KUNDI la wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba linalowashirikisha wanasiasa wa vyama vya upinzani, maarufu kama Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), limekuwa mwiba mkali kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kinapanga mikakati kulisambaratisha.
Ukawa inayoongozwa na vinara wa vyama vikubwa vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi pamoja na vingine vidogo visivyokuwa na wabunge, inaonekana kuwa mwiba kwa Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kwa kudhibiti uvunjwaji wa kanuni ili kuibeba CCM.
Awali CCM ililipuuza kundi hilo na kulibeza, lakini baada ya kuona nguvu yake wakati wa kumtetea Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba apewe muda wa kutosha, hofu ilitanda.
Ukawa tumieni huwezo wenu wote wa kufikir na nguvu zenu zote mpaka kieleweke, nyie ccm ni mbwa koko wa kijani
ReplyDelete