PIGO KWA MNYIKA:KUKOSA FURSA NONO KISA HANA SHAHADA

Kwa wale tuliokuwa na nia njema na kijana Mnyika tumekuwa tukitumia juhudi sana kumuasa arudi shule akasome lakini ushauri wetu haukuzingatiwa na mhusika.

kufuatia ukaidi wake huo, leo amehadhirika kwa kukosa nafasi na fursa NONO zaidi kisa tu hana hata stashahada (diploma) ukiachilia mbali shahaba ya kwanza.

Kwa ufupi ni kwamba - ndugu Mnyika alikuwa miongoni mwa wajumbe ambao walitakiwa kuwa wenyeviti wa kamati kwenye bunge la katiba kwa mujibu wa maoni ya wajumbe kadhaa.

Lakini kwa bahati mbaya maoni na mapenzi ya wajumbe hao yaliyeyuka ghafla baada ya maamuzi ya kamati ya kanuni kuweka kigezo cha shahada kama hitaji la kuwa mwenyekiti au makamu mwenyekiti kwenye kamati za bunge maalumu la katiba.

Aidha, juhudi kadhaa zilifanywa na wapenzi wa Mnyika kuweza kukipoteza kigezo cha shahada ili kisimzuie Mnyika kuwa mwenyekiti wa kamati mojawapo ya bunge kati ya 12 zitakazo undwa. 

Lakini jitihada hizo za wapenzi wa Mnyika hazikuzaa matunda hivyo kugonga mwamba baada ya mhe Simbachawene kusisitiza kuwa hitaji la kuwa na shahada ili uwe mwenyekiti wa kamati ni la kisheria. 

Rai yangu: Kama Mnyika kweli ni kichwa kama ambavyo anapambwa na baadhi ya mashabiki wake. Hivi kupata shahada kuna ugumu gani kwake? Si arudi shule ili awe asset kwa taifa kuliko huku kudhalilika kwake kwa kukosa shahada.

"UONGOZI HAUTAKI UJANJA UJANJA"
Source:Jamii Forums
Tags

Post a Comment

43 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hilo nalo neno. Mi binafsi mwakan naanza kutafuta degree. Mnyika rudi shule

    ReplyDelete
    Replies
    1. sitaki kuamini kama mnyika hata kabisa shahada wallah anapiga kelelele tu kumbe hana lolote kasome mnyika kasomeeee shame on u hatutaki mambulula sisi

      Delete
    2. Kazi yake kumfuatilia Zitto kumbe elimu yenyewe ya zumbukula. Kweli ndio maana akina Zitto na Kitila walikuwa na haki ya kusema akili ndogo kuongoza akili kubwa.

      Delete
    3. Kilaza mkubwa.....nenda shule man. Utaishia kumuandama Zitto for nothing. Nenda shule kafute ujinga.......acha umbululaaazzzz.....kinyago weeee......

      Delete
  2. Mwandishi umehongwa kumchafua mnyika, eleza tofauti ya shahada, na stashahada, Kisha Dems mnyika alichonacho ni kilo na alichokikosa kilo mburura wew na jamiiforum ya magamba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuna lolote akasome manina zake sio kuuza sura kideoni tu,ndo maana hata nidhamu ya kawaida tu ya kutofautisha aliekaa darasani na asie kaa darasani jamaa hana.Utii sifuri kumbe bichwa la kuku.

      Delete
    2. Hahahaaa! Dogo anang'arisha sharubu tu pale mjengoni kumbe kichwa box duh! Kweli kua uuaone siyo maghorofa ni mambo kama hayo.....aibu kweli..

      Delete
    3. tofaut ya shahada na stashahada. Shahada ni degree na stashahada ni diploma. Ukienda mbali zaid, kuna shahada ya uzamili ambayo ni masters na shahada ya uzamivu ambayo ni phd

      Delete
    4. We dada inaelekea unajua Kiswahili fasaha,ndo kwanzo hicho Kiswahili nakisikia Leo

      Delete
    5. Nan Huyo Dada umeona sket hapo!

