TUNDU LISSU:SITTA ANANITONESHA VIDONDA

Mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu amesema ktendo cha Mwenyekiti wa Bunge la Katiba kubadilisha kanuni kwa kutoa muda zaidi wa kuwasilishwa kwa rasimu ya katiba, kinamkera.

Lissu alisema kitendo kama hicho ndicho kilichomfanya yeye na mjumbe mwenzake, Ismail Jussa kutaka kujiuzulu mara mbili kutokana na kupingana na wajumbe wenzao.

Akizungumza na gazeti hili jana mjini hapa, Lissu alisema walitaka kujiuzulu kutokana na kuchoshwa na wajumbe kufikia makubaliano ndani ya vikao, lakini wakitoka nje wanarudi na mabadiliko.

“Tulikuwa hatusongi mbele tunafanya uamuzi na kufikia makubalino, lakini wenzetu baadaye wanaenda kujadiliana upya na kuja na mapendekezo tofauti na kuturudisha nyuma,” alisema Lissu.

“Baada ya majadiliano yao, mimi na Jussa tuliomba tujiondoe lakini walituomba tusijiuzulu kwa masharti kuwa tunachokubaliana  hawataweza kubadilisha.”

Alisema kile ambacho kimeanza kutokea sasa ni kitendo cha Mwenyekiti Sitta kubadilisha kanuni ya 47 (a) ya Bunge hilo juu ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kupewa muda unaofaa kuwasilisha rasimu katika Bunge Maalumu la Katiba.

Lissu,  ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), alisema pia hata kubadilisha kanuni kwa kupokea kwanza taarifa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na baadaye ndipo Rais Jakaya Kikwete azungumze ni jambo wanalolipinga.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Endeleeni kujitengenezea mazingira mazur na family zenu, ss yetu macho tu ila tunaomba msituvurugie amani yetu ndan ya nchii hii

    ReplyDelete
  2. Lisu safi sana komaa nao...

    ReplyDelete
    Replies
    1. unajua kuwa amani ni tunu ya taifa letu?

      Delete
  3. lisu umetoneshwa wp, acha maneno mingi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad