RAGE ANA POINTI, SIMBA KWELI MAMBUMBUMBU.

Ninaposikia kauli za viongozi wa vilabu vyetu hapa Tanzania, huwa najiuliza maswali mengi sana. Weekend hii umefanyika mkutano wa wanachama wa Simba Sports club katika bwalo la polisi pale Oyster Bay. Katika mkutano huo, mwenyekiti wa sasa wa klabu hiyo alitoa kauli zenye utata kidogo, miongoni mwa kauli zake ilikua hivi, “Simba oyeee…. Mimi sitagombea tena katika uchaguzi ujao, sina njaa, mimi sio masikini…. Hata mkinizomea nasemaje, sina njaa wala si masikini, msiwe kama mambumbumbu”.


Kauli hizi za mwenyekiti wa klabu hii ya simba, zimeibua hoja kadhaa kichwani mwangu ambazo nazitafakari katika makala hii.

Simba Sports Club, timu iliyoanzishwa miaka ya 1930, na kuwa na wapenzi na wanachama wanaokadiriwa kufikia milioni tano (5) kwa ujumla, hadi leo inafanyia mikutano yake kwenye bwalo la polisi.


Simba Sc, miongoni mwa timu zenye umri mkubwa hapa Tanzania, (inakadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 75), ina jengo kariakoo ambalo hata kupata eneo la kuegesha gari ni taabu.

Hadi leo, timu hii iliyowahi kufika makundi ya ligi ya mabingwa Afrika mwaka 2003, haina mkataba na kampuni yoyote ya utengenezaji wa vifaa vya michezo, kama Adidas au Nike wala kampuni yoyote kubwa, bali inategemea vifaa vya mchezo kutoka kwa wadhamini wa ligi.


Hadi leo, pesa za usajili wa wachezaji zinatoka mifukoni mwa watu wachache, na hata mauzo ya wachezaji hao hurudi kwenye akaunti zao binafsi za benki, na hakuna mwanachama mwenye uhalali wa kuhoji matumizi ya fedha hizo. 
i ni baadhi ya hoja nilizonazo kichwani mwangu, ambazo zinaashiria ukweli wa kauli ya mwenyekiti wa Simba, kwamba wanachama wake ni mambumbumbu. Sina maana ya kumtukana wala kumkejeli mtu, ila nia yangu ni kuwafumbua macho wanachama wa Simba, ili kama ni kufanya mabadiliko, basi wakati ndio huu wa kuondokana na kauli za kudhalilishwa kutoka kwa viongozi wao.


Hivi Simba Sc, ni kampuni, ama taasisi, ama biashara ya watu binafsi? Kwa utaratibu uliopo kwasasa, inaashiria kwamba Simba Sc ni taasisi Fulani, inayopata udhamini kutoka kwa wadhamini wa ligi na wadhamini wa timu, ambapo ndani yake inafanyika biashara ya WATU Fulani wachache. 

Mfano mzuri ni pale mwenyekiti wa club hii alipoamua kufanya usajili wa mchezaji mmoja kutoka Zanzibar, na usajili ule ulifanyikia sebuleni kwa mwenyekiti huyu, kwa kumkabidhi kitita cha fedha, wakapiga picha, zikaenea mitandaoni. Endapo mchezaji huyu akiuzwa kwenda timu nyingine kwa kitita kirefu zaidi, ni mwanachama gani mwenye uhalali wa kuhoji matumizi ya pesa za mauzo yake? Maana hakuna mwanachama anayejua pesa za manunuzi yake zilitoka wapi, ndio maana nimesema kwamba ni biashara ya watu binafsi.


Kama Simba Sc ingekua ni kampuni, leo hii mambo yangekua tofauti. Timu ingeweza kujitegemea kiuchumi, ingekua na waajiriwa wa kudumu ambao wangeifanya timu hii kuwa biashara ya kudumu kwa faida ya wanachama na wapenzi wote kwa ujumla na si kwa watu wachache peke yake. Makampuni mbali mbali yangeweza kuwekeza kwenye timu hii kwasababu imani ya matumizi ya pesa ingekuwepo.
 Eliya Rioba.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kasema hana njaa, wala wasiomuone kama anag'ang'ania madaraka akimaliza mda wake hagombei tena, hizi team zetu za bongo ni majungu tu bila kuwa mchawi huwezi ukaziongoza

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad