TUNDU LISSU NAE AMSHUKIA LOWASSA

KADA wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi, Edward Lowassa anadaiwa kutumia kigezo cha udini kutaka kuungwa mkono kwenye harakati za kukimbilia Ikulu jambo linalohatarisha amani ya nchi.

Aidha Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kuweka hadharani majina ya watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya ambayo aliwahi kulitangazia Taifa kuwa anayo vinginevyo itakuwa ni vigumu kuondoa mashaka kuwa si mshirika wao.

Hayo yalisemwa juzi na Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Tundu Lissu na wakati akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Sombetini, Ally Bananga kwenye viwanja vya Ngusero.

Lissu alisema kuwa baada ya Lowassa kuona hana sifa za uongozi kutokana na kuwa si muadilifu wala safi kulingana na tuhuma za ufisadi zinazomwandama ameamua kukimbilia makanisani akiwashawishi viongozi wa dini wamuuunge mkono kwa kigezo cha kuwa ni Mkristo mwenzao.

“Kuna makada wengine wa CCM nao wanazunguka huko misikitini wakisema hii ni zamu yetu sisi Waislam hivyo anashawishi wamchague kwa kigezo cha Uislam tu .Hawa watu wanasahau dini si kigezo wala sifa ya uongozi tuwakataeni, sijui wanalipeleka wapi hili Taifa zaidi wanatutafutia machafuko hawatufai wote hawa,” alisema Lissu.

Akizungumzia muswada wa madiliko ya katiba, Lissu alisema kuwa katiba inasema kuwa nchi ni moja lakini kwa sasa kuna Maamiri Jeshi wawili ambao mmoja ni Mwenyekiti wa CCM, Kikwete na mwingine ni Makamu wake, Dk Mohamed Shein jambo alilosema kuwa ni hatari sana hasa ikitokea wakitofautiana na kupishana kauli ilihali wote wanamajeshi.
Tags

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tema cheche kamanda, hawa wanaomwaga pesa makanisani watatuchafulia nchi, siyo waadilifu kabisaaaa, kwanza hizo hela wamezitoa wapi?, Mwalimu Nyerere alisema " kama umenunuliwa utazirudishaje?' "maana ikulu hakuna biashara pale!!" Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Mzee wa richmond akichukua nchi watanzania tumekwisha.

    ReplyDelete
  3. Atauza nchi na watu wake huyu jamaa noma.

    ReplyDelete
  4. Bora auze kisha atugawie kila mtu mshiko wake achape mwendo aende anako jua maana wote wanaotaka madaraka mimi nawaona ni sawa wote, hakuna hata mmoja mwenye kutaka madaraka ili awasaidie wananchi ki ukweli kabisa, bali kwanza ni yeye pili walio muwezesha kuchukua madaraka kisha rafiki zake, ndugu na jamaa zake, baada ya hapo miaka mitano itakua imekwisha anaanza tena kutaka kuendelea na madaraka yake sasa mwananchi wa kawaida atafaidika na nini toka kwa viongozi? wote Lisu na Lowasa (CCM na gamba/Chadema M4C mafi matupu)

    ReplyDelete
  5. Tutamchagua mpende msipende! kwani msafi nani? wote wanapenda pochi tu hapa! tuhuma sio kosa! Naomba Lowasa aeendelee na harakati zake! Nidhahiri anatisha ndio mana watu wanaogopa!

    ReplyDelete
  6. Lowassa mnamtuhumu kwa udini....na nyinyi wa "ukabila" na "ngumi" jeeee???

    ReplyDelete
  7. LOASSA atachaguliwa namafisadi wenzake! siyo wtz wamaisha yachini wanaokanda mizwa naselikali yamafisadi

    ReplyDelete
  8. basi apeleke na misikitini kama analipenda hili taifa

    ReplyDelete
  9. Lowasa amekuwa akihudhuria sherehe na kuchangia pesa misikitini na makanisani, mzee mwache agombee ilitumchague kwani unadhani Richmond Mr President alikuwa haifaham!!! Wapinzani hamjajipanda ningumu sana kuwakabidhi nchi

    ReplyDelete
  10. Xaxa mnazani chadema mtachukua nchi acheni ujinga mtaishia ubunge tu na mtake msitake lowasa ndo prezidaa!

    ReplyDelete
  11. atakuwa prezedaa wako, lakini c wa watanzania, tumechoka kuibiwa!!

    ReplyDelete
  12. hao jamaaa hap wanaomshabikia lowasa ni Nora wasingezaliwa kabisaaaaaa

    ReplyDelete
  13. wana akili duni, hawajuai nini kuhusu leo au kesho, wao wapo wapo tu!!!! pumbaf

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad