RIDHIWANI KIKWETE "SIASA NINAZO FANYA HAZINA UHUSIANO NA BABA YANGU"

Chalinze. Mshindi wa kura za maoni za kugombea ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Kikwete amesema siasa anazofanya sasa hazina uhusiano wala ubia na baba yake.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kura za maoni za chama hicho katika jimbo hilo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Msata alisema anafanya siasa kwa maisha yake na si kwa mgongo wa baba yake kwani aliingia katika siasa akiwa na umri wa miaka mitano na hakuwahi kufanya hivyo kwa sababu ya baba yake.

“Siasa ninayofanya haina uhusiano na baba yangu, nafanya siasa kwa maisha yangu na sina ubia na baba yangu katika hili” alisema mtoto huyo wa Rais Jakaya Kikwete.

Akijibu swali la kwa nini amejiingiza katika siasa tofauti na maneno yake aliyowahi kutamka mwaka 2010 kuwa hawezi kushiriki katika kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo hilo, Ridhiwani alisema wakati huo hakuwa tayari.

“Kwenye siasa usiwe muwazi katika kila kitu, ukiwa hivyo unawapa nafasi maadui kukushambulia, mimi hapa Chalinze ni kwetu, kwa wazazi wangu na kule Bagamoyo tunakwenda tu kikazi na ndiyo maana nikaamua kurudi nyumbani kuomba ridhaa. Nashukuru kuongoza katika kura za maoni ninaona ni kiasi gani ninaungwa mkono,” alisema.

Katika kura hizo za maoni Ridhiwani alibuka mshindi kwa kura 758, akifuatiwa na Imani Madega aliyepata kura 335, Ramadhan Maneno (206) na Mkwazu Changwa (17).

Kamati Kuu ya CCM (CC), inatarajiwa kukutana Machi 8, mwaka huu k
Tags

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kama siyo baba tusingekujua!!!

    ReplyDelete
  2. kaza buti dogo ucsikilize maneno ya wachawi, huyo alokomenti hapo juu ni mtoto wa mchawi, piga kazi ukitaka na uraisi umepata, ccm oyeeeeeeeeeee!!!.

    ReplyDelete
  3. oyeeeeeeeeeeee!! mdau hapo juu uko sawa kabsaaaaaaaa! wamuache muremureeeeeee (ccm).

    ReplyDelete
  4. oyeeeeeeeeeeeeeeee!!! mdau hapo juu uko sawa, waliache muvi la ccm liendelee, muremureeeee (ccm).

    ReplyDelete
  5. Kila kitu watafanya kabla Baba hajaondoka kwenye hekalu: Harusi, Ubunge, na menineyo mengi tutayasikia kabla ya uchaguzi.

    ReplyDelete
  6. kwel kabsa mdau

    ReplyDelete
  7. Maji hufata mkondo

    ReplyDelete
  8. Nenda katafune mafweza si wote mafisadi pumbavu zenu

    ReplyDelete
  9. CHADEMA HOYEEEE!!

    ReplyDelete
  10. CHADEMA HOYEEEE!!

    ReplyDelete
  11. Nyote hapo mijinga tu Angalieni nchi ilipo pabaya Deni la Tanzania ni kubwa vijukuu vyetu na vijukuu watalikuta ili deni la mkapa na kikwete mnasifia upumbavu jalibu kuhuliza safari moja ya raisi inatucost kiasi gani na raisi wetu kila kukicha yuko mara Texas au DC just to talk with Tanzania abroad leo mnasema sijui mtoto wake ndio raisi wa kesho nivitu vidogo watanzania inabidi tuviangalie sana sio kwamba hatuvioni

    ReplyDelete
  12. hayo yote taliyosifia hapo juu si MADANGANYIKA!! yapo mengi tu!!!

    ReplyDelete
  13. Rizi1 we nenda kaendeleze libeneke la kuachiana,tena enjoy maisha yako na akikisha na wanao wanagombea, mi shabiki yako hapa migomigo nasubiri kula ugali na mrenda.

    ReplyDelete
  14. Mbona watoto wa mkapa mwinyi jiiiii hata Nyerere .Huyu ridhiwani yaleyale ya North korea

    ReplyDelete
  15. Kutoka Makao Makuu ya Chadema nimepata habari za chereko chereko, nderemo na vifijo kutoka kwa vichaa wa chama hicho wanaoshangilia kwamba wamepata fursa ya kumnanga bwana mkubwa na kumwamika hadharani mapungufu yake kwa kisingizio cha siasa ya uchaguzi.

    Kwa sababu hiyo mie nimetangulia Chalinze kushuhudia majanga ya mkubwa ya kuvuliwa nguo, mkubwa kupashwa mpaka apashike, mkubwa kupewa vipande vyake na hata mkubwa adhaniaye kahitimu siasa kufundishwa siasa ya vyama vingi maana yake nini.

    Nawaarifu wadau wanaonitafuta naondoka Darisalama nami nitapatikana Chalinze kwa kuwa Chalinze ndiko kutakuwa na shughuli ifaayo kushuhudiwa na wote maana “vichaa wa Chadema” wamepania kutangaza siri za bwana mkubwa, vimada wa bwana mkubwa, nyumba ndogo zake, tuhuma na shutuma dhidi yake.

    “Vichaa wa Chadema” ambao baadhi yao ni wabunge, kama Tundu Lissu wa Singida Vijijini, Mchungaji Peter Msigwa wa Iringa Mjini, Ezekiel Wenje wa Nyamagana, Godbless Lema wa Arusha Mjini na Kamanda Sugu wa Mbeya Mjini wanashangilia eti watapata nafasi ya kumsema na kumnanga Kikwete nyumbani kwao Chalinze.

    Nimelazimika kutangulia Chalinze kuwahi nafasi nzuri ya kukaa niweze kuwasikia “vichaa hawa” wakisaidiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chadema, yule sijui Mkira, Munchari au Mnyabasi kutoka Tarime, John Heche na Wilfred Lwakatare wakimpiga vijembe babake mgombea, Jakaya Kikwete.

    Nasikia kikao cha mwisho cha kumteua Ridhwani kitafanyika Jumapili nami ningekuwa na msiri yeyote kikaoni humo ningewashauri wasimteue Ridhwani kwa sababu kumteua Ridhwani ni sawa na kuwapa Chadema penati nao hawawezi kukosoea kupiga penati.

    Ridhwani kama raia mwingine yeyote wa Tanzania anayo haki kuteuliwa kugombea nafasi yoyote ikiwa pamoja na ubunge, lakini kumteua sasa ni kuwapa nafasi Chadema kumkaanga Kikwete na mwanaye na hapo yatasemwa mengi kwenye mikutano ya kampeni.

    Utafurahi kwa mfano kumsikia Tundu Lissu akimsimulia jinsi Ridhwani alivyofanya mazoezi ya uanasheria wenyewe wanaita externship zamani iliitwa internship katika kampuni moja ya mawakili jijini Dar es Salaam.
    Atasema jinsi kampuni hiyo ilivyoanzisha kampuni ya kitapeli au ya wizi na kukomba mabilioni ya shilingi wakati wa kampeni za Kikwete.

    Utafurahi pia kumsika Mchungaji Msigwa akielezea jinsi Ridhwani alivyoitisha kikao cha viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM nyumbani kwao Bagamoyo na katika kikao hicho Ridhwani akatangaza kwamba rais ajaye hatatoka Kaskazini kwa maana ya mikoa ya Ausha, Manyara na Tanga.

    Utafurahi vilevile atakapoinuka mkutanoni Bwana Heche au Sugu au Lema au Wenje na kukumbushia jinsi alivyojitokeza aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Frederick Sumaye, na kukanusha kuwa CCM anayoifahamu yeye haina utaratibu wa kufahamu rais ajaye atatoka kanda gani.

    Utafurahi kumsikia Wilfred Lwakatare ataposimama na kusimulia jinsi kiongozi wa nchi, Kikwete, alipokiuka sheria zote na katiba nzima ya Jamhuri, kwa kuwasamehe wezi wa EPA.

    Huenda vilevile akasimama Lema Wenje akasema mkutanoni kwenye kampeni na kuhoji ni wapi Rais wa nchi alipokutana na wezi wale wa EPA. Je, ni nyumbani kwake, yaani nyumba ile aliyopewa bure eti kanunua nyumba ya serikali? Au walikutana hotelini?

    Kiongozi wa nchi anakutana na wezi kuwaomba warudishe pesa walizoiba badala ya kutumia na kufuata sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ambayo inaelekeza mtuhumiwa wa wizi kama EPA atahudumiwaje – atakamatwa, atawekwa ndani, atapepelezwa, atashitakiwa na kufungwa ushahidi ukitimia. Lakini EPA watatendewa kama maofisa wa kibalozi.

    Nasema lazima nihudhurie kampeni hizo za Chalinze niwasikie wanasiasa machachari wa Chadema wakiwavua nguo viongozi wa CCM na hasa rais Kikwete kwa vile mwanaye atakuwa anawania ubunge wa jimbo hilo.

    Ndiyo maana nawashauri wenye kuweza kutoa ushauri wamshauri Kikwete na mwanaye Ridhwani waachane na ubunge wa Chalinze kwa sababu matokeo yake yatakuwa makubwa huku vichaa wa Chadema wakipata uwanja halali wa kumchafua kiongozi wa nchi.

    Mwenye hamu kama mie na anifuate Chalinze tushuhudie uhondo wa kashafa halali mikutanoni kwenye kampeni Chalinze.


    mwisho

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad