USHOGA WA DK.CHENI HUU HAPA FILAMU YAKE YAZUIWA

Stori: Brighton Masalu
SIKU chache baada ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kuzuia filamu ya mkongwe katika sinema za Kibongo, Mahsein Awadh Said ‘Dk. Cheni’ ijulikanayo kwa jina la Nimekubali isiingie sokoni kwa madai kuwa imekiuka maadili ya Kitanzania, msanii huyo ameibuka na kueleza kinagaubaga, Risasi Jumamosi limenasa sauti yake.

Akizungumza na mwandishi wetu Jumatano ya wiki hii maeneo ya Mlimani City jijini Dar, msanii huyo alisema amesikitishwa na maamuzi ya bodi hiyo huku akidai kuwa lengo la filamu hiyo ni kukemea tabia za kishoga zinazoendelea kuibuka kwa vijana ikiwa ni pamoja na kupinga uhalali wa ndoa za jinsia moja

Katika maelezo hayo, DK. Cheni ambaye huzitendea haki filamu zake kwa kuvaa uhusika halisi, alisema moja ya kigezo ambacho bodi hiyo imekitumia kuzuia filamu hiyo ni pamoja na muonekano wa bango la filamu hiyo ambalo linamuonesha msanii huyo akiwa amevaa vazi la shera huku akiwa amejiremba kwa madai kuwa ni kuchochea ushoga jambo ambalo msanii huyo amelipinga vibaya.

“Eti ushoga wangu uko kwenye kujiremba sana, hakika wamenionea sana, lengo letu ni kuonya na kukemea vikali vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja, huwezi kuelimisha bila kuonesha madhara yake kwa vitendo kama ilivyo ndani ya filamu hiyo.

“Lakini, ndani ya filamu hiyo, kuna kipande ambacho kinaonesha kiongozi wa serikali akikemea kitendo hicho, sasa hapo ushoga wangu uko wapi? Kuvalia shera kwenye kava? Siyo sahihi,” alisema Dk. Cheni.
Mbali na kava hilo, msanii huyo alidai haoni kosa lolote katika filamu hiyo hivyo ataendelea kupigania haki yake na kwamba hayuko tayari kuonewa.

Jitihada za kumpa mkurugenzi wa bodi ya filamu,  Joyce Fissoo ili kuelezea juu ya sekeseke hilo, ziligonga mwamba hadi gazeti hili linaingia mtamboni lakini imedaiwa kuwa bodi hiyo itasimamia msimamo wake.
Source:Global Publishers

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ole wake yeyote ajifananishae na mwanamke kwa namna moja au nyingine au mwanamke ajifananishae na mwanaume, mafundisho ya din yameonya, kuigiza ni tayar umejifananisha tumia njia nyingine kukosoa si hiyo tuuu wengine watapenda utakavyo igiza ndio utakuwa mwanzo mbaya kwao

    ReplyDelete
  2. Umesema kweli mdau, kuelimisha sio kuvaa kama wahusika maana Kuna ndugu zetu wanapenda kuiga Kula kitu. Wasije kuiga na kuharibu jamii yetu. Mungu awape laana wanaofanya ushoga na usagaji

    ReplyDelete
  3. Freemason agenda.. What an evil act. You have to have gay tendencies to be dressing like one.. For once my government has done the right thing

    ReplyDelete
  4. Jamani mbona joti alikuwa akiuvaa uhalisia wa mwanamke na watu tunaangalia na kucheka tena yeye wala hakuwa akikemea, tubadilike jamani saivi ushoga tz umezidi hasa Dar vijana wadogo mpaka huruma. Haya mambo yakinyamaziwa yatazidi na mwisho kuonekana kawaida kama 1st world countries kwenye laana.

    ReplyDelete
  5. ww cheni jiangalie hiyo filam yako watafute mashoga wezio muangalie tushatoshwa na upuuzi wenu hamvunzi watu bali mnaharibu kuna mambo hayafai hata kuiigizawa kwa mila na desturi zetu hapa cheni umechemka

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad