BUNGE LA KATIBA NA WANANCHI WAKO NJIA PANDA

Kwa neno moja unaweza kusema kwamba wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na wananchi kwa ujumla wako “njiapanda”.

Hii ni baada ya hotuba ya ufunguzi wa Bunge hilo iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete kuibua mambo mazito ambayo kimsingi yanatofautiana na mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.

Huku wananchi wakijiuliza nini hatima ya Bunge hilo baada ya hotuba hiyo, baadhi ya wajumbe ambao wiki hii ndiyo wanaanza kujadili rasimu hiyo, watakuwa katika wakati mgumu wa kuamua wafuate maoni ya nani, kati ya viongozi hao wawili.

Ingawa Rais Kikwete amesema mara kadhaa kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba ndiyo waamuzi. Mambo mengi aliyoibua yanaonyesha kutokubaliana kwake na baadhi ya maoni ya wananchi yaliyomo katika rasimu, ambayo Jaji Warioba amewahi kusema kuwa yanatakiwa kuheshimiwa.

Wakizungumzia tofauti hizo, mjumbe wa Bunge la Katiba, Ezekiah Oluoch alisema kauli za Rais Kikwete na Jaji Warioba zimezidi kuwagawa wajumbe wa Bunge hilo kwa maelezo kuwa tangu awali wajumbe hao walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili; ya wanaotaka muundo wa Muungano uwe wa serikali tatu na wale wanaotaka serikali mbili.

Alisema kama suala la muundo wa Serikali likishindikana kupatiwa mwafaka ni vyema likarudishwa kwa wananchi ili wapige kura ya maoni kuchagua aina wanayoitaka, kisha suala hilo lirejeshwe tena katika Bunge la Katiba kwa ajili ya kuboreshwa.

“Rais alipoanza kuzungumza alikuwa kama mkuu wa nchi lakini mwisho wa hotuba yake aligeuka kuwa mwenyekiti wa CCM. Kifupi alichokizungumza kimekwenda tofauti na wadhifa wake,” alisema.

Naye Deo Filikunjombe alisema: “Nadhani kwa hotuba hizi mbili, kazi ya wajumbe wa Bunge la Katiba itakuwa rahisi. Maana sasa wameshajua uzuri na ubaya wa serikali tatu na mbili.

“Hata kama kutakuwa na tofauti, wananchi ndiyo watakuwa wa mwisho kuamua kama Katiba hii ipite au isipite. Tunachotakiwa wajumbe ni kuwa makini na uamuzi wetu.”

Naye Yusuf Manyanga alisema: “Bunge la Katiba limejaa watu wenye busara. Sidhani kama tutashindwa kuelewana maana hata katika biashara ya utumbo inzi ni wengi lakini utumbo unauzika.”

Katika hotuba yake aliyoitoa Ijumaa iliyopita Rais Kikwete aligusia mambo saba ya msingi yaliyomo katika rasimu ya Katiba na kutaka yatazamwe kwa kina, huku akibainisha kuwa mengine hayawezekani kutekelezeka.
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mtajibeba sisi tunataka katiba

    ReplyDelete
  2. Utajibeba na wewe,unajitoa wakati wanakula kodi yako,yababa ako,ya girfrnd/boyfrnd wako,dada yako na yabibi yako kijijini.na bado yakiwashinda wataongeza siku afu sikiliza budget ijayo kila kitu juu anzia usafiri,matibabu na huduma muhimu ikiwemo bidhaa sasa sijui wao wanajibeba vipi hapo.... ?fikiria kwa upeo mdogo sana utagundua ni jinsi gani siasa inagusa kila kitu kwenye maisha yako sio kusema mtajibeba sema nitajibeba

    ReplyDelete
    Replies
    1. We msenge nn? Katunge yako, fyuuuuu

      Delete
    2. We ndo msenge tena wa mombasa.kushadadia mambo unadandia gari kwa mbele,kadandie mbolo za waarabu mombasa,kaongea sense unajamba tu hapo mkundu ushafirwa naona unanyege na leo njoo geto nikupe ukuni ukamsimulie na dada yako na yeye aje nimpe

      Delete
  3. Nyie kuleni tu huko mjengoni, wansiasa wote sio wa kweli,

    ReplyDelete
  4. nyie hapo juu mnalaana au!!!!nyooo

    ReplyDelete
  5. Mie naishi kivyangu bila ya katiba sababu hainisaidii na chochote

    ReplyDelete
    Replies
    1. haukusaidii chochote ungekuwa huru kuishi si ungekuwa mkimbizi saizi?

      Delete
  6. JK hajui kuwa wananchi wanataka kuwe na kikomo cha ubunge kwa sababu wamegundua kuwa ni njia ya kutafuta utajiri sio kuwatetea wananchi na sasa imekuwa viongozi wanafanya mbio za vijiti nchi yetu wanapokezana kifamilia.Wananchi matatizo yao yapo pale pale,matibabu shida nyie mnakewnda India na Marekani,shule za watu wa kawaida mbovu,rushwa kila mahali nk

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad