Stori: Joseph Shaluwa na Erick Evarist
MASKINI! Stori zilizozagaa mitaani kuhusu mali za aliyekuwa mkali wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba zinasema kuwa, zimeuzwa na kampuni aliyoiacha, Kanumba The Great Film imefilisika, Ijumaa Wikienda linakupa ripoti iliyoshiba.
Habari zinadai kuwa baada ya kifo cha Kanumba Aprili 7, 2012, mali alizoziacha zinafujwa, hakuna utaratibu mzuri wa kusimamia mamb
na kwamba, uzalishaji wa sinema katika kampuni yake ni mdogo tofauti na enzi za uhai wake.
Chanzo chetu cha habari ambacho ni mmoja wa wasanii wa filamu Bongo aliye na ukaribu na familia hiyo, alisema ni kweli kuna tatizo la usimamizi na uendelezaji wa mali za marehemu lakini akasema ni jambo la kawaida kwa sababu marehemu ameondoka na mbinu zake.
“Kila mtu ana nyota yake kaka, asikudanganye mtu, lakini pia kila mmoja ana namna anavyojua kuendesha biashara zake, sasa Kanumba alikuwa na mikakati yake, hawa walioachiwa nao wana mikakati yao. Mfano, hawataweza kutoa sinema nyingi kwa sababu soko la waliobaki si kubwa kama ilivyokuwa kwa Kanumba.
“Angalia hata ushindani... hivi kweli Seth (Bosco, ‘mdogo wa Kanumba’) anaweza kupambana na magwiji kama JB (Jacob Steven) au Ray (Vincent Kigosi) sokoni? Watu waache lawama,” alisema msanii huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina.
MDOGO WAKE ABANWA
Waandishi wa habari hizi walifunga safari hadi Sinza–Mori, Dar zilipo Ofisi za Kanumba The Great Film na kuzungumza na mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco ambaye alisisitiza kampuni ya marehemu kaka yake haijafilisika kama maneno yalivyozagaa mitaani.
“Hao wanaosema eti kampuni ya Kanumba imefilisika wanakurupuka tu, hawana cha kufanya lakini nataka kuwahakikishia kuwa, hatujayumba ila tunakabiliwa na changamoto za kawaida tu kama inavyokuwa kwa kampuni nyingine,” alisema Seth.
KUHUSU LEXUS
WIKIENDA:Tulisikia gari alilokuwa akitembelea marehemu Kanumba, Toyota Lexus limeuzwa. Ni kwa nini na liliuzwa kwa bei gani?
SETH: Kama familia tuliamua kuliuza kwa sababu ya gharama za uendeshaji. Lile gari linatumia mafuta mengi sana na matengenezo yake ni makubwa na hatukuona sababu za kuingia kwenye gharama kubwa za namna hiyo.
Kuhusu bei lililouziwa, kwa kweli sifahamu. Kama unavyojua baada ya mtu kufariki dunia, huwa kuna msimamizi wa mirathi, yeye ndiye anayejua kuhusu hilo.
UZALISHAJI
WIKIENDA: Kipindi cha Kanumba, alikuwa akitoa sinema nyingi sana, nadhani kama sikosei ilikuwa moja kila baada ya miezi miwili wakati mwingine kila mwezi sinema moja lakini baada ya yeye kuondoka, uzalishaji hakuna tena.
Mfano mpaka sasa kuna sinema mbili tu sokoni tangu alipokufa ambapo inakaribia miaka miwili sasa. Tatizo ni nini?
SETH: Ni kweli, lakini si kwa sababu ya tatizo la fedha – ni uhitaji. Unajua kuna changamoto nyingi sana kwenye tasnia yetu. Ni kweli mpaka sasa tumetoa sinema mbili; Malaika na Wonderful Girl ambayo tayari iko kwa msambazaji lakini bado haijaingia mitaani.
Mwaka huu ndiyo tumeanza, kuna kazi moja tunaifanya sasa hivi, ingawa si ya kwetu, sisi tunasimamia kwenye production (kuizalisha) lakini mipango ya mwaka huu ni mikubwa, mapema sana, tutaanza kurekodi kazi yetu nyingine, kwa sasa siwezi kusema jina lake ila inakuja
OFISI VIPI?
WIKIENDA: Kwa nini muda mwingi ofisi inakuwa imefungwa tofauti na ilivyokuwa kwa marehemu Kanumba?
SETH: Kaka hii ni kampuni, sisi tunafanya biashara na mteja wangu hahitaji kunifuata. Mimi mteja wangu ni Steps, ambaye namtayarishia kazi kisha nampelekea.
Milango inaweza kuwa imefungwa lakini kazi za ‘editing’ zikawa zinaendelea ndani au tukafunga ofisi lakini tukawa location tunarekodi, kuna tatizo gani hapo?
WIKIENDA: Lakini marehemu alikuwa anauza hadi filamu hapa ofisini? Imekuwaje siku hizi?
SETH: Hatujawahi kuuza sinema hapa ofisini ila tulikuwa tunaweka kama mfano wa kazi zilizowahi kufanywa na marehemu – si za watu wala kampuni nyingine. Lengo lilikuwa kuwapa watu wanaotutembelea (bure), si kwa kuwauzia.
Bila shaka maelezo hayo ya Seth yatakuwa yamejibu maneno yote yanayosemwa mitaani.
Credits:Global Publishers
KUHUSU KUTEKETEA KWA MALI ZA KANUMBA HII NI STORI KAMILI
11
March 03, 2014
Tags
mtu akifa anakufa na vitu vyake vyote
ReplyDeletemwenye maono akifa basi kila kitu kinakufa. kwasababu maono ya Kanumba hakuna mwingine aliyenayo kwahiyo mtu hawezi akaendelea unless msanii yuko majuu alafu foundation yake indeleze. ila bongo hakuna hiyo kitu.
ReplyDeletedah sad story
ReplyDeleteKanumba tutakukumbuka daima
ReplyDeleteR.I.P kanumba....
ReplyDeleteNitaendelea kukupenda daima kanumba pumzika kwa aman
ReplyDeleteI loved this guy...my your soul rest in peace Kanumba
ReplyDeleterest in peace bro.
ReplyDeletekanumba kila nikikumbuka kuwa sintaonatena filamu zako mpya katika ulimwengu huu machozi yananitoka. nitakupenda daima upumzike kwa amani
ReplyDeleteLulu lulu lulu duuuuu
ReplyDeleteRIP KANUMBA
ReplyDelete