      Delete
  3. Duh!! Kumbe msela maneno kibao hata ka degree hana!! Lakini sishangai hata bowe wake ni ujanjaujanja tu shule hakuna. Wakasome bn ujanja bila shule utakwama tu!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Waliona shahada CCM ni akina Mulugo, ambao wamesoma sana hata hawakumbuki Tanzania ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

      Wenye shahada CCM ni wengi sana, walizipata Bar, hawakusoma hata dibaji ya vitabu ila wana mpaka PhD

      Delete
    2. huyo dada ako mnyika hata hiyo pia hana

      Delete
  4. Hahahahahaaa zumbukuku kijana mdogo,unapata nafasi ya madaraka unashindwa kujiendeleza.Ss hata uko bungeni unatuwakilishaga nn!!!Pumbavu tunaituma mijinga kutuwakilisha maeneo muhimu watz.Tutalia na umaskini hadi mwisho wa dunia tucpobadilika.

    ReplyDelete
    Replies
    1. A point n imeiipenda ipo clear

      Delete
  5. We mwandishi huna cha maana umekaa kichama sana(CCM)historia ya elimu ya mnyika iko wazi.ni kweli hana hiyo stashahada lakini unaelewa kilicho nyuma ya pazia kwanini alifukuzwa UDSM?kwa taarifa yako mnyika ni zaidi hata ya hao maprofessor kiutendaji na kiuelewa na ndio maana yuko juu na anakubalika.kuna watu wamesoma hadi nje ya nchi hii lakini kwenye uongozi hakuna kitu.kama ulikuwa ujui basi naomba tambua philosophy nyingi zinasema KIONGOZI WA UMMA ANAPIMWA KWA MATOKEO YA KAZI YAKE(impacts) NA SIO ELIMU

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tusitetee wajinga jamani,muda anao akasome.

      Delete
    2. Kiukweli mshkaji hamnazo kabisa eti jitu linatetea eti alifukuzwa chuo sasa hiyo ni sifa, acheni mambo hayo hakuna ujanja hapo aende shule anaogopa kuliwa kichwa akasome asilete ujanja ujanja na dogo mbowe naye apokew salam kwa maana wamekaa kiujanja janja hawana busara hata pale mjengoni, nenda shule dogo

      Delete
    3. wapi ufanyiwe itervew bila vyeti wewe acha kuongea umbulula kwa disin hiyo wengi tungekuwa viongozi bila vyeti mnyika akasome tu shwain nyie aache bla bla atamuongozaje prof. ihali yeye ngumbalu, halafu eti mnataka urais urais mchezo kajipangeni upyaaaaaaa

      Delete
  6. huu ni ujinga , yaani sisi wafrica sijui tukoje, sijui lini? watu watawaza kuwajibika badala ya ukipata patumie na ukikosa pajutie, ndio maana sisi wafrica atuendelei kwa ajili ya kutojalai maslhi ya Taifa zima si binafsi, alafu tunsahau kama ni majukumu tu uongozi kama majukumu mengine ya kazi, na tuna tabia ya kuto kufwata sheria, za nchi tulizoziweka zinamuhusu kila mmja wetu, uwe kiongozi, police au raia wa kawaida

    ReplyDelete
  7. Anony 6:20
    Tofauti ya shahada na stashahada: Shahada ni degree kwa kimombo na stashahada ni diploma ambayo yaweza kuwa stashahada ya kawaida-Diploma au stashada ya juu Adv diploma, Sasa kwa mujibu wa mwandishi mh Mnyika hivyo vyote hana na ushauri uliyotolewa kimsingi ni mzuri

    ReplyDelete
  8. Vigogo wengi wamenunua magamba kwanini na yeye asiwe miongoni mwao?mi Nina shemeji yangu mzito serikalini ila kanunua gamba.Anapetaaaa Nani atamjua?

    ReplyDelete
  9. Nape in action

    ReplyDelete
  10. Makamanda Hapo ndo wanapokosea!!! Wanajipahope kuwa SERA ndo inakupeleka bungeni!!! Eti hata umeishia la pili Kama Una sera bc umeliona jengo

    ReplyDelete
  11. mpeni jimbo nape, uyo mnyika arudi shule mwakani akatafute shahada....dah

    ReplyDelete
    Replies
    1. shule bongo!!mbona magige changuduo....

      Delete
  12. Wakina Nshala walifukwaga UDSM miaka hiyo ya 90 enzi za NCCR mageuzi, lakini hakujibweteka, alipigania akarudi chuo akapata shahada yake leo hii ana Phd ya kutoka Havard, kama mtu ni bongo lala alibahatisha kupata nafasi ya chuo akifukuzwa atachekelea na atabaki mtaani na kisingizio cha nilifukuzwa nilifukuzwa, kwani alifukuzwa peke yake

    ReplyDelete
  13. mimi nadhani uongozi ni kipawa,hata kama mtu hana elimu anaweza kuongoza,wangapi wana elimu na hatuoni wanachokkifanya?

    ReplyDelete
  14. Hii mpya.jmn ndio maana zitto hatakiwi kisa elimu leo nimeelewa kabisa

    ReplyDelete
    Replies
    1. si wameona atawapiku wote elimu hawana katika bench lao unategemea nn

      Delete
  15. haya macccmmm yako kila kona, hizo hela za wananchi mnazotumia kuwahonga hawa malimbukeni waaandishi, zitaisha tu na siku moja mtakuwa chali kwa kudra za mwenyenzi Mungu, hata kama hana hata form four cheti, lakini anatufaa, vipi hao mabunge yenu ambayo yanahivyo veti, mpaka sasa hivi wametusaidia nini kama siyo kutufilisi tu watanzania!! ipo siku.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mjipange sana kusoma ndiko kutakapo mkomboa mtanzania na si kingine na ndio maana wazee wanaendelea kuongoza vijana wavivu kusoma kazi yao wanaitaji hela mapema that is the problem halafu wanasema wazee wameng'ang'ania madaraka kwa sababu shule hakuna mnategemea nn watoongoza mpka wanazikwa ee

      Delete
    2. tuwajibike tuache makele,, kila jambo lina wkt wake, angesoma kw bidii angekuwa na vyeti angelikomboa taifa kama kweli ana uchungu nalo, chuo kimemshinda ataweza ya dunia au ndo ujanjaujanja, arudi shule akajifunze adabu

      Delete
  16. Mnyika hana papara atawajibu vizuri tu, nakuwaumbua kwa kuonyesha vyeti vyake

    ReplyDelete
  17. Hii habari imekaa kisiasa sana! mnyika ana masters aloipata UDSM degree alisoma St Augustine Mwanza sasa hao mnaoulizia shahada yake sijui mpo pori gani lenye giza nene!
    Acheni kutumia siasa kuchafua watu

    ReplyDelete
  18. Rafiki yangu hapo sitakuunga mkono kama ni kweli rudi shul haraka maana kuna kazi nyingi 2nawez tukiwa wengi lakini mwenye vyeti vya ju ndie mwenye kazi hapo hamna ujanja.dunia ya shv elimu kwanza mambo mengine badae.LAKINI hapo mks zimeshk mpaka nikuone darasn

    ReplyDelete
  19. Wengi wanacomment humu hawaijui siasa hawana reference wayanayoongea. Sio lazimakucomment kama huna pita tu

    ReplyDelete
  20. Kuwajibika kunaanzia chini(msingi), kama alishindwa kuwajibika akafukuzwa shule, nna wasiwasi hata huku duniani atazingua mda wowote, time will tell.....

    ReplyDelete
  21. nyie macccccmmm jaribuni hata siku moja kusema mnatetea uongozi sababu tumefanya hivi na tunapanga kufanya vile kwenye maendeleo ya nchi, siyo kukaa na majungu tu yasiyokuwa na msingi, wangapi nyie ni maprofesa serikalini lakini hamna kitu!! acheni hizo.

    ReplyDelete
  22. Acheni ushabiki wa kijinga nyie watumwa wa ccm,hamkumbuki enzi za chama kimoja mlivyokuwa mnaiongoza nchi hii kimburula wabunge wengi walikuwa darasa la nne na wengine hata chembe ya darasa hawakuwa nayo,mnacoment bila kumbukumbu ndo maana mnaitwa mamburula. Leo pia wabunge wenu wengi hawana elimu wanaupata kwahela tu

    ReplyDelete
  23. mbona yeye ni waziri kivuli wa wizara ya maji na umwagiliaji na kila uchao anamkosoa Profesa Jumanne Maghembe ni kwa jeuri ipi??

    ReplyDelete
  24. Nyie kaka wa watu ana masters tena ya udsm kpnd mm nipo 2nd year yeye alikuwa anasoma masters acheni uzushi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad