KUNUKA KIKWAPA NA WEUSI KATIKATI YA MAPAJA YANGU VINANINYIMA RAHA

Naomba niombe msaada kwenu wadau,nina matatizo sijui niseme shida  ambazo kiukweli zinanikosesha raha,nimekua nikihangaika sana kutafuta dawa ya kumaliza harufu ya kikwapa,yaani ni kwamba nimejaribu kila aina ya deodorant,na perfumes za kila aina lakini harufu haiishi,itokee bahati mbaya nisahau kupata Deodorant jamani sio siri najisikia hata mimi mwenyewe jinsi ninavyotoa harufu kali,zaidi ya harufu makwapa yangu ni meusi,ajabu,niliambiwa deodorant za Forever Living zinasaidia kumaliza weusi makwapani lakini wapi sioni tofauti,nawaombeni mnisaidie jamani nakosa raha,kifupi harufu utadhani lile jasho wanalonuka wanaume,wakati mwingine nafikia hata kujinyanyapaa mwenyewe,kwa kutokwenda kwenye shuhuli,nahisi wenzangu wananisema,shida inakuja muda wa kazi,kwani siwezi kukwepa kwenda ofisini,kiukweli it is so embarrassing.

La pili,huohuo weusi,katikati ya mapaja nako hakufai,yaani nikipanua miguu utadhani nimesilibwa lami hapo kati,nimejaribu kutumia mikorogo,haikusaidia,cream zile za hospitali za ngozi,pia nimejaribu,angalau kidogo utaona natakata,tatizo lake baada ya muda yanatoka mapele kama vijipu nashindwa hata kutembea shauri ya friction,nilipata ushauri wa kuvaa skin tight ili kuepusha friction,lakini lile la weusi lipo palepale,wenzangu nawaomba,kama kuna mtu alishawahi pata  matatizo kama yangu,naomba msaada tutani,jamani siyo siri,pamoja na kutaka nionekane maridadi,lakini pia wakati wa majambos si mwajua kuna muda wa mahabuba kwenda down,sasa inapofikia hapo,dah,najisikia aibu kwa maana naona kama vile najichoresha,na jamaa yangu huwa hakubali bila kunipagawisha kwa njia hiyo,sasa nipo na wakati mgumu
.
Huwa napendelea sana kusoma story kila wikiendi ila wamama/wadada saa nyingine mna maneno makali ambayo yanatukatisha tamaa kuomba ushauri humu,nawaombeni jamani,wengine hatuna pa kusemea wala wa kutupa ushauri wa kweli,tusaidiane jamani,Samahani kama nimewakwaza

Post a Comment

21 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Chukua sufuria ya ugal baada ya kupika weka Maji hadi ukoko ulainike baada ya apo tumia Yale Maji kuosha sehemu zote zinazotoa harufu fanya hvyo kama wiki moja then toa feedback sawa!

    ReplyDelete
  2. Tumia ndimu kusugua hilo kwapa pia deodorant nivea kavu,mapajani vaa skin tite

    ReplyDelete
  3. Nawa kwa maji uliyooshea mchele

    ReplyDelete
  4. Pole mwaya...hili janga huwapata sana watu wanene mapaja husuguana hata ukivaa skin tight. Hebu jaribu dawa inaitwa DARK SPORT labda itasaidia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli kama ni mnene jaribu kupunguza uzito kwa kunywa maji ya moto kila asubuhi na kupunguza kula hapo utaweza kuondoa mabaka meusi kwani yanasababishwa na unene

      Delete
  5. DHDGDHGUGGHGHGGHDGF

    ReplyDelete
  6. Tumia ndimu kusugulia kwapa then paka miski itasaidia kupoteza harufu, pia jaribu kuoga na sabuni ya Dettol cool. Ama kuhusu mapaja dawa yake chukua mafuta ya nazi uchanganye na tangawizi grade 1 ya unga usiifanye nzito itakubabua na kukunyofoa, jipake wakati wa kulala, ni moto dadangu lakini in shaa allah utaona mabadiliko.

    ReplyDelete
  7. Pole mdada mim dawa nijuazo za kwapa wadau wengine washataja ni maji ya ukoko wa ugali au maji ya mchele na limao wengi husema ni dawa jarbu na utupe matokeo

    ReplyDelete
  8. PAKA JIVU KWENYE PAJA KILA SIKU USIKU ITAONDOA LAMI YOTE ULIYOKUNAYO.

    ReplyDelete
    Replies
    1. sorry ndugu yangu, hilo jivu unapakaje?? unaeka maji au vp?? nna hilo tatizo sijui litatuliwaje, naba msaada, asante

      Delete
  9. Hakikisha kwapa wakati wote linakuwa safi. Huachi kinyweleo kinachomoza, hakikisha unakwangua kila baada siku mbili.

    ReplyDelete
  10. Chukua ndimu zichemshe kidogo then jisigulie nazo kwapa kila siku mara mbili. Alafu tumia scrub either ya cucumber, peach au yoyote ulo nayo. Sugua kwapa yatoa weusi na mapaja pia sugua yatoa na vipele pia. Ukioga uwe una kitu cha kujisugulia either dodoki taulo kkidogo. nywele za kwapa ka unazo nyoa nazo pia husababisha harufu. Alafu kama ni mlaji wa sea foods sana punguza maana pia zachangia. Kuhusu deodorant usitumie za spray tumia roll on nivea. Na ukipaka perfume usipulize ikiwa umevaa nguo kwa kwapa pija nguo ka huja vaa then vaa..au ukiwa ushavaa usipulizie direct kwa kwapa maana unaziba pose kisha ndio later harufu. Nihayo tu. Ukifuata utasaidika trust me

    ReplyDelete
  11. Pole sana na ikiwa unatatizo husitumie tena kemical utapata matatizo zaid kwani sehem kama hizo kuna kinga na unapotumia hizo unaua na kuruhusu uvamiz kwa iyo mi naweza kukusaidia kwa kukupa dawa utakayo tumia kwa siku 7 na utapona na kuwa na aman. feilymusa2@gmail.com.

    ReplyDelete
  12. Pole sana we dada, ila kwenye maelezo yako inonesha hujaonana na daktar zaidi ya kununua dawa na kutumia bila ushaur wa daktar, jaribu kuonana na daktar yoyote bingwa wa magonjwa kama hayo na ikishindikana hapo, jua ni pepo ndo lina kutesa , itakulazimu uende kwa church ukaombewe

    ReplyDelete
  13. Pole sana mdada cha kukushauri nenda kwa dr wa ngozi umweleze tatizo , dawa zipo na itakwisha harufu yote . Kuna sindano ambazo huwa zinapigwa mara moja kwa mwaka , kuna vidonge pia na kuna dawa ingine ni kama deodorant inaitwa Aluminium hii sana sana unaipata penye maduka ya madawa mungu atakusaidia utapona dada angu na pole sana na tatizo hilo.

    ReplyDelete
  14. Daaah leo mmenikosha hakuna aliyetukana tukienda hivi tutafika, pole sana dada zingatia ushauri uliopewa.

    ReplyDelete
  15. Aliiomba asitukanwe kwan wengi hawatoi shida seriouse ndo maana wanaambulia matusi na michambo. Na inaonekana wanaotukana n wanaume maana hapo wanawake ndo wamejibu

    ReplyDelete
  16. Pole sana, wewe hunuki kwapa ila unanuka mwili mzima, na nilimsikia doctor akieleza kwamba hiyo mara nyingi humpata mtu ambaye anakuwa na matatizo ya haja kubwa kama na wewe unatatizo la kukaa zaidi ya siku tatu au zaidi bila kupata haja kubwa huenda ikawa ndio sababu sasa pamoja na dawa zote ulizopewa hapo juu na ndizo ninazozifahamu hata mimi, maana nilikuwa na Hgirl wangu naye alisaidiwa na dawa hizo hapo juu hasa ndimu kusugua jaribu kujitahidi angalau upate choo kikubwa japo mara mbili kwa siku ikishindikana hata mara moja si mbaya pia muone doctor kwa ushauri zaidi kuhusu hilo nililokueleza. mapaja meusi paka AMOL G cream inasaidia sana hata kwa kuwashwa kuleeee kwa bibi na kingineko pia usiache kuvaa skin tight. nakusikitikia sana hasa ukiwa Dar na joto likizidi najua unawapa shida off.mates wako utapona.

    ReplyDelete
  17. Pole dada.Fuate uliyoambiwa na utafanikiwa.Ushahuri wangu ni wa kupunguza uzito iwapo wewe nikibonge sasa. Jaribu "LEMON DETOX DIET" na pia "CABBAGE SOUP DIET". Zote mbili fuata moja kwa wakati wake na wala sio zote mbili at the sametime. Utafurahia matukio hasa kwa mapaja yanayo gwarusana. You can google for more details on the two diets. Pole sana

    ReplyDelete
  18. Pole sana mpendwa, mapoja na ushauri woote fuata uliyoambiwa, ila na mimi nakuongezea hii, changanya mafuta ya nazi, mafuta ya mgando na greseline ya maji. Vichanganye vyote kwa pamoja na hakikisha vimechanganyikana sawasawa, ukishanyoa kwapa likiwa halina hata unywele osha kama ulivyoshauriwa na wengine halafu ukishakausha paka huo mchanganyiko wako. Pili kuhusu hayo mapaja yaoshe kwa kwaji ya moto changanya na sabuni ya unga au sabuni yoyote ya maji hasa zile za kuogea chukua brush au kijiwe kilaini usugue kwa utaratibu ukimwagia hayo maji ya mchanganyiko uwe kama unajiloweka kwa muda hata wa nusu saa ukisugu hata na kwapa sugua na kitambaa cha kitaulo, sugua kila siku ukisha ikausha paka huo mchanganyiko. Utakuwa msafiiii sana, Pole mwaya.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad