Zimebaki siku 13, kabla ya kufungwa rasmi kwa pazia la kupigia kura wasanii na kazi zao katika kinyanganyiro cha kuwania tuzo za filamu Afrika zijulikanazo kwa jina la ‘Africa Magic Viewers, Choice Awards, (AMVCA).
Katika mashindano hayo, swali linabaki kwa tamthilia ya Siri ya Mtungi kama itaweza kung’ara kwa kunyakua tuzo, pamoja wa walioshiriki wakiwania tuzo mbalimbali.
Mbali na tamthilia hiyo msanii Juma Rajabu (Cheche), aliyeigiza kwenye filamu hiyo anawania Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume akichuana na waigizaji wengine watatu kutoka nchi tofauti za Afrika.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice (Tanzania), inayoratibu mashindano hayo, Barbara Kambogi alisema kuwa kazi kubwa iliyopo mbele ni Wananchi kuhakikisha wanampigia kura mshiriki wa Tanzania katika tuzo hizo kubwa za filamu barani Afrika.
Kwa mujibu wa Kambogi wadau wa filamu na Watanzania kwa jumla cha wanaweza kupiga kura kadiri wawezavyo kabla ya kufungwa kwa hatua hiyo Machi tatu mwaka huu.
Multchoice imebainisha kuwa tuzo hizo zitatolewa Machi nane na kwamba zitaonyeshwa moja kwa moja kutoka Lagos, Nigeria na DSTV, pamoja na GOtv.
Kupiga kura
Kambogi alitaja namba za kumpigia kura Cheche akieleza kuwa wadau na Watanzania wanatakiwa kutuma neno 2a kwenda namba +2783142100415 au kwenye mtandao-> htt:// goo.gl / o72lu5. “Unaweza kumpigia kura mara nyingi zaidi kila baada ya saa moja kama Mwigizaji Bora wa kiume kwenye Tamthilia,” alisema Kambogi.
Tuzo zinazoshindaniwa
Multchoice ilizitaja tuzo zitakazoshindaniwa katika AMVCA kuwa ni 28, kukiwa na vipengele 26 kimoja kipya ambacho ni maalumu kwa ajili ya kutambua na kuheshimu watu waliotoa mchango muhimu kwa kujenga enzi mpya katika filamu barani Afrika kiitwacho Era.
Baadhi ya tuzo hizo ni Mwigizaji Bora wa Kike wa Drama, Mwigizaji Bora wa Kike kwenye Filamu za Vichekesho, Mwigizaji Bora wa Kusaidia katika Filamu za Drama, Mwigizaji Bora wa Kiume wa Filamu za Vichekesho, Filamu Fupi Bora, Mwandishi Bora wa Filamu za Vichekesho, Mtayarishaji Bora wa Filamu, Mhariri Bora wa Video na Filamu Bora ya Vichekesho.
Siri ya mtungi yapenya vipengele saba
Kwa mujibu wa Multchoice filamu ya Siri ya Mtungi, imefanikiwa kujitokeza katika kuwania tuzo kwenye vipengele saba vya mashindano hayo huku pia washiriki wake wakiwania tuzo.
Vipengele hivyo ni pamoja na; Tuzo ya Mwigizaji Bora kwenye Drama, ikiwakilishwa na Juma Rajabu, Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Filamu za Vichekesho, Filamu Bora iliyotumia lugha kiufasaha (Kiswahili) na Mwandaaji Bora Mwenye Kipaji (Kyle Quint).
Pia imejitokeza kuwania Tuzo ya Mhariri Bora wa Sauti aikiwakilishwa na Jordan Riber, Tuzo ya Mbunifu Bora wa Mavazi (Doreen Estanzia Noni) na Tuzo ya Mpambaji Bora ikiwakilishwa na Rehema Samo
TAMTHILIA YA SIRI YA MTUNGU KUNG'ARA TUZO ZA FILAMU AFRICA
0
February 22, 2014
Tags