ZITTO AIBUKA NA DVD, INAYOWANANGA VIONGOZI WA CHADEMA

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
WAKATI Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, akijipanga kuanza ziara katika mikoa kadhaa nchini kujibu mapigo ya tuhuma dhidi yake zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye ziara ya Operesheni M4C Pamoja Daima, mbunge huyo ameibuka na DVD inayowananga viongozi wa CHADEMA.
Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa DVD hizo zitasambazwa kwenye mikoa na maeneo yote atakayofanya mikutano ya hadhara mbunge huyo, kama moja ya harakati na mikakati ya kujisafisha na tuhuma za usaliti zinazomkabili ndani ya chama.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa DVD hizo zinatengenezwa kwenye kampuni moja iliyopo eneo la Kariakoo ambayo imepewa tenda ya kuchapa nakala 10,000 na kampuni nyingine zaidi ya tatu, nazo zimepewa tenda ya kuchapa DVD hizo kwa idadi tofauti.
Hata hivyo jambo la kushangaza ni kwamba katika jaradio la DVD hizo kuna rangi ya njano, nyeupe, bluu nyepesi, bluu nzito pamoja na bendera ya taifa.
Rangi zilizotumika kwenye jaradio hilo hazina uhusiano na rangi za bendera ya CHADEMA wala chama chochote cha siasa nchini.
Mbali ya jaradio hilo kupambwa na rangi hizo, pia limepambwa na picha kadhaa za mikutano aliyopata kuifanya mwanasiasa huyo katika maeneo mbalimbali na nyakati tofauti nchini, huku picha kubwa ikimwonyesha Zitto akiwa amevalia suti huku akitabasamu.
Jaradio hilo pia limezungukwa na maandishi mbalimbali ambayo yanasomeka:
‘Uadilifu, Uzalendo na Uwajibikaji, ndio silaha yetu katika kutetea wanyonge na maskini wote wa Tanzania, tuungane kwa pamoja.’  ‘Tanzania Kwanza’
Maandishi mengine makubwa yanamtambulisha mbunge huyo ambayo  nayo yanasomeka:
‘Zitto Zuberi Kabwe, Mtetezi wa Wanyonge, Tumaini la Maskini wa Tanzania”
Jaradio hilo pia limeweka mawasiliano ya mbunge huyo ya simu ya mkononi, barua pepe, Facebook na Twitter.
Hakuna maelezo yanayoonyesha kama DVD hizo zinauzwa au zinatolewa bure.
Ndani ya DVD
DVD hizo ambazo nakala tunayo, zinaonyesha picha ya mikutano ya hadhara ya mbunge huyo aliyoifanya mkoani Kigoma mara baada ya Kamati Kuu (CC) ya CHADEMA kumvua nyadhifa zake na Mahakama Kuu kushikilia hatima ya uanachama wake baada ya kukabiliwa na tishio la kuvuliwa uanachama.

Kwa mujibu wa DVD hizo, katika moja ya mikutano ya mkoani Kigoma, Zitto anasikika akiuambia umati wa wafuasi wake waliofurika kumsikiliza akieleza chanzo cha mgogoro wake na CHADEMA ni msimamo wake wa kuhoji hesabu za fedha za vyama vya siasa, kikiwemo CHADEMA na kumuagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya uhakiki.

Kama ambavyo amepata kukaririwa mara kwa mara, Zitto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) anasema CHADEMA ilimtaka awajulishe kwanza kabla ya kumuagiza CAG kufanya ukaguzi ili kutoa fursa ya kuweka hesabu zao vizuri.

DVD hiyo pia inamuonyesha Zitto akisema sababu nyingine ya ugomvi wake na CHADEMA ni dhamira yake ya kutaka kuwania uenyekiti wa CHADEMA, nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Freeman Mbowe, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Huku akishangiliwa na maelfu ya wafuasi wake, baadhi wakiwa na mabango ya kumsifia, Zitto anasema hajawahi kupewa fedha na CCM kuisaliti CHADEMA na kuongeza kwamba atakuwa wa mwisho kutoka ndani ya chama hicho alichojiunga nacho akiwa na umri wa miaka 16.

Dk. Kitila Mkumbo naye yumo

DVD hiyo pia inamuonyesha aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu la CHADEMA, Dk. Kitila Mkumbo, akieleza sababu za yeye kutaka kujiuzulu kabla ya Kamati Kuu kuamua kumvua uanachama.

Dk. Kitila pia anaonekana  kwenye DVD hiyo akielezea waraka ulioandikwa na Samson Mwigamba ambao ulinaswa ukielezea mikakati ya kutaka kuung’oa uongozi wa Mbowe kwenye nafasi ya uenyekiti.

Kwa kifupi maelezo ya Dk. Kitila ni  yale aliyopata kuyatoa siku yeye na Zitto walipofanya mkutano na vyombo vya habari katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam wakitetea waraka huo kwamba haukuwa wa uasi kama ilivyotafsiriwa na CHADEMA.

Wiki iliyopita gazeti hili liliibua mkakati  unaodaiwa kufadhiliwa na  Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kutaka kumtumia Zitto kupambana na CHADEMA waziwazi.

Katika mkakati huo CCM inadaiwa kutaka kukodisha helikopta ya kumpeleka Zitto katika mikoa minne kwa gharama ya sh milioni 50, mara tu baada ya CHADEMA kuhitimisha Operesheni yao ya M4C Pamoja Daima.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vilivyo karibu na Zitto na CCM, yeye na chama hicho sasa wana adui mmoja – CHADEMA; na wameamua kujibu mapigo baada ya kuridhika kwamba kwa vyovyote Zitto amekwisha kupoteza uanachama wake katika CHADEMA.

Nia yao ni kumtumia Zitto kuleta mpasuko katika CHADEMA, na kufunika mjadala wa mgogoro wa CCM, kero za wananchi na mchakato wa Katiba mpya.

Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya CHADEMA – Naibu Katibu Mkuu Bara, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mjumbe wa Baraza Kuu na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni – anatarajia kutumia helikopta yenye uwezo wa kubeba watu wanne, ambayo inadaiwa kukodishwa na wapinzani wa CHADEMA.

Kwa mujibu wa habari hizo, lengo la ziara ya Zitto ni kujibu mapigo ya CHADEMA, hasa katika maeneo ambayo baadhi ya makada na viongozi wa chama hicho wamepita na kuzungumzia hatima yake kisiasa, hasa walipojibu maswali ya wananchi kuhusu sakata lake kuvuliwa uongozi kwa tuhuma za usaliti, na hatimaye Zitto kwenda mahakamani kuzuia chama kujadili uanachama wake.

Katika kesi ya msingi, Zitto aliyewahi kuwa maarufu akiwa kiongozi wa CHADEMA, anaomba arudishiwe nyadhifa zake zote, na apatiwe nakala za uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ili aweze kukata rufaa Baraza Kuu.
CHANZO NI TANZANIA DAIMA

Post a Comment

22 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu sisimizi bado yupo? anatafuta nini huyu? wewe siyo mtetezi wa wanyonge, wewe ni mbinafsi mwenye tamaa kubwa, wala usiwadanganye watanzania, watu kama nyie ndiyo mnavuruga harakati za ukombozi na kubakisha unyonyaji, haufai kaka, DVD zako hazitasaidia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ukuma kama azitasaidia inakuhusu nn?

      Delete
  2. Nyoo mpumbavu ww, nani sisimizi? Sisimiz ni mpumbavu mwenzio mbowe asokuwa na elimu hata kidogo , mtoto wa mitaan kapata bahati ya kumuoa kigogo wa chadema ndio maana yuko chadema au ww Mburulaaz hujui!? Au na ww umekimbia shule? Nenda kwenye blog ya wananchi, le mutuz usome CV ya boss wako mbowe, ...msx msonyooo!!!! Unashadidia vitu usivyovijuaaa, fara weeee

    ReplyDelete
  3. ZITO, SISI WENYEWE HATUMTAKI! NIMBINAFIS KAMA ALIKUWA NANIA NZURI NA CHADEMA MBONA JIMBONI KWAKE KUNA MADIWANI WATATU WACHAMA CHAKE? WOTE WADINI YAKE! HATAKAMA AJEDVD NALAPTOPU ATUGAWIE BULE HA2MWELEWI NAFIKI MKUBWA,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kumbe tatizo la Zitto ni dini yake? Afadhali mmeamua kua wa kweli cdm! Kweli nimeamini chadema ni chama cha ukanda na uchaga na parokiani.

      Delete
  4. Hongela zito! chama chako ccm wameahidi kukusaidia usafili wa helkoper kuzunguka nakusambaza dvd inchin, itakusaidia cdm wakuludishe kwenye chama!

    ReplyDelete
  5. Wote mafisadi wananchi wa hali yachini ndo wanaumia

    ReplyDelete
  6. WOTE NI WALE WALE WANYWA UJI WA MGONJWA HAKUNA CHA MBUNGE WA CUF, CCM WALA CHADEMA, WOTE WANATETEA MATUMBO YAO WAKATI WALALA HOI NA WALIPA KODI WANAKUFA NJAA. ACHANA NA SIASA, CHANGA LA MACHO. KESHO WATAELEWANA WANANCHI TUBAKI MALUMBANO.

    ReplyDelete
  7. Siasa shida Shida tupu ccm oyeeeee

    ReplyDelete
  8. zito sismizi tu, pamoja na elimu yake lakini imeshindwa kumsaidia kufikiri, amebaki kufikiria tumbo lake tu, hana lolote, aende kwao kigoma na hizo dvd zake ndiyo zitamsaidia, aliyekuambia kiongozi lazima awe na elimu ya juu ninani ndiyo aweze kuongoza, tuna maprofesa wangapi viongozi lakini hamna kitu, ebu fikiria kwanza kabla ya kuongea we mtoto wa ccm ambaye utabaki soma shule za kata tu, halafu uliowachagua wanakuibieni na kupeleka watoto wao ulaya, zito zito, mpe mambo basi siyo unashabikia upepo ule!!

    ReplyDelete
  9. Wewe zitto yupo juu ndo mana mababa mzima yanahaha yanajua atawaharibia zitto tuko nyuma yako we ndo mwenyekiti wa chadema watake wasitake atoki mtu mpaka kieleweke hapa

    ReplyDelete
    Replies
    1. uenyekiti atapata lakini sio wa cdm labda wa chama cha wasio na adabu

      Delete
  10. Zito pambana mpaka kieleweke hatutaki chama ambacho kinadidimiza demokrasia.

    ReplyDelete
  11. Unayesema walalahoi kuma kuma kweli je na mbowee ni mlala hoi mwenzanko kuma ww? Kubali wote wasenge cdm zito ongea ukweli baba tupo nyuma yako

    ReplyDelete
  12. Chadema chama cha wachaga na tumeishawastukia wakitaka mabadiliko wabadili halo viongozi wao wa juu.

    ReplyDelete
  13. Zito yupo juu kigoma, mwambieni alete usenge wake nyanda za juu namaanisha mbeya, iringa aone mziki wake, kama ajarudi na pumbu moja, manyoko zake kabisa.

    ReplyDelete
  14. nyie wote mnayamsifia huyu kifaranga zito ni ccm, tunaomba msiingilie mambo ya Chadema, nendeni huko kwenu kuna matatizo sana ya kifisadi, kayatatueni kwanza ndiyo muingilie wengine, mbwa nyie.

    ReplyDelete
  15. Nyie wasenge,kwani Kilimanjaro hakuna wabunge Wa ccm,mbona mlema wa TLP alishinda na sio CDM,acheni usenge,ukweli utajulikana Tu,kwa hiyo mlitaka wakigoma wasichague watu wanaowapenda?mikundu nyie,mfyuuuuuuuuuuuuu.

    ReplyDelete
  16. Zitto karikoroga kulinjwa anaona tabu Heee. Kwishineyeeeeee. Umetokota hasa nenda hk ccm kama utapata urais burula weee

    ReplyDelete
  17. zito endelea na harakati zako ww ni mpiganaji hawa wafuasi wengine wa Chadema hawana maslahi na nchi hii wana siasa zile za ndio mzee ninachoamini hawa viongozi wa chadema wanakuogopa wanajua ukiwa mwenyekiti ww viongozi waongo watakua hawana nguvu chadema hawa akina dr slaa wanahubiri siasa za kinafiki si zakimaendeleo wao kila siku mipasho hawana jipya itokee sitofahamu wanamisimamo ambayo hata kueleweka haieleweki ujuwajitu umewazidi

    ReplyDelete
  18. chadema mwanzo ilianza vizuri jinsi wanyeviti walivyokuwa na uchaguzi.lakuni sasa mbowe naona asali imemnogea.amwachie tu zitto na yeye tuine uongozi wake na ndio democrasia

    ReplyDelete
  19. zito hawezi kuwa kiongozi wa Chadema, hana maadili hayo, alikataaa posho bungeni akawa anachukua rushwa za usimamizi wa hesabu za serikali, mbururala tu yule, kwanza fala yule ni ccm, atakuwaje kiongozi wa Chadema, aende huko ccm kulipo mpa umaarufu, maanake yule kijana amesahau Chadema ndiyo iliyomuweka pale alipo sasa hivi, "kweli shukurani ya punda ni mateke!!!" pumbaf!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad