TUNDU LISSU:WABUNGE WENGI BONGO HAWAJUI KINGEREZA

Mbunge wa Singida Mashariki, mnadhimu wa upinzani na mwanasheria mkuu wa CHADEMA mh. Tundu Lissu, amesema kuwa wabunge wengi wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hawajui lugha ya kiingereza kitendo kinachowafanya wakose ufanisi katika kazi zao za kibunge hususani mijadala mbalimbali bungeni na nje ya bunge. 

Mwanasheria huyo amekiita kitendo hicho kuwa ni janga la taifa ambapo ameshauri suala hilo litazamwe upya ili tuwe na wabunge wanaoweza kuwa tija kwa taifa.

Ikumbukwe kuwa wabunge wengi wa bunge hili wamekuwa wakituhumiwa kuwa na elimu za kidato cha nne (iv) au chini ya hapo na wengine kidato cha sita chenye matokeo mabaya.

source; cluods fm na star tv.

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ili iweje kwani mnaowawakilisha ni waingereza au ni wazawa mbona huo niukoloni tunataka lugha iwe ya kiswahili bungeni ili kila mwanchi ajue kinachojiri kwani mlivyokuja kwa wananchi kuomba kura hamkuzungumza kingereza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ni jinga.kuna mikataba imeandikwa kizungu wao ni ku sin

      Delete
  2. Sugu alieacha shule form two anaongoza

    ReplyDelete
  3. Umedata tundu kwani mama yako ma baba yako wanajus kingeleza ! Ulivyo kuja kuomba wananchi wa kupigie kura uliomba kwa kingeleza au kimyiramba au kinyaturu? Unapenda kuropoka kama nguchiro au ulishinda kwa ndumba unawafanya wenzako mambulula we ndio mbulula wa kwanza bungeni

    ReplyDelete
  4. Amekosea angeweka pia hawana Adabu hawajiheshimu Kama kipindi cha Baba Wa Taifa!!! tuchulie swala la Huyu viti maalum Wa Chadema JOYCE MUKYA!!! Yan Ni Uchafu kwa kweli bunge letu alina MVUTO kb kbs Ni Vihiyo na kayumba!!!

    ReplyDelete
  5. Tunapozaa watoto tuwapeni majina mazuri. Mana majina yana athari na mtu mwenyewe!
    Hebu fikiri unategemea nini mtu anapoitwa "TUNDU" Kawaida matundu mengi huwa na uchafu ndani yake,mfano Tundu la choo nk.

    ReplyDelete
  6. Yupo sahihi kwa 7babu mikataba mingi imeandikwa kwa kingereza au wajitahid kuibadil iwe ktk kiswahili itawasaidia kupitisha ki2 ambacho wanajifaham vzur

    ReplyDelete
  7. Mtu huwez kusign mkataba bila kuelewa na kwa ufahamu wangu ikitaka mkataba wako usainiwe lazima uwasilishe kwa lugha inayoeleweka kwa mlengwa . English ni muhmu ckatai ila kama kiongozi ni vyema kusupport lugha yako sio kuponda.

    ReplyDelete
  8. Ukitaka kujua kua ni kweli wabunge wetu hawajui kidhungu ni inapokuja issue ya kujieleza kwa kidhungu wanapoomba nafasi za uwakilishi bunge la Afrika Mashariki yaani ni majanga. Tundu umenena......

    ReplyDelete
  9. Ikumbukwe kuwa nchi yetu kwa kiasi kikubwa inaendeshwa kwa uhisani toka nje. Hivyo ni vyema kufahamu kizungu coz wao ndio wanaotupatia ufadhili ili kuepuka pia kuingia mikataba feki. Lugha ni muhimu ukatae au ukatae huo ndio ukweli

    ReplyDelete
  10. Ikumbukwe kuwa nchi yetu kwa kiasi kikubwa inaendeshwa kwa uhisani toka nje. Hivyo ni vyema kufahamu kizungu coz wao ndio wanaotupatia ufadhili ili kuepuka pia kuingia mikataba feki. Lugha ni muhimu ukatae au ukatae huo ndio ukweli

    ReplyDelete
  11. Kingereza ndoo kinaleta maendeleyo ?au ni miundo mpya ya serekali

    ReplyDelete
  12. Sasa ikiwa ww ni mbunge na hujui kiengereza ww ni mbunge wa aina? gani utawakilisha watu wako vipi? Ww waitwa muhishimiwa hata kiengereza hujui muhishimiwa aina gani ww???

    ReplyDelete
  13. Huyo lisu mbona alichemka mahakama kuu na kuomba kutumia kiswahili...tobo lisu na ye mwathirika ktk hilo

    ReplyDelete
  14. KUJUA LUGHA NI MUHIMU ILA POINT YANGU NI KWAMBA TUKIENZI KISWAHILI, LINAPOKUJA SWALA LA MIKATABA AU WARSHA, FURANI KUWE NA MKALIMANI AU MIKATABA ITAFSIRIWE KWA LUGHA YETU YA KISWHAILI. TUSIKUBALI KUENDESHWA, MBONA MCHINA ANAONGEA LUGHA YAKE, BADO NA MAJINA YAO NI LUGHA YAO, SISI TUNABEZA LUGHA YETU, MAJINA YENYEWE UTASIKIA MSWAHILI ANAITWA CLINTON, WEWE!

    ReplyDelete
  15. Hakuna mikataba inayosainiwa na wabunge, mikataba inasainiwa na Mawaziri au wataalum serikalini,wabunge kazi yao ni kujadili miswaada mbalimbali na kuipitisha na siku zote wanatakiwa waongee kiswahili. sio muhimu sana wajue kiingereza kwa ufasaha hicho hicho chakuombea maji kinatosha kwani sio wabunge tu bali waTZ wengi hawajui hiyo lugha yawezekana hata mwenyewe Tundu Lissu ni hivyo hivyo.
    Nawasilisha

    ReplyDelete
  16. yer yer yer english is a big problem in this Country, not only Bungen but also in academi issues. you know,Oh!!!!!!!!!!! nilikuwa najaribu nami kuandika kingereza maneno yakaniishia. Kiswahili Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad