SITTA:NAGOMBEA UENYEKITI WA BUNGE LA KATIBA KUTIMIZA NDOTO YA RAIS

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema atagombea uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu anaamini kuwa ana sifa za kutosha.

Hii ni mara ya kwanza kwa Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa kuweka wazi uamuzi wake huo. Mwingine anayetajwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.

Sifa za mtu anayepaswa kuongoza Bunge hilo ni kuwa na shahada ya sheria kutoka katika chuo kinachotambulika pia kuwa na uzoefu wa kuendesha mijadala kama ya Bunge.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema pamoja na propaganda chafu zinazoenezwa dhidi yake, hatakata tamaa na kwamba ataendelea na msimamo wake huo ili nchi ipate Katiba bora.

“Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeainisha sifa za mtu anayetakiwa kuwa mwenyekiti na mimi nina sifa na nina mipango mizuri ya kuwafanya Watanzania wapate Katiba bora kama ndoto ya Rais wetu (Jakaya Kikwete) ilivyo,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu njama za kumzuia asigombee nafasi hiyo, Sitta alisema “Haishangazi watu hao kutumia mbinu chafu… Hawana maadili, ndiyo maana wananihofia lakini sishtuki hata kidogo.”

Sitta ambaye pia ni mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alisema wabaya wake wamekuwa wakieneza maneno ya uongo kwamba ikiwa atakalia kiti hicho, atasimamia mpango wa Serikali tatu.

“Wanasema Sitta ataruhusu Serikali tatu, sasa nashangaa maana wajumbe ndiyo wenye mamlaka hayo… wanaeneza propaganda kuwa nina mkataba na wapinzani ndiyo maana wananiunga mkono. Wanasema mambo ya ovyo kabisa,” alisema.

Sitta alisema wapinzani kama walivyo wajumbe wengine kutoka CCM na makundi mengine, wanamuunga mkono kwa kuwa wanaamini akikalia kiti hicho ataendesha Bunge hilo kwa misingi ya uwazi na haki.

“Mimi sina mkataba na wapinzani ila wao kama watu wengine wananiunga mkono kwa sababu wanajua nitatenda haki, nina rekodi nzuri katika kuliendesha Bunge la Tisa wala hiyo haina mashaka,” alisisitiza Sitta.
Tags

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli kabisa huyu Mzee anafaa...

    ReplyDelete
  2. tatizo ccm wengi vilaza hapo wasom wachache wanawaendesha wengne 7bu hawakuelew
    upite baba unafaa kabisaa
    nmependa vigezo jaman mambo kuwekana mtt wa mjomba co

    ReplyDelete
  3. sasa nitashangaa kweli kama wakimpitisha babu wa rada na vijisenti na kumuacha mzee Sita, hapo ndiyo ntakapojua hii katiba itakuwa siyo ya maslahi ya watanzania wote, bali ni kwa maslahi ya MAFISADI!!

    ReplyDelete
  4. Unafaa babaa wakuacheee kidogoo!

    ReplyDelete
    Replies
    1. anafaa kuwa mwenyekiti wa bunge na wala sio rais

      Delete
  5. Sio kuwa na sifa tu bali anao uwezo mkubwa

    ReplyDelete
  6. Anafaa sana na nifundisho watendaji wengine kufanya kazi wanazopewa ili tuwakumbuke kama tunavyo mkumbuka mzee sita

    ReplyDelete
  7. in large extent SITA is quarified one with enough experience compare 2 others
    i'm appreciate u sita

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kiingereza jaman hiki!

      Delete
    2. Jamani lugha za watu hizoooo daaah ha ha haaa c bora utie swaga za lugha ya mamako tu? shule yenyewe ya kata halafu mnajamba jamba humu mtajua wapi kutema mayai jmn.

      Delete
  8. POOR ENGLISH AS IF YOU HAVE NEVER BEEN TO SCHOOL.

    ReplyDelete
  9. Sita is the best , god bless him

    ReplyDelete
  10. Sioni sababu ya katiba mpya, badilisheni vipengele tuendelee na maisha.

    ReplyDelete
  11. hata uraisi anafaa huyu mzee, kuliko wote wengine waliobaki ccm, pamoja binafsi siyo ccm.

    ReplyDelete
  12. Ila mwenyekiti wa muda Kificho ni noma angekuwa kiongozi mwingine hili bunge lingekwisha sambaratika ni yale yale ya Nyerere mgombea uras kung'angania ikulu kuna raha gani 'tunahitaji mijadala huru,wazi na inayotoa fursa sawa kwa wajumbe wote bila jazba wala mabavu hilo Kificho amepata asilimia 99.99999999999.........je SITTA ataweza yetu macho asijekuwa Mikhail Gorbachev aliyesambaratisha USSR mtoto akililia wembe mpe

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad