TAARIFA ZA HABARI ZA TANZANIA HAZINA MVUTO KABISA JAMANI...BADILIKENI

Nilishaliongelea hilo kwenye post zilizopita nikilinganisha na Habari za TV za Kenya....sasa Bongo5 nao wameliongelea swala hilo kama ifuatavyo:

"Habari nyingi kwenye TV za kibongo hazina mvuto. Unaweza kufurahia kuangalia habari labda kama siku hiyo kuna ajali kubwa imetokea, bungeni kumeumana ama siku Barack Obama akirudi tena Bongo. Kusipokuwa na matukio ya kuvutia yaliyopo tayari, taarifa za habari kwenye TV zetu zinaboa si kidogo.
Watakujazia habari za mikutano, semina, warsha na mikutano na waandishi wa habari ambazo hazivutii hata chembe. Zinaweza kuwa na vigezo vya kuitwa ‘news’ lakini hizi si habari unazoweza kuziona kwenye TV za watu wanaojielewa. Hizi ni habari za kupoteza muda tu na wala hazina ‘impact’ yoyote kwa wananchi.
Nafahamu mazingira ya kufanya kazi kwenye TV za Tanzania na ninalo jibu la uhakika la kwanini habari za semina, warsha au press conference ndizo zinazotawala line-up ya habari kwenye vituo vyetu. Sababu kubwa ni kwamba waandishi wengi wa habari wanalipwa ujira mdogo mno na hivyo ili kujikimu kimaisha inabidi wafanye zaidi story za warsha na mikutano ambazo huwapa posho za hapa na pale.
Hiyo ina maana kuwa waandishi wengi wa habari hawana muda wa kuandika habari za kuvutia zinazohitaji ubunifu zaidi, muda wa kutosha na ‘mnuso wa habari’ (nose for news). Wamiliki wa vyombo vya habari wanahitaji kuwekeza zaidi katika kuwalipa vizuri waandishi wanaokusanya habari zao, kuwa na usafiri wa kuaminika na kuwa na wahariri wabunifu wenye uwezo wa kujua habari zenye mvuto, zenye impact na zilizoandikwa kwa kina.
Taarifa za habari pia zinatakiwa kuhusisha wataalam ama wachambuzi wa masuala mbalimbali kutilia mkazo ripoti husika. Mashirika makubwa ya habari ya kimataifa hupenda kutumiza ‘contributors’ mbalimbali ambao huhusika katika uchambuzi wa masuala ya siasa, biashara na uchumi, masuala ya jamii pamoja na michezo na burudani.
Kwa kutumia watu hawa, habari hupanuliwa zaidi na kuzungumzwa katika mtazamo mpana.
Kwa mfano, weekend hii Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amedai kuwa bara la Afrika halimtendei haki Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama mtu muhimu kwenye harakati za ukombozi wa Afrika kutoka kwa wakoloni. Hii ni habari ambayo inaweza kuripotiwa kwenye taarifa za habari katika TV za Tanzania kwa kuichambua zaidi kwa kuhusisha wazee na viongozi wa zamani watakaotoa maoni yao kutokana na kauli hii, viongozi wa juu wa Tanzania na hata wasomi wa vyuo vikuu kuipa wigo zaidi.
Kwa ufupi, matatizo makubwa kwenye taarifa za habari kwenye vituo vyetu vya runinga ni pamoja na:
Habari nyingi hazivutii
Wasomaji wengi wa habari hawana mvuto na hawavalishwi vizuri
Muonekano na uwasilishaji wa habari ni wa kawaida
Hakuna habari za kina na zenye uchambuzi
Habari si za kutafuta, nyingi ni za matukio ya kuandaliwa
Hakuna matumizi ya wataalam katika fani mbalimbali
Uandishi wa script hautumii maneno yenye kuvuta usikivu wa watu au matumizi ya lugha ya macho
Matumizi ya ripota wanaotumia simu za mkononi
Wasomaji wa habari hawategenezwi kuwa ‘TV personalities’ kama ilivyo Kenya ambako wamezaliwa watu maarufu na wenye ushawishi wakiwemo Julie Gichuru, Kanze Dena na Lulu Hassan au Swaleh Mdoe wa Citizen TV au Larry Madowo wa NTV na wengine
Habari zinakuwa serious mno na kusahau upande wa ‘humor’
Uandishi wa habari unachukuliwa kama taaluma kupitiliza na kusahau kuwa uandishi pia ni sanaa inayohitaji ubunifu kama uandishi wa vitabu au utunzi wa mashairi yenye mvuto
Waandishi wa habari na maripota wa TV ambao wako chini ya wahariri, wanatakiwa kuanza kufikiria nje ya box na kutafuta habari za maana na kuondokana na uandishi uliozoeleka wa‘Madiwani wa kata ya ‘Mti Mkavu’ wametakiwa kuwa waadilifu katika kazi yao’ ‘Ama mbunge wa Kilimabubu ameweka jiwe la msingi kwenye shule ya Mnazi Mchungu’.
Watazame aina ya habari wenzetu huziandika ambazo huwa na mvuto, zimechambuliwa vizuri, zimetumia vyanzo vya kutosha na uandishi wa script wenye maneno matamu"
Bongo5

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. dah! hata mimi ameweza kunishawishi, ni kweli aisee, nimejikuta siku hizi sipendi kufuatilia habari kwenye tv. japo sikujua kwanini. ni kweli hazina mvuto, wako juujuu mno.

    ReplyDelete
  2. A realy professional write Up,Waandishi wabongo wanatakiwa wajue kwamba si kila tukio ni habari. Hivi watu wameenda shule kweli??..wanazijua News values?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli kbs! Ukianzia kivaa hawajui! Wakisoma taarifa inakuwa fupi sn! Hawako smart!!! Sisi tunaangalia CITZEN ya Kenya"

      Delete
    2. Ingawaje hatupo kenya hata mimi naangalia Citizen Kenya swahili news na english zote utazani cnn africa sasa ukirudi Itv.
      Channel 10 au Tbc uyadhani unaangalia zile tv za box tulizokua tunatengeza tulikua wadogo duuu halafu wadada kama wa tbc bomu kbs tv is also abt personality uzuri wa mtangazi awe mwanamme au mwanamke

      Delete
  3. Tukubali bongo hakuna creativity watu wanasoma wanakariri vyuoni wakitoka hapo kwenye tv. kwanza ni lazima wachague waandishi wenye mvuto sio wale wanaotangaza redioni ndio wanahamia kwenye tv. fungu la pesa liwe la kutosha.waajiri mpaka costume designer.make up artist.professional cameramen.editors.

    ReplyDelete
  4. Yan wawe na watu special Wa kusoma taarifa ya Habari! Wawe wenye MVUTO! Smart! Wenye meno mazuri yaliokaa kwenye mpangilio! MIMI Nashangaa sn UTAKUTA MTU chini Kavaa jeans juu anatupia koti! Kwa ajili anakaa kwenye mmeza Utafikiri kwenye bucha!!! Wasimame Kama Kenya!

    ReplyDelete
  5. Sijawahi coment chochote ila leo umenigusa.siku hizi me naangalia CITIZEN ya kenya na huko kenya sijawahi hata fika.watangazaji wako smart wana ufahamu mkubwa wa vitu vingi na habari zinavutia.tv zetu nina miezi sijawahi hata angalia.taarifa hazivutii wanangazaji kama vile wanashikiwa bastola too much serious jamani hawajui vitu vingi.me nlijua ni mimi mwenyewe kumbe tuko wengi.tubadilike.citzen tv ni nzuri jamani atangaze shwale mdoe aseme juzi nlikuwa kwa babu.....ah usipime.au lulu kipindi kile cha uchaguzi...du hadi raha.tubadilike tz

    ReplyDelete
  6. hazina mvuto wala maana, ndiyo maana hata sijishughulishi kuziangalia, utakuta wanazungumza topic fulani bila kuirudia vizuri, ikishapita imepita kweli inabidi wachangamke

    ReplyDelete
  7. Hahahahaa naomba samahani then naomba nichangie kitu....
    Matukio yanayoonyeshwa na vituo vya habari nchini hutokana na sisi wenyewe so huwa vinagusa jamiii fulani
    Kuna vitu vingi vimekuwa vikipatiwa ufumbuzi kupitia taarifa za habari.
    Tusitake kuiga vitu visivyo na maana kwetu...waacheni watangaze kile walicho kiona alimradi kiwe kinagusa jamii fulanii..

    ReplyDelete
  8. Ht design ya stage haivutii,colour Nixon pia tatizo,maana unaona ukungu tu.......kenyans are really creative.....bila shaka EATV wana wakenya,kidogo show Sao zina mvuto but not so sure......

    ReplyDelete
  9. Mbunge wa Kinga, amewashauri kina mama kujitegemea na kupeleka watoto kwenye chanjo. Aliyasema hayo alipokuwa akikabidhi baiskeli 3 kwa madiwani wa ikombe.

    Hizo ndizo habari zetu. Total waste of air and time. True our media lacks substance

    ReplyDelete
    Replies
    1. Eti nini..umenivunja mbavu.ukweli mtupu.tz baaadooo sana.huwezi fananisha na CITIZEN ya kenya.mh wadada wanaotangaza no mvutoo at all

      Delete
  10. Yani wengine waleta kutuonyesha makeup zao na suti zao za mr price. Hata alama za usomaji hawajui kuzizingatia wakat wanasoma. Wapo kama machiriku. Mafuriko wanasema mafriko. Kweli jamani kina jaki kombe mweee no mvuto

    ReplyDelete
  11. Wengi hajasomea ni kujuana

    ReplyDelete
  12. Kaletwa na mjomba sasa afanyeje?waachen wauze sura

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad