PIGO TAKATIFU LAIKUMBA YANGA....KAMA CHELSEA VILE

KAMA ilivyokuwa kwa Chelsea katika Ligi Kuu ya England juzi kwa kufungwa na kutibuliwa mbio za kuwania taji la nchi hiyo, Yanga jana ilipata pigo kama hilo kutoka kwa Mgambo JKT ya Tanga.

Wakati Chelsea ikilala kwa bao 1-0 kutoka kwa Crystal Palace na kocha wake mbwatukaji, Jose Mourinho akikiri mbio za ubingwa zimekwisha, mabingwa watetezi wa Bara, Yanga jana walichapwa mabao 2-1 na timu hiyo ya Kabuku wilayani Handeni na kuwapa pigo kubwa katika mbio za ubingwa.

Kwa matokeo hayo, Yanga imebakiwa na pointi 46 katika nafasi ya pili huku timu waliyokuwa wakibanana nayo, Azam FC imefikisha pointi 53 baada ya jana kuishinda Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga sasa imebakiwa na mechi nne dhidi ya JKT Ruvu, Kagera Sugar, JKT Oljoro na Simba, ambazo kama ikishinda zote, itafikisha 58 wakati Azam FC imebakiza mechi tatu dhidi ya Ruvu Shooting, Mbeya City na JKT Ruvu ambazo ikishinda zote, itafikisha pointi 62 na kutawazwa bingwa msimu wa 2013/14.

Kwa Yanga, matokeo ya jana kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, ni pigo kubwa kwao kwani sasa inabidi waiombee dua mbaya Azam FC na yenyewe ikihitaji kushinda mechi zilizobaki ili itetee ubingwa.

Mgambo JKT ilikuwa ya kwanza kuandika bao katika dakika ya pili tu lililofungwa na Fully Maganga, ambalo lilidumu hadi mapumziko.

Iliwachukua Yanga dakika nane za kipindi cha pili kusawazisha kwa penalti iliyokwamishwa wavuni na nahodha Nadir Haroub.

Bao lililoipa pigo Yanga lilifungwa kwa penalti katika dakika ya 65 baada ya mwamuzi Alex Mahagi wa Mwanza kuamuru pigo hilo la adhabu kubwa kutokana na beki Kelvin Yondani kumfanyia madhambi Malimi Busungu akielekea kufunga.

Busungu alipiga penalti hiyo na kumfunga kipa Juma Kaseja, na kuandika bao la pili ambalo licha ya juhudi kubwa za Yanga kutaka kusawazisha, hali haikuwa rahisi na hivyo Mgambo JKT kuandika ushindi wake wa pili mkubwa msimu huu, kwani kwenye uwanja huo, waliifunga Simba kwa bao 1-0.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Replies
    1. Mkundu wa marehem bibi yako

      Delete
  2. Yanga wana sikio la kuma lisiosikia mboo wamebebwaa mpaka mwamuzi amechoka

    ReplyDelete
  3. mbeya na azam ndo mwaka wao

    ReplyDelete
  4. simba si vibaya tukawa wa tazamaji

    ReplyDelete
  5. eeeh mtakuwa watazamaji kwa muda mrefu saaaaana mabwege nyie, msubiri mabonanza tu!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad