VIONGOZI WAMETAFUNA FEDHA ZA BANK YA DUNIA, ASEMA DK SLAA

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amedai kuwa  baadhi ya viongozi wa Serikali wamegawana na kutafuna fedha zilitolewa na Benki ya Dunia, ili kugharimia miradi ya kuchimba visima 10  vya maji katika kila wilaya nchini.

Dk Slaa alitoa tuhuma hizo juzi jioni, alipokuwa akihutibia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo, mjini  Musoma.

Kiongozi huyo wa Chadema yuko katika Operesheni ya M4C Pamoja Daima.

Alisema kitendo hicho kinafanywa wakati Watanzania na hasa wanawake wakikabiliwa tatizo kubwa la kukosa huduma za maji kiasi cha kushinda hata kwa siku tatu bila kuoga.

“Ngoja niwaambie hivi sasa Serikali imekuwa ikiweka vikwazo vingi katika utekelezaji wa mradi wa maji kupitia Benki ya Dunia, ukweli ni kwamba fedha zote zilizotolewa zimeliwa sasa wameanza kuhaha wasijue cha kufanya,” alisema na kuongeza.

Wakati huohuo, Geofrey Nyang’oro na Raymond Kaminyonge wanaripoti kutoka Iringa kuwa viongozi wa Chadema Taifa wakiongozwa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wamekamatwa na polisi mkoani hapa na kushikiliwa kwa muda wakituhumiwa kuzidisha muda katika mikutano waliyoifanya katika Jimbo la Kalenga wilayani hapa juzi.

Mbowe alikuwa ameambatana na viongozi wa chama hicho juzi, walifanya mikutano mbalimbali mkoani hapa, ambapo katika Jimbo la Kalenga walifanya mikutano katika Vijiji vya Wassa,Nzihi, Kidamali na kisha kushindwa kufanya mkutano mmoja uliotakiwa kufanyika katika Kijiji cha Mgama kwa madai muda ulikuwa umekishwa.

Mwenyekiti huyo pamoja na viongozi wawili wa Chadema, Mbunge Peter Msigwa na Halima Mdee walikamatwa saa tatu asubuhi wakati mwenyekiti huyo alipokuwa akijiaandaa kuondoka mkoani humo kwenda mkoani Pwani kuendelea na mikutano ya Operesheni M4C pamoja Daima inayoendelea kwa sasa kote nchini. Hii ni mara ya pili kwa kiongozi huyo kukamatwa na kuhojiwa  ambapo mara ya kwanza ilikuwa Agosti 25 mwaka jana.
Source:Mwananchi

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama ushahidi unao waeleze wabunge wako waipeleke hoja bungeni.Hatutaki porojo za kwenye majukwaa, mkialikwa kunywa juice Ikulu hamuwaabii...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio kaka nimeipenda hiyo maana hawa kwa kuropoka wamezidi

      Delete
  2. Kuiba kwa nchi yetu imekuwa kitu cha kawaida wananvhi wamekikubali kwani polisi na judiciary wamepoteza proffessionalism ni kula rushwa tu,wwe ndio utapigwa vita.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli, na hata waliokuwa na nia na mapenzi mema na nchi inawalazimu either to join them au kukaa kimya.na the general mentality ya wananchi imebadilika ie, ukiwa fisadi, muuza unga, play boy and all other negative behaviors unaoneka kuwa bora zaidi.

      Delete
  3. Ww bwiga vip unapenda kuropoka WW na Mboe mbona ndio zenu kutafuna pesa za chama au ilo ulioni unaona ya wenzako? Tuliza makalio chini ufungue ata bar Uuze.

    ReplyDelete
  4. CHADEMA-Chagga Development Movement Association.Lazima 2chukue Nchi 2015.

    ReplyDelete
  5. Nasikia viongozi wa Chadema wamepandisha bei ya kununuliwa msimu ujao wa uchaguzi, sijui km akina Mkono wataweza ku afford?
    Siasa za bongo biashara ni kununuana tu...

    ReplyDelete
  6. Na mtaibiwa sana wadanganyika, na mnastahili kuibiwa pambafu kabisa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad