Dar es Salaam. Baadhi ya makada wa CCM ambao wataitwa mbele ya Kamati ya Maadili na Usalama ya chama hicho, wanakabiliwa na shtaka la kutoa rushwa kwa lengo la kushawishi kukubaliwa kwao, Mwananchi limebaini.
Makada hao ni wale wanaodaiwa kuwa katika harakati za kuwania urais wa 2015, hatua ambayo imekigawa chama hicho katika makundi yasiyo rasmi ya yanayowaunga mkono wagombea hao.
Tovuti hili imedokezwa kuwa mgombea mmoja wa nafasi hiyo mwenye ushawishi mkubwa aligawa fedha Sh200,000 zilizoambatana na kadi za kuwatakia heri ya Krismasi na Mwaka Mpya 2014 idadi kubwa ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.
Kadhalika, habari kutoka ndani ya chama hicho zinasema baadhi ya wanaojiwinda kwa ajili ya uongozi, pia waligawa fedha kwa kigezo cha kuwashukuru wajumbe waliowachagua kuingia katika Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Hata hivyo, taarifa zaidi zinasema baadhi ya wajumbe waliopelekewa kadi hizo na fedha, walitoa taarifa kwa uongozi wa juu wa CCM pamoja na kuzirejesha, huku wakitaka wahusika wachukuliwe hatua.
“Kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa baadhi ya watu ndani ya chama kwamba ugawaji wa fedha nyingi kiasi hicho haupaswi kuvumiliwa hata kidogo, kwa hiyo ni dhahiri kwamba suala la chama kuchukua hatua halina mbadala, lazima hatua zichukuliwe,” alisema mmoja wa watendaji wa CCM makao makuu Dodoma na kuongeza:
“Waliorejesha hizo kadi na fedha hatukuwaruhusu waondoke hivihivi, bali tuliwataka waandike barua za malalamiko maana tunaweza kuwahitaji kwa ajili ya kutoa ushahidi mbele ya Kamati ya Maadili.”
Uchunguzi unaonyesha kuwa miongoni mwa waliorudisha fedha na kadi hizo ni wenyeviti wa wilaya na wajumbe wa NEC wa wilaya ambao ni sehemu ya walioshinikiza kuchukuliwa kwa hatua.
Akizungumzia suala hilo mwishoni mwa wiki iliyopita, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Philip Mangula alisema mwanachama yeyote wa chama hicho hatakiwi kutoa michango, misaada, zawadi kwa mtu au katika shughuli yoyote bila kupata ridhaa ya uongozi.
“Kufanya jambo hilo ni kwenda kinyume na kanuni za chama. Ndani ya chama kila ngazi ina Kamati ya Maadili, wote ambao wameanza kwenda kinyume na kanuni za chama watahojiwa katika kamati hizo,” alisema Mangula na kuongeza:
“Hairuhusiwi kuwasafirisha wajumbe, kuwapa malazi, chakula, vinywaji na ukifanya hivyo utakuwa unakwenda kinyume na utaratibu uliowekwa na Kamati ya Sheria, Katiba na Kampeni.”
Akihutubia kilele cha maadhimisho ya miaka 37 tangu kuzaliwa kwa chama hicho, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliziagiza Kamati za Maadili na Usalama, kuwachukulia hatua stahiki viongozi na wanachama wake wanaomwaga fedha ili kupata uongozi.
Kadhalika, Rais Kikwete alipozungumza na wajumbe wa Halmashauri ya CCM ya Mkoa wa Mbeya, alisema kuanza kwa kampeni kabla ya wakati wake ni moja ya mambo yanayosikitisha na kwamba suala hilo limekabidhiwa kwa Mangula kwa hatua zaidi za kinidhamu.
Source: Mwananchi
rais ni magufuli tu, nyie wengine hapo mnatafuta kick na hakuna ataewapa kura wezi wakubwa
ReplyDeleteLowassa my president.
ReplyDeletewe mtoto mbona husomeki
ReplyDeleteI hate lowasa,kwanza hizo pesa zake hazimtoshii?mbona watu wana tamaa hivi?kwanza ni ana ukabila na amesema yeye na ole medeye wanafukuza wachaga wote arusha wabak waarusha na wameru
ReplyDeleteStore za kupika,unamchukia ww na roho yako mbaya,lowassa shine n he will always shine wether u lyk y o not ndo presidaa jinyonge na kamasi kavp
DeleteLowadsa ni mbinafsiiiii,kutwa kujilimbikizia Mali na familia yake,mkewe anaroho ya kutu,alivyokuwa waziri mkuu ilikuwa balaaa akiwa rais je?Mungu tuepushe na huyu majinuni,amen
Deletefi saadi mkubwa.
ReplyDeletekuna watu wengine washajimilikisha hii nchi, au wana ndoto za ajabu, atakayeamua rais wetu ajae ni MUNGU tu, hata ukimwaga pesa kiasi gani haitasaidia, tena hizo pesa chafu ndiyo hazitasaidia kabissaaa, tutazipokea lakini hatukupigii kura!!
ReplyDeleteyoyote anayemwaga pesa nikwamba akipata urais nilazima arudishe pesa yake aliyogawa kwahiyo kueni macho pia mbadilike wa Tanzania mjue mbichi na mbivu mtanyonywa mpaka basi hivi hamchoki kuichagua Chukua Chako Mapema
ReplyDeleteLowQzq huyo
Deleteaaamkeniii watanzania, badilikeni si mnaona jinsi watu wanavyorithishana vyeo!!!
ReplyDeletewenye hekima tanzania ni wengi sana na wanauwezo wa kuiongoza nchi yetu vizuri but sisi wachaguaji ndio shida.wapi dr salim.tuangalie watu wenye level ya kimataifa..hawa wanaotajwa si wabaya je tuwachekeche tuone nani alifanya nn? na mimi napenda wenye nia wajitangaze mapema ili tuwajue.
ReplyDeleteLowassa I solute you Dady!!! Nakumbuka unabii Wa Tb Joshua!!! Uko juu Dady!! Wewe Ndo president wangu 2015!!! be blessing
ReplyDeleteLowasa kafuge ng'ombe tu urais wa nchi hii huwezi unasumbuka bila utasababisa uchaguzi ufanyike mara kwakujiuzulu kwako.
Deleteano wa 9:35AM Feb 12th, Lowassa atakuwa raisi wako wa Monduli 2015!! usiwe na wasiwasi!
ReplyDelete