevya vilikuwa vinaelekea nchi za Afrika Magharibi.
Habari kwa mujibu wa gazeti la Shanghai Daily la China.