Kocha wa Manchester United David Moyes ameandika barua ya wazi kwa mashabiki wa klabu hiyo akielezea kwamba msimu wake wa kwanza ndani ya klabu umekuwa mbovu zaidi kuliko ilivyotegemewa.
Akiwasifu mashabiki kwa uvumilivu wao Mscotish huyu ambae aliteuliwa na Sir Alex Ferguson amekiri kwamba matokeo yao mabovu yanamshangaza mpaka yeye lakini ana uhakika kila kitu kitakaa sawa mbeleni.
‘Wakati nilifahamu hii kazi ingekuwa na changamoto nyingi ni wakati nilipopewa jukumu hili, lakini msimu mgumu tulionao hakikuwa kitu ambacho nilikifiria, jambo ambalo nina uhakika mashabiki wote hawakudhani hali ingekuwa hivi,” aliandika Moyes.
‘Wachezaji wangu na makocha wenzangu wanajaribu kwa kila namna kuhakikisha timu inarudi katika kufanya vizuri,
wote tumezoea kuiona Manchester United inayofanikiwa na sapoti mliyowapa wachezaji na mimi katika kipindi chote cha msimu ni kubwa sana’
‘Tunapocheza ugenini mashabiki wetu waliosafiri wameendelea kuwa bora kabisa katika nchi hii na wakati tunapokuwa Old Trafford imani yenu kwenye timu imekuwa ikionekana wazi, kuisapoti timu yenu wakati inashinda ni rahisi lakini ni ngumu sana wakati mambo yanapokuwa mabaya, nyinyi mmekuwa nasi katika kipindi chote’
‘Kila magumu tunayopitia yatatufanya tuwe bora zaidi, timu imara na klabu bora huko mbeleni, kwa miaka mingi sasa mmekuwa mkishuhudia vikosi vya ushindi na kwa muda fulani, nina uhakika kabisa tutaiona Manchester United tuliyoizoea.”
Source:shaffihdauda.com
Moyes ni mbwa,tuachie man u yetu.
ReplyDeleteUngepewa ww hyo timu ungetufanyia nn?
DeleteMech ndo inanza hiv punde.Je ni big match kwetu, tukifungwa najiuzulu ku chek soka bola
ReplyDeleteMan u hoyeeeeeeeeeee! tupen raaahaaaaaa!2 0 kwasasa mwaaaaaa!
ReplyDeleteOraaaaa raaaaha 3 0
ReplyDeleteWAPI,SISI NDO WAPENZI,TUNAJUA HATUSHUKI DARAJA NA HATA TUKASHUKA TUTABAKIA KUWA NI WAPENZI WA MAN.UNITED FOREVER,HIYO KUSHINDWA NI YA MUDA MFUPI TU,KWANI MIAKA MINGAPI TUMESHASHINDA NA MBONA HAMUKUSEMA LOLOTE,HUYU KOCHA BADO NI MPYA, APEWE MUDA AZOEE TIMU NA WACHEZAJI, HONGERA DAVID MOYES,HONGERA MA UNITE
ReplyDelete