MBIO za urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimezidi kuibua mambo mapya, baada ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, kudai atachukua uamuzi mgumu kama chama chake kitateua mgombea urais asiye na sifa. Akizungumza katika kipindi cha Hapa na Pale, kinachorushwa na Radio Tumaini, mjini Dar es Salaam jana asubuhi, Sumaye alisema kama CCM itafanya mambo ya ajabu kwa kuteua mgombea asiyekubalika wala kuwa na sifa za kiongozi mwadilifu, atafungua ukurasa mpya.
“Nitachukua uamuzi mgumu kama CCM watateua mgombea ambaye hana sifa ya kuwaongoza Watanzania, nitachukua uamuzi mgumu, haiwezekani tukaongozwa na watu wanaotoa fedha nyingi kila kukicha.
“CCM wakifanya mambo ya ajabu kwa kuchukua mtu ambaye ametoa fedha, nitatafuta njia nyingine,” alisema.
Alisema hata siku moja hatakuwa na kinyongo kama atateuliwa mtu safi na mwenye moyo mweupe wa kusaidia Watanzania.
Alipoulizwa swali kama atagombea urais, alisema “Mimi sisemi kama nagombea, nakwambia muda ukifika nitasema tu, kwa wakati huu naomba tuendelee kutulia kwanza.
“Muda ukifika nitaamua nini cha kufanya, unajua unapotaka kuchukua uamuzi huu kuna mambo mazito ambayo unapaswa kuyatafakari kwa undani zaidi.
“Miongoni mwa mambo haya, ni kusaidia Watanzania kutoka walipo ili wapige hatua moja mbele zaidi, kuachana na tabia ya mtu mmoja kujitajirisha kupita kiasi,” alisema Sumaye.
Alisema kama Watanzania wakimhitaji ili awasadie, atakuwa tayari kufanya hivyo.
“Muda ukiwadia na Watanzania wakisema wananihitaji, basi nami nitakuwa tayari kuwasaidia…jukumu hili linahitaji mtu mwenye busara sana,” alisema Sumaye.
Alipoulizwa kuhusiana na hali ya CCM kwa sasa, alisema kuna tofauti kubwa katia ya CCM ya mwaka 1977 na ya sasa ambayo imekuwa ikikumbwa na matukio mengi.
Njia Mbadala, au Vipi?.....Hahaha!
ReplyDeleteWatakukolimba hao mafisadi wewe cheza nao, wanatoa watu kucha hao mashetani, ni bora uanze kimya kimya mzee.
ReplyDeletehahahahahahahaha mheshimiwa bwana eti wakiitaj uwasaidie upo tayari khaa so unataka ww ndo uwe rais au? Samahan lakin!! Vp vile vijishamba visemavyo ulijilimbikizia au ww ndo hitaki jitajirisha kupita kias tunakujua mheshimiwa coz ulisha kuwa waziri mkuu wetu!! Owk poa tukikuhtaj tutakuambia tunakuombea uzima tu!!
ReplyDeleteumenena Mhs Sumaye, kweli tunataka mtu ambaye anataka kuwasaidia watanzinia na si kujitajirisha yeye mwenyewe au kurudisha fedha za watu alizohonga kuingia ikulu, itakumbukwa hata Mwalimu Nyerere alisema, "ukimwona mtu anatumia pesa kutaka kwenda ikulu, mwogope kama ukoma" "sababu atazirudishaje kama kakopa, wakati ikulu hakuna biashara yeyote" jamani tumuenzi baba wa Taifa ili taifa hili lisijepotea tukaingia kwenye machafuko yasiyo faa, awe mtu kutoka ccm au Chadema, au chama chochote, lakini awe muadilifu tu, Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDelete